Watu wote mnaomuamini Mungu mje, nina swali kwenu 😢

Watu wote mnaomuamini Mungu mje, nina swali kwenu 😢

hizi dini tatu hizi za Abrahamic Religions huwa hazihitaji mtu utumie reasoning wala logical thinking.
Ukianza kufanya reasoning na logical thinking tu, kuna maandiko mengi utaanza kuya-doubt kwenye dini yako.

Hawataki maswali ya ku-reasoning.
Ukifanya reasoning, starting asking questions, watakushambulia na kukwambia "imani yako haba."

Faida kubwa ya hizi dini, zimeongeza ustaarabu, otherwise dunia ingekuwa troubled mno.

Ukizichukulia hizo Abrahamic Religions kwa mtizamo huo, ni poa sana.
Just lower your expectations lakini lenga mbali (aim very far) tufute chozi kisha tusogeze siku, when our time is up (death) tutarudisha nutrients kwenye food chain - food web.

Tutarudisha nutrients ili viumbe vingine vistawi kwa hizo nutrients (directly or indirectly) na hivi viumbe vingine navyo muda wao utaisha, vitarudisha nutrients na vyenyewe, the circle goes over and over again.

Life! Ukiliwaza sana logically , unaweza usione umuhimu wa kuwepo duniani, kila pakikucha tunazidi kusogea kwenye kifo.

Uzuri ni kwamba kila binadamu anayo ile mentality kwamba "kesho will be a better day" ila without this one, aiseeee tungekuwa "wanyama (cruel)" mno, the end of humanity.
Nadhani ni suala tu la mabadiliko ya kisiasa pindi zilipo asisiwa siasa za kidiplomasia na kushika hatamu Wala sio dini ndio kwamba zimeleta ustaarabu ukifuatilia siasa za kidunia vyema hizo dini ni chanzo Cha maafa makubwa sana duniani nadhani unafahamu Kwa kina kuhusu vita za crusade SI Cristianism sio islamists wameua sana watu hizo dini ni Cancer

Kilicho kuja kuleta ustaarabu kamili katika huu ulimwengu ni mapinduzi ya kisera na siasa za kidunia ni baada ya bara la Ulaya kuamua kuachana na siasa zenye mafungamano ya kidini na kunipa democracy nafasi yake wakachagua kuipa science na technology nafasi ya kufanya gunduzi innovation mbali mbali dini ikapewa kisogo Kisha democracy ikapewa nafasi ya kushika Kijiti Cha kuyaongoza mataifa Yao

Ijapo kuwa democracy Ina madhaifu yake lakini Kwa kiasi kikubwa imeweza kuleta power imbalance Katka mataifa na katika jamii kinyume na hapo mambo yange kuwa ni more than worse

Hebu fikiria kama Nchi yetu ingekuwa chini ya uongozi wa Taliban !? Hali ingekuwaje !?

Dini imeachwa itumike tu kwaajili ya kushape jamii lakini hazijapewa fursa ya kuendelea kutumika kama Sheria kuu katika ngazi ya za kitaifa na ngazi za kimataifa na pia watu wakapewa uhuru na hiyari ya kuzifuata hizo dini au kutozifuata

Laiti kama dini zingeachwa ziwe Zina tumika as Sheria za Nchi Dunia isingekuwa katika huu ustaarabu nafuu uliopo hii Leo , Dini ni chanzo Cha vurugu nzito duniani that's why still tunaona baadhi ya mataifa makubwa huzitumia dini kubrain wash watu na kupenyeza magaidi ili waweze kuleta machafuko katika mataifa ambayo hayataki kuzifauat hizo Nchi kubwa , hapo unajifunza Nini !? Unapata kujifunza kwamba dini ni silaha inayo tumiwa kwaajili ya kuwagawa watu kwasababu ndani ya mafundisho ya kidini Kuna ubinafsi wa Hali ya juu !

Waumini wa hizo Dini zote za abramic Huwa wanafundishwa na dini zao kujiona kuwa wao ndio wana haki au wapo sahihi na ndio tabaka sahihi kuliko matabaka mengine Kitendo ambacho kina wafanya waumini wa dini hizo kutembea huku wakiwa wamebeba ubinafsi Tayari ndani ya mioyo Yao una Kuta ni rahisi Kwa mkristo au muislam kubaguana kisa tu hizo Imani zao kitendo ambacho ni rahisi Kwa mtu au watu wenye ujuzi wa kucheza na psychology za watu kuweza kuwatumia waumini hao kupandikiza chuki na hatimae kuweza kuwagawa na kuleta machafuko katika Jamii
 
Dhumuni la kujaribu wanadamu ni nini?
Kulingana na maandiko yenu, Mungu anajua mwanzo mpaka mwisho wa maisha yako, so anakujaribu ili iweje?

Je Mungu anafurahia kudhalilisha au kuumiza watu bila sababu? au lengo la kuleta mitihani yenye machungu kama kukupa furaha ya watoto mapacha na kuwanyakua kabla hawajaishi ni nini?

Asante, hatujapoa!
Inabidi aulizwe yeye mwenyewe M/Mungu , nikupe tips za kumuuliza na akakujibu… usije ukalalamika hapa baada ya majibu
 
Nikikumbuka bimkubwa wangu alivyoteseka kuumwa miaka 16 hadi alikuwa anasema bora nife niwapumzishe wanangu na kuniugiza maana alikuwa wakufanyiwa kila kitu. Aliteseka sana kwa kweli hadi mda mwingine alikuwa anafunga kitenge ili ajinyonge,haya maisha yanamateso sana. But kauli ya mwisho aliyomwambia Daktari wakati yuko ICU anaelekea kukata kauli alisema, 'WAAMBIE WANANGU NASHUKURU KWA YOTE WALIPIGANIA UHAI WANGU MIMI SINA CHAKUWALIPA WALA SINA CHA KUWADAI, NITAWAOMBEA NIENDAKO'šŸ˜”šŸ˜”
Pole sana šŸ«‚ , mimi nina mawazo kama huyo kiongozi uliyemquote, nikipata terminal illness ambayo nina uhakika imefikia hatua isiyo na tiba, basi tayari nimeshajiandaa kujiondoa hapa duniani kwa haraka kadri itakavyowezekana.

Ni logical decison ambayo inamsave kila mtu kutoka kwenye unnecessary suffering.
 
Mungu anatoa uzima lakini shetani ndiye muuaji. Lawama si kwa Mungu bali ni kwa shetani aliye muuaji na kwa watu ambao hawakubali kumwamini Yesu ili waokoke na walindwe na nguvu za Mungu. Ukiokoka unakuwa na ulinxi wa Mungu!.
Huyo shetani aliumbwa na nani?
Mungu alifanya makosa kumuumba? ilikuwaje akamshinda muumbaji kwenye uovu mpaka sasa anatesa viumbe wasio na hatia?

Naanzaje kumlaumu shetani muuaji bila kumlaumu aliyemuumba huyo shetani?
 
Mkuu endelea, nakusikiliza!
View attachment 3588782
Swali la kujiuliza kwanini wewe hapo ulipo ni mkristo au muislam!? Je laiti kama ungezaliwa china ungekuwa ni muumini wa hizo Dini !?

Jibu nadhani litakuwa ni hapana

So kama jibu ni hapana hauoni kwamba sababu ya wewe kuwa kwenye Moja ya hizo dini ni jambo ulilorithishwa na wazazi wako au walezi wako !? Kwanini urithishwe kitu Pasipo kushirikishwa What if huyo aliye kurithisha huwenda hakuwa na mtazamo chanya kuhusu hizo dini akajikuta tu Yuko brainwash akachagua kuzifuata cause wazazi nao ni binaadamu wa kawaida they can make mistake

Na je mara nyingi tunapo muongelea mungu Huwa tuna mkusudia mungu yupi hasaa !? Maana ukienda china wana mungu wao ukienda India wana Miungu Yao ukienda Haiti it's the same ukienda Mongolia it's the same !! So sisi tuna mzungumzia mungu yupi!? Na tuna uhakika upi kuwa mungu wetu ni sahihi kuliko mungu wa wachina Au mungu wa wahindi !?

Na je mpaka Leo hii hamuoni kwamba hayo mafundisho yenu Kuna sehemu hayana tija haya apply kabisa mazingira ya watu wengine mfano ukienda china habari za kina musa sijui yesu Muhammad hakuna hizo habari so unawezaje kumwambia mtu wa china kuhusu habari za bible na Quran akakuelewa !?

Wakati wana Miungu Yao and Kila kukicha wanazidi kufanikiwa!!!
 
Binafsi sipo tayari kuteseka kwa ugonjwa naoona hauponi. Death is peaceful. Ukifa hakuna maumivu tena. Tena kwangu ambae kufa na kuishi is equal to zero. Sasa nabaki nateseka ili iweje?? Uoaga wetu tu
Kweli kabisa šŸ“Œ
 
Pole sana. Biologia inatueleza kwamba hizo hitilafu huwa zinatokana na Mutation.
Pole sana. Biologia inatueleza kwamba hizo hitilafu huwa zinatokana na Mutation.
Mmh, endelea kiongozi, I'm listening
Oprah Winfrey GIF.gif
 
Maswali ya kitoto ni magumu sana kwa sababu watoto huwa wanakuwa bado hawajawa brainwashed na dini au kutishwa.
Maswali ya kitoto sio magumu Bali uyo ata ukimjibu awezi kukuelewa kwasababu akili zake bado changa
 
Kitendawili cha Epicurus: Hoja hii inasema ikiwa Mungu ana uwezo wote na ana upendo wote, asingeruhusu watoto wasio na hatia wateseke.
Wewe unaona kwa matendo yake kwa watoto, ana upendo kwao?
Uwepo wa mateso haya huwafanya baadhi ya watu kuamini kuwa aidha Mungu hayupo, hana uwezo wote, au hana upendo.
Wewe unaamini kwamba ana uwezo? (if so, inamaanisha anaruhusu mateso kwa kudhamiria watu wateseke)
Ana upendo (ila nachagua kuumiza na kuleta maumivu) huo ni upendo wa namna gani?
 
Mwenyewe kachemka akamrusha Duniani😁😁😁Jamaa linanguvu sana! Kutoboa ngumu.
Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu na ninyi mkaao ndani yake. Ole wa nchi na bahari; kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu akiwa na ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache.
Ufunuo 12:12
 
Back
Top Bottom