Hahaha, Unajua ni vitu vidogo sana usafi, chakula kimepikwa kwa temperatature sahihi. Vijiko vioshe kwa sabuni au 100% tempetarute.Kwani kila asokotwaye tumbo na kuarisha lazima afe? Huyo kichaa tumbo linamsokota mpaka linapona lenyewe na utamkuta amelala popote, je wewe unaweza? Kwahiyo unaona ni sawa kusimamisha shughuli zako kwa kula uchafu?
unaogopa kula paka nini? Watu wanakula mpaka mbwa na wako fresh tu, kikubwa usafi uzingatiwe.Tatizo idara ya chakula wanapokea mishahara ya bure tu, watu wanalishwa mafuta ya transformer na mishkaki ya paka sababu hakuna ukaguzi wa vyakula mitaani.
Na ndio sababu kuu huwa nakula chakula cha nyumbani tu, ni aidha niondike nacho kwenda kazini, nirudi mchana ama niletewe kazini.
Bonge la TangazoNadhani hakuna chakula kinachosambaza magonjwa Tanzania hii kama kachumbari.
Mtu anaenda maliwatoni na maji ya kopo. Hata hajajitawaza vya kutosha anakuja kukata kachumbari. Wewe unapewa hiyo kachumbari unafakamia. Magonjwa mengi sana yanaenea kwa mtindo huu.
Amiba, vidonda vya tumbo, typhoid, minyoo, shigella na mengine lukuki. Ni wakati kwa mabwana afya kuhakikisha watu wote wanaoshika chakula kama kuandaa kachumbari, kuandaa chachandu, kukata nyama choma au kukata matunda wanavaa gloves(Wakata matunda wengi wanajitahidi kwa hili).
Hili linaweza punguza zaidi ya asilimia 50 ya magonjwa ya matumbo, baya kuliko yote likiwa vidonda vya tumbo.
Kabisa. Mtu anasema haponi vidonda vya tumbo kumbe anapona na kuambukizwa tena na tena.Wanaofanya biashara ya chips wengi kachumbali zao hawatengenezi wenyewe wananunua sokoni kama Shekilango etc na sio kachumbali tu hata pilipili zakutengenezwa ...ni wakati Sasa mabwana afya wa masoko kuhimiza hiyo hygiene masokoni.
Watu wazamani waliishi mazingira ambayo sio rafiki kwa afya lakini life span yao ilikuwa ni kubwa kuzidi hii modern generationIngekuwa ukiumwa mara moja unatengeneza kinga na huumwi tena ingekuwa sawa. Lakini kwa sababu kuumwa au kuwa exposed na wadudu wa magonjwa hakutengenezi kinga ya milele, lazima tuchukue tahadhari.
Vichaa wanaumwa sana sema hawasemi. Pia maisha ya vichaa wengi ni mafupi sana. Wengi hawafiki uzeeni.
Point sio wote tuwe vichaaMkuu unataka wote tuwe vichaa? Lifestyle hiyo?
No haipo hivyo.Kwani kila asokotwaye tumbo na kuarisha lazima afe? Huyo kichaa tumbo linamsokota mpaka linapona lenyewe na utamkuta amelala popote, je wewe unaweza? Kwahiyo unaona ni sawa kusimamisha shughuli zako kwa kula uchafu?
Nani kakudanganya? Watu wa zamani ilikuwa ni bahati kufika miaka 40. Watu walikuwa wanakufa balaa. Fanya tafiti utaona jinsi ukisasa ulivyoongeza lifespan ya mwanadamu.Watu wazamani waliishi mazingira ambayo sio rafiki kwa afya lakini life span yao ilikuwa ni kubwa kuzidi hii modern generation
Sio avae kwenye mikono tu,inabidi wajifunike hata usoni na maplastiki,maana kwa mji kama Dar wenye joto kali halafu mpishi yuko jikoni jasho linatirirka usoni,unafikiri mpaka amalize kupika hakuna hata kitone kimoja cha jasho kinachoingia kwenye chakula au chipsi mayai zetu za mitaani...?Nadhani hakuna chakula kinachosambaza magonjwa Tanzania hii kama kachumbari.
Mtu anaenda maliwatoni na maji ya kopo. Hata hajajitawaza vya kutosha anakuja kukata kachumbari. Wewe unapewa hiyo kachumbari unafakamia. Magonjwa mengi sana yanaenea kwa mtindo huu.
Amiba, vidonda vya tumbo, typhoid, minyoo, shigella na mengine lukuki. Ni wakati kwa mabwana afya kuhakikisha watu wote wanaoshika chakula kama kuandaa kachumbari, kuandaa chachandu, kukata nyama choma au kukata matunda wanavaa gloves(Wakata matunda wengi wanajitahidi kwa hili).
Hili linaweza punguza zaidi ya asilimia 50 ya magonjwa ya matumbo, baya kuliko yote likiwa vidonda vya tumbo.
Darlin umelike hapo unanifundisha nini...??Huku uswahilini tunakula mihogo iliyotiwa kachumbari zenye nyanya zilizooza.
Na hatuharishi yani fresh tu.
So kuna kitu ambacho mimi nimekibaini.
Ni kwamba unapokuwa mtu wa kuchukua caution za kiafya kwa kila kitu kuna hasara pia ambayo unaipata.
Hasara hiyo ni kupoteza immune ya kuweza kupambana na bacteria nyemelezi.
Zile kinga zikikaa mwilini bila kupata challenge zinakuwa useless na mwisho wa siku zinakufa.
Ebu fikiria hii.
Ni vichaa wangapi ambao tunawaona wakiokota vyakula vilivyooza majalalani na kuvila?
Wanalala sehemu ambayo ni unsafe wanapigwa na mbu usiku mzima na huwezi kumuona amezima eti maleria imempanda.
Maana yake ni kwamba kinga yake iko active na ina nguvu kwasababu kila siku anapokula chakula kichafu.
Mwili una adopt na kuanza ku generate kinga kuendana na mazingira hayo.
Ndio maana chungwa alilookota jalalani akala, ukipewa wewe lazima tumbo liume na kuharisha juu.
Kwa hiyo ukiangalia kwa hizo circumstances utaweza kuona mazoea yana play part kufanya kinga iwe active au passive.
Mimi hizo sijawah sizielewagiiUkienda sokoni kwenye matunda, ukipita matunda ya juisi haya hapa ukiyaangalia yamebondeka lojolojo hayapo vizuri, watu wananunua wanatengemezea juisi zile za kuuzwa au zile wanaweka kwenye migahawa, mungu tulinde tu.