Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 64,960
- 111,265
Sayansi katika mambo mengi inaeleza why and how, Kuna baadhi ya mambo hailezi why kwa wakati fulani (hata hivyo kutokueleza why sio kushindwa bali ni ukomo wa uelewa kwa muda huo tu kwa sababu kila siku knowledge katika sayansi inakuwa)Sayansi inaeleza kuhusu how sio why.
Itakuelezea namna cancer inavyotokea, lakini haiwezi kujibu kwanini watu wanatafuta justice, hope n.k hata katikati ya suffering.
Kwa maelezo yako, basi hata upendo wa mama kwa mtoto au huzuni ya kumpoteza mwanao inabidi uiite mere biological reactions.
Nimeeleza hapo mambo mawili yenye kuelezea maisha ya binadamu ni science na social interaction. Uchungu wa kupoteza ndugu ni kutokana na biology na social relationship. Kama ukimchukua mtoto akiwa mdogo kabisa pindi tu amezaliwa halafu umtenge na mama yake halafu siku msiba wa mama yake umetokea umlete na usimuambie ni mama yake hawezi kulia au kusikia uchungu.
