Watu wote mnaomuamini Mungu mje, nina swali kwenu 😢

Sasa utakuwa na 'muhu' ya kutazama ya wengine wakati ya kwako tu menyewe mazito ya kushindwa kupepesa hata macho, utakuwa na ubavu?
 
So watoto wote wanaofia tumboni au wale wanazaliwa na magonjwa kama kansa, sababu ni mama zao kutotunza mimba vizuri?
Anyway tufanye hiyo kansa wamepewa na mungu na kufia tumboni ni mungu kawauwa🤣🤣🤣
 
Aliyekuambia watoto hawana hatia ni nani mkuu?
 
Sasa utakuwa na 'muhu' ya kutazama ya wengine wakati ya kwako tu menyewe mazito ya kushindwa kupepesa hata macho, utakuwa na ubavu?
Ndo binadam ndivyo alivyo mkuu.Wengi tu hata hapa duniani wanashida zao ila wanaangalia na kufatilia maisha ya wenzao badala ya kuangalia maisha yao. So, hawa wanaofatilia maisha ya wenzao wao hawana yakwao?? Ndo itakavyokuwa huko siku ya hukumu mkuu, tutakuwa tunacheck matendo yako ya sirini Live😄
 
MUNGU YUPO TU KICHWANI MWA WAJINGA, NA SI MAHALA PEMGINE POPOTE. KWA LUGHA NYEPESI MUNGU ANAUMBWA NA UBONGO WA MTU KILAZA ILA YEYE KAMA HAYUPO KIUHALISIA.
 
Ashakum si matusi:

Kuuliza kwanini Mungu anaacha watu wafe ni sawa na mtoto kuuliza kwanini watu wote hapo nyumbani hawamsaidii mama yake kutoka humo chumbani anapolala na baba yake maana anateseka humo kila siku usiku anamsikia mama analia! ! Tena anasikiaga na vishindo! !

Personally nawaonea wivu sana waliokufa, tena watoto ndo kabisa they get a free pass.

They're at the best place they could ever be, why do you weap for them? ? ? Unafikiri wamepoteza?

"Nimewaambia mambo ya duniani, nanyi hamkuniamini, mtaniaminije basi nitakapowaambia mambo ya mbinguni?"
Yohana.3.12.NENO


Mimi kama kuna kitu natamani kuwa na Mungu.


Wataalam wa ku invest / kubet mnaiitaje hii, yani you beleive on the best possible outcome on whatever you're putting.

Naamini kabisa kwa Mungu is the best possible world anyone could ever want to be, kiasi kwamba wewe kumuonea huruma mtu ambaye yupo kule ni roho ovu / chafu at work! ! Yani kwanini uwe huko usiwe huku uchomwe na jua upigwe na baridi kali uumwe, uumizwe na watu, uone maovu yakitendeka....


This is not to mean nataka kujiua or ni sawa kuua. Mradi niko hai leo, lengo la Mungu aliyenifanya nikawepo ni mimi niwepo hapa duniani. Ni mtu kujiuliza lengo la MUNGU ni nini juu yakE?

Utalalamika huna hiki huna kile, una hiki kibaya kile kibaya, unajua lengo la Mungu la wewe kuwa hivyo? ? ?

"Yesu akawajibu, “Huyu mtu wala wazazi wake hawakutenda dhambi. Alizaliwa kipofu ili kazi za Mungu zidhihirishwe katika maisha yake."
Yohana.9.3.NENO

Ndomana tunaambiwa tushukuru kwa kila jambo. Mwisho wa siku kila kitu kiko katika uangalizi wake. Anaona kila kitu. Ana kusudi lake na kila alichokiumba. Chochote kibaya alichoacha kitokee kaacha kwa makusudi yake.

Mfano one of the worst things that I have a hard time even thinking about ni wanaobaka watoto, yani hadi vichanga seriously! Sasa hawa wabaka watoto huku mtaani hawana alama, hata hapa JF wapo na usikute wanakubalika kwerikweri, huku kwenye mwanga kila mtu ni kama ana akili timamu, kavaa vizuri ana kazi ana mali tena ukute tajiri kama matajiri wa Epstein, tena ana mke na watoto kabisa, yani ana mambo yote watu wanayoabudu humu duniania! Lakini mwisho wa siku gizani linabaka watoto, linaua.

Halafu mwishowe mtu anakuja Kwanini Mungu anaacha watu wanabaka watoto. How about: Kwanini ubake watoto wewe pepo mchafu?

Mimi naamini yote yanayoteka duniani ni kwaajili ya wateule wa Mungu, yaani wale ambao watamchagua Mungu na kupata uzima wa milele na Mungu.

Watakuwa wamejifunza mema na mabaya, huu ndo mti tuliouchagua jamani. Baadaye kwenye umilele tukisema mabaya tunajua tunaongelea nini maana tumeona kwa macho yetu.

Ndomana Mungu anawaita wenye haki. Hata Yesu alisema hukumuni kwa haki (Yohana 7:24). Sasa wewe unaona mijitu inafanya mauzauza hukumu yako unaipeleka kwa Mungu seriously? Unafikiri viwango vyako vya haki viko sawa? Utu wako uko sawa? Kwenye Ufalme wa Mungu ukiingia utapegeuza Jehanam in zero minutes, maana utakuta watu wako zao wana amani wanaishi kwa haki halafu wewe unaenda kuanzisha vagi halafu useme kwanini Mungu kaniacha nianzishe vagi! !

Kuzaliwa na magonjwa ni matokeo ya mwili unaokufa! So if anything kuzaliwa na magonjwa just means miili yetu ni imperfect, asiyepata hili anapata lile, tunamshukuru Mungu kwa nafasi kuwepo ulimwenguni maana tungeweza tusi exist ever, na tunategemea kwa hamu kupata miili mipya isiyokufa.

"Sikilizeni, nawaambia siri: Sote hatutalala, lakini sote tutabadilishwa:

ghafula, kufumba na kufumbua, parapanda ya mwisho itakapolia. Kwa kuwa parapanda italia, nao wafu watafufuliwa na miili isiyoharibika, nasi tutabadilishwa.

Kwa maana mwili huu wa kuharibika lazima uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa lazima uvae kutokufa.

Kwa hiyo, mwili huu wa kuharibika utakapovaa kutokuharibika, nao huu mwili wa kufa utakapovaa kutokufa, ndipo lile neno lililoandikwa litakapotimia: “Mauti imemezwa kwa kushinda.”

1Wakorintho.15.51-54.NENO

Hapa naongea mwenyewe nimeingiza theater four times, hours of surgery, so I know pain, unamwambia dokta naomba painkiller anakwambia hiyo sindano tumekuchoma ndo painkiller ya mwisho hamna painkiller kubwa zaidi ya hiyo, bora hata uchungu unapanda na kushuka kuna muda mama anapumzika na uchungu, ile ni pain non stop. Nayajua maumivu na najua kuishi na matokeo ya mwili wenye matatizo. So sibwabwaji tu hapa.

Hilo ni langu najua na wengine wana mengine, huyu mapafu, huyu damu, huyu mifupa, huyu tumbo, huyu macho, yani asokuwa na hili ana lile, wote tunashiriki maumivu in one way or another tukiwa na IMANI juu ya yule aliyetufanya tuwepo, na TUMAINI kuwa kuna umilele usio na tabu zote hizi unatusubiri, tu

"Atafuta kila chozi kutoka macho yao. Mauti haitakuwepo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu, kwa maana mambo ya kwanza yamekwisha kupita."
Ufunuo.21.4.NENO
 
Na pengine hakuna maisha kabla ya kifo. au maisha mazuri yasiyo na taabu yanaweza ysimfurahishe kila mtu.
NB: Mungu yupo ila uthibitisho wa uwepo wake kwa njia ya macho, damu na nyama, hakika ni mgumu,.
Wewe umethibitisha vipi kama yupo?
 
Mungu kaweka kanuni katika uumbaji wake,nje ya kanuni hizo ni matatizo ya kiumbaji,mathalani,katuumba Ili mwili uwe vizuri basi tuwe active kama vile kutembea nk,sasa hata vyakula kaweka vipi tule vipi sumu, watoto kupata hayo matatizo tangu wakiwa uja uzito siyo kosa la Mungu ni kosa lako, Mungu habadili kanuni zake,maji hayatopanda mlima wala hutoshiba kwa mionzi ya jua


  1. Kwanini mungu wako anaruhusu ujauzito utungwe, mtoto akue mpaka akaribie kuzaliwa halafu afie tumboni?
Wewe mbeba mimba umekiuka kanuni za uumbaji,usipotulia ukapata kaswende,mtoto ataozea tumboni


  1. Naomba kueleweshwa; kwanini Mungu wako muweza yote, anaruhusu vifo vya watoto wasio na hatia? Na, ni nini sababu ya kuwaumba watoto wakiwa na mapungufu ambayo anajua yatakatisha uhai wao?
Kimsingi swali lako ni moja
Huenda umepoteza mtoto,pole
 
Na pengine hakuna maisha kabla ya kifo. au maisha mazuri yasiyo na taabu yanaweza ysimfurahishe kila mtu.

Wewe umethibitisha vipi kama yupo?
Bwana kiranga tulimwambia Mungu yupo,tukimpa mpangilio maalum wa universe na umbile la binadam kama dalili ya uwepo wa designer
Elon musk kwa sasa anaamini kuna Mungu/designer wa universe baada ya project yake ya anga za mbali
Ukijiuliza pua yako ilijuaje duniani kuna hewa itahitaji kuvuta,na macho yako yalijuaje kuna mwanga duniani yakakaa hapo,utang'amua kuna designer
 
Majanga yanatokea sababu ya ubinadamu tu! Fikiria mzazi anamlea mtoto wake katika malezi bora lakini baadae mtoto anakua shoga, changudoa au mla unga kwa matakwa yake mwenyewe utasema kuna kosa la mzazi hapo?

Basi ndivyo ilivyo Mungu na mwanadamu, wazungu kutwa wanakazana kutengeneza mabomu ya nucleur siku ya kilipuka tutamlaumu Mungu?

Usikute rafiki yako kuna masharti ya jinsi ya kulinda ujauzito aliyakosea mfano baadhi ya dawa hivyo imepelekea umauti wa watoto.

Njia za Mungu hazichunguziki.
 
Hayo maswali uliyouliza honestly asilimia kubwa ya watu wamewahi kujiuliza pia, wengine tumejiuliza kimya kimya tukikosa kabisa majibu

Wengine waliuliza hayo maswali wakiwa na visu mikononi, sumu kwenye glass, au kamba tayari juu ya mtu. Wengine waliuliza huku vifua vyao vimeloa machozi na kamasi kutokana na maumivu ya maisha

And still hakuna majibu ya moja kwa moja

Wengine walichoka kabisa wakaamua kuikimbia hii dunia baada ya kujiuliza maswali hayo na kukosa answers😢

Wengine wameamua tu kuacha huu muundo wa dunia uwe jinsi ulivyo, because maisha yenyewe yanaonekana too complicated kuelewa kila kitu kuna mda maisha yanakosa hata maana

Mungu amejificha sana
Kama angekuwa anaonekana live mbele yetu, wengi tungependa kumuuliza kwanini mambo yanaenda hivi kwenye maisha ya watu

Kwanini ana ruhusu maumivu kwa watu kiasi mpka wanapungukiwa imani ya kumuamini

Kiasi watu husema Mungu hayupo😢
Na sometimes wana hoja
 
Sababu ya Mungu wako kuamua kuadhibu vizazi na vizazi vya wale waliokosea awali ni ipi?
Waliokosea wameshakufa, ila vizazi vinavyofuata wanaadhibiwa ili iweje?
Ni pale tu watakapomtambua Yesu ndiye Bwana na Mwokozi wa maisha yao na kuamua kumfuata Yesu kwa maosha yao yote.
Mungu tayari anajua maisha ya mwanadamu kuanzia mwanzo mpaka mwisho, so wale amabao hawatampokea Yesu anawatesa kwanini?
 
Niliyosoma, ninayosoma na nitakayosoma sinayo mamlaka ya kielimu kuyajua na kuyafanyia kazi, bali kila kitu ni uharibifu tu, kujua au kutokuja ni ujinga tu.
 
Mtoto mdogo mbona unazunguka zunguka sana badala ya kuwa direct 🤭
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…