Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Nadhani hakuna chakula kinachosambaza magonjwa Tanzania hii kama kachumbari.
Mtu anaenda maliwatoni na maji ya kopo. Hata hajajitawaza vya kutosha anakuja kukata kachumbari. Wewe unapewa hiyo kachumbari unafakamia. Magonjwa mengi sana yanaenea kwa mtindo huu.
Amiba, vidonda vya tumbo, typhoid, minyoo, shigella na mengine lukuki. Ni wakati kwa mabwana afya kuhakikisha watu wote wanaoshika chakula kama kuandaa kachumbari, kuandaa chachandu, kukata nyama choma au kukata matunda wanavaa gloves(Wakata matunda wengi wanajitahidi kwa hili).
Hili linaweza punguza zaidi ya asilimia 50 ya magonjwa ya matumbo, baya kuliko yote likiwa vidonda vya tumbo.