Watu wote mnaomuamini Mungu mje, nina swali kwenu 😢

Watu wote mnaomuamini Mungu mje, nina swali kwenu 😢

Ikiwa sisi wanadamu tumepiga marufuku au tumeharamisha adhabu za ujumla "collective punishment" inakuaje mungu mkamilifu aione ni sawa??
Kuna haki gani kumuhukumu mtu kwa makosa ya mwingi? Common sense na logic sio kila mtu ahukumiwe na awajibishwe kwa kosa lake?!
Ndivyo Mungu anavyosema kwa hekima yake maana inapoishia akili ya mwanadamu ndipo yeye huanza.
 
Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu na ninyi mkaao ndani yake. Ole wa nchi na bahari; kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu akiwa na ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache.
Ufunuo 12:12
Jamaa kma alifanikiwa kushawishi robo tatu ya malaika mbinguni atakushindwa wewe ambae hata Mungu hujawahi kumuona? Kuna kitu hakikuwa sawa tu ndo maana jamaa akalianzisha hawezi kukurupuka tu. Ni vile hajawahi kupewa nafasi yakusema jambo kilitokea nini hadi akazinguana na muumba bali analishwa maneno tu mara alikuwa na wivu,mara alikuwa mjeuri mara alitaka kumpindua Mungu. Vitabu vyote vinamsema vibaya na kumchora vibaya hadi wanamuweka mapembe, vitabu vyote anaezungumza ni Mungu na manabii/ mitume wake.
Hafu hizo 'OLE' mbona ni nyingi sana kwenye hivyo vitabu? Dini zisingejengwa kwa mfumo wa 'OLE' au vitisho sidhani kma zingepata wafuasi wengi kiasi hiki. Watu wanaziogopa hizo OLE.
 
Pole sana šŸ«‚ , mimi nina mawazo kama huyo kiongozi uliyemquote, nikipata terminal illness ambayo nina uhakika imefikia hatua isiyo na tiba, basi tayari nimeshajiandaa kujiondoa hapa duniani kwa haraka kadri itakavyowezekana.

Ni logical decison ambayo inamsave kila mtu kutoka kwenye unnecessary suffering.
Maumivu ya mda mrefu ni mateso sana. Kma ni mtu wako wa karibu inauma sana hasa kma mnafanya kila jambo na ugonjwa hauonekani ila mtu anaumwa sana na anaisha kila siku hadi hatua anarudi utotoni yaan hawezi kufanya kitu tena ni wakuhudumiwa.
 
Hakuna Hali iliyokamilika, Kila Hali ina upungufu wake na uimara wake. Hakuna maana ya kuwepo kiumbe chochote duniani ikiwa Kila kitu Kipo 100%, hii ni fikra ya kawaida tu inayozunguka sayari na nyota zote za ulimwengu...
Kama unaona hakuna maana ya kuwepo kiumbe chochote duniani ikiwa kila kitu kipo 100% basi bora binadamu wangekuwa wanaugua homa na mafua tu ila sio Malaria, HIV, TB, Cancer na vifo. Hata hivyo sio kweli kwamba hii ni fikra ya kawaida tu inayozunguka ulimwengu wote. Huu ni mtazamo wako wa dini yako tu.
 
Kama aliweza kumfukuza Adam na Eva bustanini akawapa adhabu.. huyu akatafute kwa jasho, huyu akazae kwa uchungu. basi wacha tuendelee kunywa hicho kikombe, ukiachana na maswahibu ya ulimwengu wa giza wa kina Mshana


Hii story inatuchanganya tu mbuzi mwenyewe anazaa kwa uchungu simba anataabika weeee ndio akamate windo sasa Hawa walikula tunda gani!!!
 
Mmh, endelea kiongozi, I'm listening
View attachment 3588984
Ni wakati mbegu ya baba na yai la mama zinalandana ili kutengeneza kiumbe aliyekamilika mwenye 46 chromosomes, kuna tokea hitilafu kidogo kwenye Crossings kama ziki cross ndivyo sivyo.
Hii hupelekea mtoto kuzaliwa na matatizo kama vile hormones kuzidi, unavyoona mwanaume kafanana na mwanamke na watu mtaani wanaaasemaga yule hormones za mama zimezidi,.. Pia matatizo kama Down's syndrome (Utaahira) n.k. Hii ndyo hupelekea mtoto kuzaliwa kidogo na matatizo au utofauti.

Kwa Case kama ya kwako, ambapo umesema kuwa mtoto mmoja alifia tumboni na mwingine alizaliwa na utumbo hatuwezi tukasema moja kwa moja kuwa ilisababishwa na Mutation, kwa sababu kuna factors zingine zinaweza kusababisha hvyo pia kama vile Mwanamke kupigwa wakati wa ujauzito, matumizi ya Pombe & Sigara na Pain Killers in Gestation Period, n. k
 
Haijalishi wewe ni muislamu au mkristo, kama una imani yoyote inayoamini kwenye "Mungu" nina maswali hapo chini kwa ajili yako.
  1. Kwanini Mungu anaruhusu watoto wazaliwe na changamoto za kiafya ambazo hazina tiba na zitawatesa watoto mpaka wanapokufa wakiwa bado watoto wachanga au wadogo? (cancer za watoto, matatizo ya moyo, ubongo, upumuaji etc.)

  2. Kwanini mungu wako anaruhusu ujauzito utungwe, mtoto akue mpaka akaribie kuzaliwa halafu afie tumboni?

  3. Naomba kueleweshwa; kwanini Mungu wako muweza yote, anaruhusu vifo vya watoto wasio na hatia? Na, ni nini sababu ya kuwaumba watoto wakiwa na mapungufu ambayo anajua yatakatisha uhai wao?

    SABABU YA KULETA HUU UZI:
    Nimeumia 😭, mtu wangu wa karibu amepoteza watoto wawil mapacha; mmoja amefia tumboni, mwingine amezaliwa na uvimbe kichwani, amemaliza siku tano amefariki. Inaniwia vigumu kuamini kwamba kuna sababu yoyote hawa watoto walistahili hayo waliyoyapitia.

    View attachment 3588755

    Naomba utumie lugha nyepesi na unifundishe, kama kuna Mungu kwanini anaruhusu mambo ya kikatili namna hii?

    Asante na Alamsiki!
Nakushauri pia ujiulize swali hili: Kwanini tulikubali kula tunda tulilokatazwa tusile?
Niaminivyo mimi ni kwamba sisi wenyewe(uzao wa Adam na Hawa) ndio chanzo cha matatizo na mambo yote mabaya tunayoyaona leo. Tuliambiwa tukila tunda la katikati ya bustani tutakufa, tukakaidi, tukala. Hivyo sisi sote(including watoto) tunakula mshahara wa dhambi yetu ya kukataa kutii agizo la Mungu. Hata hivyo, ninaamini pia kila chenye mwanzo kina mwisho. Hivyo ninaungana na wenye imani kwamba dunia hii inakaribia mwisho, na siku moja tutaingia katika mbingu mpya na nchi mpya isiyokuwa na ubaya wala jambo lolote lenye kuleta huzuni. Tusubiri, muda utaongea
 
Nakushauri pia ujiulize swali hili: Kwanini tulikubali kula tunda tulilokatazwa tusile?
Niaminivyo mimi ni kwamba sisi wenyewe(uzao wa Adam na Hawa) ndio chanzo cha matatizo na mambo yote mabaya tunayoyaona leo. Tuliambiwa tukila tunda la katikati ya bustani tutakufa, tukakaidi, tukala. Hivyo sisi sote(including watoto) tunakula mshahara wa dhambi yetu ya kukataa kutii agizo la Mungu. Hata hivyo, ninaamini pia kila chenye mwanzo kina mwisho. Hivyo ninaungana na wenye imani kwamba dunia hii inakaribia mwisho, na siku moja tutaingia katika mbingu mpya na nchi mpya isiyokuwa na ubaya wala jambo lolote lenye kuleta huzuni. Tusubiri, muda utaongea
Kwa nini unasema "tulikubali* ? Labda ungesema "walikubali". Hata hivyo hizo ni hadithi tena fiction tu za Wayahudi tu ambazo zinaaminiwa na kuchukuliwa kama ni uhalisia na kweli na Wakristo pamoja na Waislamu. Watu wengine kama Wahindu au Budha nao wana hadithi zao tofauti kabisa. Wanasayansi wao hhawamtambui Adam na Hawa, wanasema binadamu ni matokeo ya evolution.
 
Kama unaona hakuna maana ya kuwepo kiumbe chochote duniani ikiwa kila kitu kipo 100% basi bora binadamu wangekuwa wanaugua homa na mafua tu ila sio Malaria, HIV, TB, Cancer na vifo. Hata hivyo sio kweli kwamba hii ni fikra ya kawaida tu inayozunguka ulimwengu wote. Huu ni mtazamo wako wa dini yako tu.
Kama kweli utakuwa na akili basi niambie ni kitu au Hali gani iko kamili asilimia Mia moja katika haya maisha?, nataka unijibu Hilo swali kama kweli wewe Una akili timamu na Nafikiri hujui maana ya dini.
 
Binadamu wameweza kumfikiria mungu alivyo, ndio maana kila jamii ina tafsiri yake ya mungu au mungu wao ni tofauti na wengine. Kwa mungu anayefikiriwa na Abrahamic religions ana tabia nyingi za kiume.
Hio kumfikiria kitofauti sasa ndio mjue hamko completed , mmefumbwa.
Kumfikiria sawa basi hatwakuwa Mungu tena.

Hivi kwanini yoda asiwe binti wa zamani? Na binti wa zamani asiwe yoda?
 
Kama kweli utakuwa na akili basi niambie ni kitu au Hali gani iko kamili asilimia Mia moja katika haya maisha?, nataka unijibu Hilo swali kama kweli wewe Una akili timamu na Nafikiri hujui maana ya dini.
Kwanza kuwa kamili ni nini? Halafu kwa nini unaona hakuna maana ya kiumbe chochote kuwa kamili hapa duniani??
 
Hio kumfikiria kitofauti sasa ndio mjue hamko completed , mmefumbwa.
Kumfikiria sawa basi hatwakuwa Mungu tena.

Hivi kwanini yoda asiwe binti wa zamani? Na binti wa zamani asiwe yoda?
A lot of gibberish, it doesn't make any sense.
 
jibu ni hili
Mungu ni nguvu si kiumbe .. Na hiyo nguvu hua haiingilii jambo bila kuamriwa ilifanye .. kwa mfano ilipaswa huyo mjamzito kwa ssaala aiamuru nguvu hiyo imjaalie watoto wenye afya na uzima inge tii .. ILA NGUVU HIYO KAMWE HAIWEZ KUBADILI UALI YA MTU BILA RUHUSA .. tujifunze kusali kwa iman yeyote tu .. ELEWA TU MUNGU NI NGUVU SI KIUMBE MFANO LAHISI CHUKULIAGA MUNGU NI SAWA NA MOTO .. moto unaweza ukautumia utakavyo ila moto kama moto wenyewe hauwez ukajiamria tu kua leo ngoja ukuchomee nyama choma au ngoja leo ukuchomee nyumba .. bali ww utakavyo utumia ndivyo utafanya ... Na mungu pia yupo hivyo...ni nguvu ipo tuli tu uibadili ww ikusaidie nn ?.
Chai
 
Kwanza kuwa kamili ni nini? Halafu kwa nini unaona hakuna maana ya kiumbe chochote kuwa kamili hapa duniani??
Jibu Hilo swali langu Kwanza maana ulinijibu mwanzo Kwa kuonyesha kuwa unajua majibu au ulikuwa hujui unachokiandika?... Sasa basi ngoja nkujibu kiufupi, Kamili ni Kutokuwa na upungufu wowote ule haijalishi ni muda gani utapita, ulisema huu ni mtazamo wa dini yangu, je unahisi huu ni mtazamo wa dini na si ukweli kuhusu maisha kama nilivyomjibu mtoa mada(hoja yangu iliakisi) kuwa haijalishi uko na Imani au mungu gani Hali hii ya Kutokuwa kamili itamkumba Kila mtu hivyo mtu asijihisi mnyonge au mbaya Kwa Hali kama hizo za kufiwa na watoto as long as unafanya kuokoa mengine ni nje ya uwezo wako na ndiyo kutokuwa kamili huko....Swali lako la pili ni kwamba, maana ipo kwenye Jambo lisilo kamili na ndio ili kitu kilete maana kinahitaji marekebisho Kila wakati (huu ni mtazamo changamshi).
 
Mungu ni nini?

"Cause and effect" kila kitu kinasababu... Na hicho kisababishi kiliwezekana kutokana na Free Will aliyonayo kila mtu.

Ukiachana na masuala ya dini ambayo siyo ya kutegemea kwasababu hayana uhalisia. ni utashi wa watu wa utamaduni flani na siyo wa mungu.

Na huu ulimwengu unaongozwa kwa kanuni, kama haufiati kanuni basi matokeo yake usitarajie kinyume chake[ huwezi kupanda bangi ukavuna maharage...]

Hizo changamoto zilizotokea na zinginezo kama kufeli kwa ogani Figo, inni, moyo,nk mara nyingi hua zinakua ni matokeo ya life style ya mtu, mzazi etc ambayo aliichagua kupitia Free Will yake.
 
Back
Top Bottom