Watuhumiwa wa mande ya Ubakaji na ulawiti waliotumwa na afande wakamatwa

Watuhumiwa wa mande ya Ubakaji na ulawiti waliotumwa na afande wakamatwa

Ile video kwa kweli inaumiza sana. Kama ndiyo binti yangu anafanyiwa hivyo hata sijui nitafanya nini wallahi.

Nasikia kuwa hao vijana wote ni wanaulinzi wetu. Ngoja tuone itakavyokuwa lakini kama sheria itashindwa kuchukua mkondo wake kisa ni wanaulinzi ndiyo tutajua tuna jamii ya namna gani 😒
Wale jamaa ilikuwa ni kunyongwa hadharani au kutandikwa risasi

Hili suala likichukuliwa simple tutawatengeneza wabakaji wengine wa aina hii

Adhabu kali ya kifo itolewe iwe onyo kwa wengine

Ule ni unyama aisee
 
Mtanii unaambiwa ni captain wa jeshi katuma wajeda wambake na kumlawiti binti huyo, kisa alitembea na mume wake. Lol

Sheria ifuate mkondo wake, Wallah.
Naanza kuamini msemo wa Mchungaji Jacob kule Youtube.

Hawa ndio wasiojulikana wanaotumiwa na watu waovu...ukitekwa tu wanatumwa kukula kiboga.
 
Jamii haitaki kuzungumzia msingi wa tatizo ni nini?

Tatizo ni wanawake wakiolewa wanaota mapembe na kugeuza ndoa ni jukwaa la mashindano.

Meanwhile wanawake haohao ukimpa cheo cha nyumba ndogo anakupa heshima zote na unamgegeda muda wowote unaojisikia hupangiwi uchi wa mgao na anakutii.

Kinyume chake mke wa ndoa anageuza nyumba uwanja wa mabishano, hana heshima, na uchi wake akupe anavyojisikia yeye, wewe uwe kama sex toy yake tu na hapa wahusika ni wanawake wenye viajira vyao vimewatia ujinga kufikia kudhani nafasi ya mwanaume kwenye nyumba inaweza kuwa replaced, never.

Tutaendelea kuwala wanawake wanaojuwa kutreat mwanaume na hao wote hawajaolewa, walioolewa tiwaache wakae na viburi vyao.
Mmh! Ni vile tu umeamua kuwa upande wa nyumba ndogo lakini kiukweli hata huyo nyumba ndogo ukimpandisha hadhi akawa mke ipo siku utakuja kuulalamikia pia.

Hapa sio wake tu hata na nyie wanaume mna kasoro zenu sababu unataka kusema unavyomjali mkeo ni sawa na unavyoujali huo mchepuko? Kama sio unategemea huduma zao kwako zitakuwa sawa?

Kwenye hili haipaswi kuangushiwa mzigo jinsia moja sababu ilivyo baadhi ya wanaume hata wapewe nini watachepuka tu na huwaga mna kamsemo kenu mnakaitaga "necha" eti , Kwamba hamuwezi kukaa na mwanamke mmoja.

Ukiona mkeo ana hizo tabia jua na wewe kuna sehemu umelega lega.
 
Kwa wale wazee wa bangbros wanaona kawaida
Wajinga sana wale jamaa 😁😁😁🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️

Screenshot_20240806_140630_Gallery.jpg
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema tayari vyombo vya dola vimeshawatia nguvuni watuhumiwa wa ubakaji na ulawiti wa msichana anayedaiwa kuwa ni mkazi wa Yombo Dovya jijini Dar es Salaam.

Agosti 4, 2024 zilisambaa video katika mitandao ya kijamii zikiwaonyesha vijana watano wakimbaka na kumlawiti binti huyo, huku wakimtuhumu kwa kile kilichosikika katika video hiyo kuwa ametembea na mume wa mtu.

Kadhalika, katika video hiyo inayodaiwa kuchukuliwa na vijana hao, binti huyo alisikika akieleza anakotokea na kumwomba msamaha mtu aliyetambulishwa kwa jina la afande.

Masauni amethibitisha kutiwa nguvuni kwa vijana hao leo, Jumanne Agosti 6, 2024 alipotafutwa na Mwananchi Digital kwa njia ya WhatsApp.

Katika ujumbe mfupi aliotumiwa kuulizwa iwapo watuhumiwa hao wameshakamatwa, Masauni alijibu kwa kuandika “tayari” kupitia ujumbe huohuo wa njia ya WhatsApp.

Hata hivyo, Waziri Masauni hajafafanua zaidi kwani amesema bado yupo kwenye mkutano kwa sasa.

Pia soma
Wapandishwe kizimbani tuwaone.

Huyo Aliyewatuma Kwa nini analindwa?

Mwisho Sijaona taasisi za Wanawake zikipaza sauti kumtetea binti.

Ni wazi wanawake ni watu wenye roho mbaya na hapo wamekausha kana kwamba Hakuna kilichotokea.

Sijajua Haki sawa wanazotaka Huwa ni kuteuliwa au kufanyaje
 
Mbona hawaeleweki? Msemaji wa Polisi anasema tuwe na subiri Uchunguzi unaendelea(Lates news -Mchana) ,Masauni anasema tayari washawakamata(Taarifa ya Asubuhi) ,mbona mnaleta MANJEGEKA?
 
Masauni alijibu kwa kuandika “tayari” kupitia ujumbe huohuo wa njia ya WhatsApp.
Nina mashaka na hili jibu, ni jepesi sana hasa likiyolewa na mtu kama masauni ambaye alikebehi suala ya utekwaji wa wananchi hususani wafuasi na wanachama wa vyama vya upinzani!!
 
Back
Top Bottom