Watu weusi ndio walivuka bahari kuu na kufanya ustaarabu kote Asia na Ulaya

Watu weusi ndio walivuka bahari kuu na kufanya ustaarabu kote Asia na Ulaya

497010a3116f128cb9d4d765657c319e.jpg
Asante Sana
 
hizo empire za kushindana kuwa na wake wengi na ng'ombe wengi na biashara kubwa ilikuwa chumvi za kuzoa ufukweni kama wanavyofanya Watu wa mwambao wa bahari hata leo na kutengeneza mikuki kama wanavyofanya Wamang'ati wa kule bonde la Eyasi. lakini kamwe hawakuwa na uwezo hata wa kutengeza redio wala baiskeli hadi Wazungu wanakuja kuwaangusha.
Kwahiyo unaamini kwamba, mikuki, majembe, majahazi, nguo zote ni mazao ya wageni Afrika? Hapana, tumepitia yote waliyo yapitia wao, ili tu lingetosha kudhihirisha kwamba, weusi ni watu, watu walio kamili, hivyo wangeweza kuyafanya yote ambayo wengine wameyafanya. Naamini yaliyo nenwa na mleta Uzi ni ya kweli na yalishatukia.

Tunaambiwa hata Simon wa Krene alikuwa ni black. Muungiliano lazima ulikuwepo.
 
Mbali sana huko, Mirambo na Mkwawa hawajui? Walitawala watu ktk mifumo iliyo hitaji elimu na maarifa makubwa. Inasemekana hata chuo kikuu cha kwanza kuwepo ulimwenguni, kilikuwepo Afrika. Kuna mengi nadhani bado hayajulikani vizuri kutuhusu.

Nawapongeza wote wenye kuyafatilia haya mambo, mapinduzi ya kweli yanaanzia kwenye ufalme wa "ubongo" na si vinginevyo. Nadhani tuko ktk mwanzo mpya.
Asante ndugu, polepole tutafika, kung'oa misumari na miiba hii dhalimu waliyotuchoma
 
Tunaambiwa hata Simon wa Krene alikuwa ni black. Muungiliano lazima ulikuwepo.
ndo maana alishurutishwa kuubeba ule Msalaba. Angekuwa Mzungu asingelazimishwa kuubeba msalaba wa Yesu. Hiyo pia inadhihirisha kuwa tulikuwa nyuma ya wenzetu miaka mingi sana. Tuamke, tupambane, tuache kulalamika kuwa tulionewa. Sisi ndo tumejionea wenyewe. tupambane tusonge mbele waliko wenzetu.
 
Kuna swali huwa najiuliza kulingana na hizi mada zinazompa nguvu myu mweusi. Kama kweli tulikuwa advanced kiasi hicho how come tupo dependent na inferior kwa ngozi nyeupe.?
Kuwa mstaarabu ina maana hata uwezo wako wa kufikiri ni mzuri so ina maana tulishindwa kufikiria kama inawezekana race nyingine inaweza kutufanyia hila kwa kuwa tumewazidi? Hivyo tukaweka mikakati ambayo ingetufanya kuikabili hila hizo zilizofanywa na mtu mweupe zidi yetu?
Hawa watu weupe walipokuja kuchukua malighafi ina maana kwa wakati huo hatukuwa tunajua uthamani wa malighafi hizo?
Histori ya darasani tunaambiwa tikuwa tunachezea bao dhahabu na vito vingine vya thamani, kweli hatukujua uthamani wa vito hivyo mpaka mtu mweupe anakuja kuchukua kwa kutubadilishia na vijiko na vitu vingine vya kipuuzi???
Tutasema tuligundua hili mara lile..je wakati hawa watu weupe wanafanya hiyo mikakati yao ya kutufanya tuwe inferior kwao tangu walipoanza hiyo miaka 500 iliyopita...je mtu mweusi alikuwa anafanya nini na ameshindwa vipi kujipanga na yeye ndie akawa superior kwa ngozi nyeupe tangu hiyo miaka 500 iliyopita???
Asante, tutayajibu maswali yako mazuri polepole
 
Maelfu ya miaka watu weusi walikwenda bara Asia na Ulaya na kufanya ustaarabu huko, mtu mweusi ndiye aliyestaarabisha Dunia, uliyofundishwa darasani Ni historia changa mno, Tena ya karibu mno, mtu mweusi hujitambui, ungelijijua wewe....!!!!!! Dunia itatikisika

The British, with the "Modern" Germans, were the originators of revisionist history. It was they who first began to write Blacks out of history after the “Race/Religious Wars" of the late medieval. Now look, the British will soon start teaching their children the truth: that Blacks were the original people of Britain. But please know, this is not the result of truth seeking, those truths were always known[/QUOTEk


kifaa cha mwanzo cha ustarabu ni elimu(ilm)na mwafrika hakua nayo-tuanzie hapo!!!
 
Tatizo wewe ni mbishi na hautaki kujua,nani amekwambia hawakuvuka nje kwenda kusaka makazi sehemu nyingine?soma kaka,soma historia tena si hyo ya kina Nyambari Nyangwine na Major Events.Hyo Spain unavyiona hapo ishatawaliwa na weusi kwa miaka mingi tu,Columbus alivyofika Marekani alikuta tayari kuna weusi walishafika kitambo,Australia yenyewe waingereza waliikuta na weusi ndio nchi yao,visiwa vya Papua New Guinea wapo weusi.

Nikuulize swali,hivi kwanini kwenye kila lugha ya asili kwa makabila yote kuna maneno ambayo ukiyatafsiri maana yake ni "soma" na "andika", sasa haya maneno walikua wanayatumia wapi kama shule zililetwa na hao wazungu wako?

Daah katika kuhakikisha white supremacy inatawala na African inferiority inajikita vizazi mpaka vizazi wazungu wamefanikiwa sana.
Asante ndugu
 
Tatizo la haya maneno cjawahi ona solid evidence kuthibitisha haya....najiuliza maandishi yap haswa ni waafrica kwa asili...kwa michoro ya kondoa irangi na mingine tunajenga hoja gani...mimi ni mtanzania na napenda kuwa mtanzani mweusi ...ni seme ni mbaguzi wa rangi pia ndani ya moyo wangu haswa ninapoona mweusi anashindwa na mzungu mf. mpira so nadhani kama ningekua na mamlaka baadhi ya maamuzi yangu yangeamua kwa rangi black first.....lakini nimeishi na wazungu wengi wanatabia tu kama za watu wa mbagala rangi tatu na wakati mwingine wachafu zaidi ya hapo...kunya ovyo..kula ovyo..kutokuoga na mengine...kusema kweli kuna vitu vingi sana wazungu wametuzidi kutokana na maisha ya sasa yalivyo (ukisasa) ni maisha yao ya kila siku yaliyopo africa pia mf..namna mzungu anavyokula, maamuzi yao...uvaaji wao..maongezi...hata jinsi tu ya kufunga kamba za kiatu ni kama wako more advance kuliko sisi...nao pia tukiwa katika maisha yetu halisi tumewazidi mf.kukata majani kwa panga, kuchinja mbuzi, kula ugali na vingine kwa mikono,..kazi nyingi za mikono zisizo na machine wabongo tupo vizuri......so kusema waafrica ndio tulikua the first ni kama uzushi flani hivi bila kuwa na evidence kuna vitu kama akili ni nature tu hata ufanyweje zinabaki...lakini nikiangalia hata wamasai na kabila nyingine za kibantu nyingi huoni huo uhalisia wa kuwa waliku vizuri kuliko wazungu......natamani watokee watu wanye uwezo wa kuthibitisha huo ukweli na watuambie tulipotelea wapi....ntakuwa mbaguzi plus now.
 
Tupambane kujiletea maendeleo. Historia haiwezi kutusaidia kitu. Hizo ni zilipendwa.
Kama tulistaarabika tulijizua vip kutokuchuliwa utumwani,unakuta mtu mmoja ana bunduki anaswaga makundi ya watu porini,MTU anatumwa apeleke barua kwa DC kilometer 40 akifika DC anaisoma barua kumbe barua inamtaka muhusika awekwe ndani au alambwe viboko.Kulikuwa na magwiji wa waganga na walozi wa hali ya juu,lkn walishindwa kuzuia utumwa hadi ulipositishwa na waliouleta baada ya uvumbuzi wa machine,hata Uhuru walitupa wao baada ya kuona kutawala direct ni gharama wakatupa Uhuru bandia kupitia kwa wakoloni weusi ili watunyonye wakishirikiana na wakoloni weusi, ndo maana miaka 50 ndani ya kujitawala Africa hakuna maendeleo, wakati wakoloni weupe walitawala mda mfupi kuliko tulioupata baada ya Uhuru lkn walileta maendeleo yanayoonekana,ikiwemo miji, miundombinu,mashule,nk.Mkoloni mpya kwa Africa ni China kupitia mkoloni mweusi ambae ndo mnufaika mkubwa kwa sasa wa raslimali za africa, kwake tutegemee tu kuiweka Africa bond km ilivo Bandari ya Malaysia na Srilanka.
 
Tatizo ni anguko la ustaarabu wa kiafrika.!

'Hapana' sio kwa kiwango hiki..!?

Tembo hakondi kufikia kiwango cha Mbuzi.

Ni Uongo mtupu na
Kutafuta Huruma.
Ndio nyinyi tukiwaita mrudi kwenye ibada yenu asilia mnaanza yesu yesu, muhamadi muhamadi!!!! Ndio watu Kama nyinyi mnatukwamisha.....lakini tutajikomboa tu
 
this is also a falacy. Kama mtu mweusi ndiye asili ya ustaarabu na maendeleo duniani alipatwa na nini leo tuko hivi. ustaarabu ziro kabisa. ukija huku mijini kama Dar es Salaam wanakunya hadi kwenye mifuko ya Malboro na kutupa jalalani. Tusijikweze sana na kutafuta huruma ya dunia. Sisi watu weusi tumechelewa sana kuzinduka. kama ni evolution basi ilianzia kwa watu weupe, wakafuta wengine kama Wahindi, Waarabu n.k ndo tunafuata sisi wa mwisho. Wakati wenzetu walishafikia hadi hatua ya kuwa na magari, meli na hata kuzindua ndege sisi bado tulikuwa hatuvai hata nguo. tusijidanganye sana kwamba tulikuwa mbele zamani wakati ni dhana ya uwongo iliyokubuhu. Tuache kutafuta kuhurumiwa, tupambane hali zetu.
nilijua tu fikra fupi hamuishagi
 
hizo falsafa tu. jana mbovu haiwezi kukusaidia kusonga mbele. Jana yetu ilikuwa mbovu ndo maana tupo nyuma, hivyo hatuna cha kujifunza kutoka jana yetu. Tupambane kusonga mbele.
Ndio nyinyi tukiwaita mrudi kwenye ibada yenu asilia mnaanza yesu yesu, muhamadi muhamadi!!!! Ndio watu Kama nyinyi mnatukwamisha.....lakini tutajikomboa tu
 
Back
Top Bottom