Watu weusi ndio walivuka bahari kuu na kufanya ustaarabu kote Asia na Ulaya

Watu weusi ndio walivuka bahari kuu na kufanya ustaarabu kote Asia na Ulaya

Sasa inakuwaje Afrika inaitwa shithole?
Wamekuchezea akili sisi Ni goldhole
Cartoon_2.jpg
 
Wengi au labda wote, tunajua kuhusu historia, hutolewa kutoka vyombo vya habari vya White - aina moja au nyingine. Kwa maana kwamba hiyo tunaita historia leo ni maandiko ya wagiriki, warumi na waarabu, tengenezo la vyombo vya habari vya White ni kuwafurahisha na kufariji watazamaji weupe , sio kuwashawishi mtu yeyote. Baada ya yote, ni kiini macho. Kwa hiyo kwanza kabisa, hebu tufafanue ni nini REAL, na ni nini fantasy
 
ndo maana alishurutishwa kuubeba ule Msalaba. Angekuwa Mzungu asingelazimishwa kuubeba msalaba wa Yesu. Hiyo pia inadhihirisha kuwa tulikuwa nyuma ya wenzetu miaka mingi sana. Tuamke, tupambane, tuache kulalamika kuwa tulionewa. Sisi ndo tumejionea wenyewe. tupambane tusonge mbele waliko wenzetu.
Pia inadhihirisha kwamba blacks walisha kuwa na maingiliano na falme za mbali hapo zamani hata kabla yao kuja kwetu. Australia ina wakazi wa asili ambao ni ma blacks, pia inasemekana walitoka Afrika miaka 50000 kabla ya Yesu.

Huyo Simon ni baada ya kuanguka nadhani. Imani ya kiislamu ina mwingine kwa jina la Lukumani.
 
Historia inatuambia kuwa columbus na Henry the navigator Ndiyo binadamu walio gundua merikebu, lakini tangu kipindi cha nabii yona merikebu zilikuwepo. Hapa inaonyesha kuwa kuna kipindi teknologia ilipotea. Mpaka baadaye Henry the navigator anagundua tena merikebu.
kule misri wakati kunajengwa pyramid chambo cha usafirishaji nilikuwa ngarawa
walikuwa wanatoa mawe upande mmoja wa MTO hadi upande mwingine
 
Unaifahamu vizuri kingdom ya mali enzi za mansa mussa? Na chuo kikuu cha kwanza inasadikika kilikuwa Timbuktu. Ndiyo maana hadi leo france anapiganisha makombola na kumaliza kabisa shahidi hizi za kihistoria.
Unajua sababu ya kurise kwa Mali empire? (sio kingdom)

Hicho chuo kikuu cha Timbuktu unadhani kilikuwa na status gani, course zipi, mitaala ipi na wakufunzi wapi labda?
 
Mkuu figisu alizochezewa mtu mweusi hazijafanyika ndani ya mwaka au miaka 10,ni zaidi ya miaka 500.
Waafrika jamani tutafute historia halisi ya Waafrika iliyoandikwa bila bias yoyote.

Sasa unafikiria uvamizi uliofanywa,uporoji wa mali asili na nguvu kazi,uharibifu wa ujuzi/elimu ya mwafrika,ufutaji wa utamaduni wetu,upandikizaji wa mfumo wa elimu usioendana na mazingira yote ya Kiafrika,ukoloni rasmi,ukoloni mambo leo,ubaguzi wa rangi unafikiri madhila haya yote yanaweza yakafanya mtu kusimama katika ukuu wake?Kwa msaada zaidi kama unataka kujua tafuta kitabu cha mwanahistoria nguli wa Kisenegali,anaitwa Cheikh Anta Diop kinaitwa,African Origin of Civilization, Myth or Reality. Bwana Diop alikuwepo kwenye mkutano maarufu wa UNESCO miaka ya 70 iliokua unajadili asili ya watu wa Misri ya kale,huyu bwana aliwashinda Wazungu pale alipothibitisha hoja kua lugha ya Wamisri wa kale ilikua inashabihiana sana na lugha ya kabila huko Senegali hivyo basi hao Wamisri wa kale walikua ni watu wenye asili ya weusi.Kwa maana hiyo Wamisri asili[Achana na hawa waarab unaowaona sasahivi ambao walikuja hapo baada ya Misri kutekwa na Waroma,baadae Wagiriki na ndio wakaja Ottomans(waarab)] ndio waliwafundisha akina Plato na Aristotle hiyo philosophia wanaosemekana wao ndio wababa .
Asante
 
Back
Top Bottom