Asili ya kitu ni asili aifutiki iko damuni,mfano kuna matajiri wengi tu Nyerere aliwafilisi kwa sera zake za kimasikini za utaifishaji na kuwasakama matajiri wa kuwanyang'anya Mali zao halali walizotafuta kihalali hata kabla ya Uhuru,na kuwafanya kuwa masikini, alipoingia Mzee ruksa akatupilia mbali sera za kuzalisha masikini, kwa kuruhusu sekta binafsi asilimia kubwa wale waliozulumiwa mali zao kwa kutaifishiwa wakiwa hawana kitu lkn wana ujuzi wa kutafuta Mali, walifanikiwa wakawa matajiri zaid, kuliko hata mali zao zilizotaifishwa.Hivo km hao Waafrica wa mwanzo wangekuwa wameendelea hata Leo tungekuwa mbali sana baada ya Uhuru km iliyo Malaysia, Singapore,nchi za Scandinavian, China ambazo Africa ilikuwa sawa kiuchumi baada ya Uhuru. Rejea thamani ya dola kabla na sasa baada ya Uhuru.