Watumishi tunapoelekea Mei Mosi tumwambie nini Rais Samia?

Anamaanisha master's degree itambulike kwenye mifumo ya ajira, Yani iwe na general impact Kama ambavyo mtu mwenye diploma akienda kusoma degree akirudi anafanyiwa recategorization..ambapo kwasasa master's degree haina impact.
Ndio..ikiwezekana na PhD kabisa..itambulike.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Warudishe fao la kujitoa hifadhi za jamii kila mtu afe na chake kwanini wapangie matumizi hela isiyokua ya kwao?? Huu ni wizi wa mchana kweupe
 
Warudishe fao la kujitoa hifadhi za jamii kila mtu afe na chake kwanini wapangie matumizi hela isiyokua ya kwao?? Huu ni wizi wa mchana kweupe
Kabisa kabisa
 
Tunakupenda sana Mama, tunaomba nyongeza ya mishahara uifanye awamu inayokuja!
 
Inawezekana sijui kweli sasa usiniache na kutokujua kwangu na kunidhihaki na kunikejeli kwa uswahili na domo langu…just eleza tu kama ni maelekezo ya standing order au Waraka upi ili usaidie na wengine wasiojua kama mimi
Ni udhaifu wa Sheria ya ajira na mahusiano kazini. Watu walishapambana sana bila mafanikio. Watu walishafikishana mpaka kwa msuluhishi, CMA bila mafanikio.

Zaidi ya 90% ya Watumishi wanaokatwa mishahara ya hivi vyama siyo wanachama wao.

Na wanakata kwa kushirikiana na serikali, maana Hakuna mtu anaweza kukatwa mshahara bila kumhusisha Mwajiri.

Warudishe fao la kujitoa hifadhi za jamii kila mtu afe na chake kwanini wapangie matumizi hela isiyokua ya kwao?? Huu ni wizi wa mchana kweupe
Hii ni sherehe ya Watumishi wa Umma ndo maana hutasikia TUGHE wala nn wakiongelea fao la kujitoa. mfano mzuri hata kwa aliyeanzisha uzi hajazungumzia. Hii sherehe siku hiyo itakua imesheheni pongezi za mama
 
Tafadhali, mwenye uwezo atuwekee hicho kifungu tukisome neno kwa neno
 
Hakuna kuhudhuria wala kushadadia mei mosi
 
Fao la kujitoa kwani watu wajiajiri ili mzunguko wa fedha uzidi kuongezeka ktk jamii
 
Hii ni sherehe ya Watumishi wa Umma ndo maana hutasikia TUGHE wala nn wakiongelea fao la kujitoa. mfano mzuri hata kwa aliyeanzisha uzi hajazungumzia. Hii sherehe siku hiyo itakua imesheheni pongezi za mama
Hahahaa yaaan siku hiyo jina litatajwa hadi tutajificha chini ya meza
 
Hii ni sherehe ya Watumishi wa Umma ndo maana hutasikia TUGHE wala nn wakiongelea fao la kujitoa. mfano mzuri hata kwa aliyeanzisha uzi hajazungumzia. Hii sherehe siku hiyo itakua imesheheni pongezi za mama
Jitahidi tuliza kichwa ili uelewe
 
Sababu zitakazotolewa pale mtakapoambiwa mwaka huu mambo sio mazuri tuvumilie..
1. Vita vya Russia na Ukraine
2. Bank ya Dunia imetutoa uchumi wa kati
3. Mfumuko wa Bei nk
Hivyo ndugu watumishi tuendelee kuupiga mwingi kwa pamoja..
Meimosi oyeeeeeeee
 
Mkuu mm hapa n mfano mzuri,nimejitoa huko na wala sikatwi hiyo sjui ada ya uwakala.
 
Bango la mwaka huu la watumishi liwe na kauli fupi tu,,AHADI NI DENI,,, c mnakumbuka aliahidi mwaka huu atawaongeza mshahara
 
Mkuu mm hapa n mfano mzuri,nimejitoa huko na wala sikatwi hiyo sjui ada ya uwakala.
Of course, Kuna watu hawakatwi. Lakini as long as hiyo Sheria ipo Ni siku yoyote wakiamua unaweza kuanza kukatwa.

Mengine yote sawa lakini namba moja hapana kwa sababu hata ingekuwa wewe usingehamisha wafanyakazi kiholela bila kujali uhitaji.Pili ukiruhusu mtu ahamie anapopataka nani? atafanya kazi maeneo ya kijijini kwani wengi wanaomba kuhamia mjini kwa visingizio anamfuata mwenzi na vingine vingi ila issue kubwa wanataka kuhamia mjini.Wengine hawataki tu kufanyia kazi mkoa au wilaya fulani nao wanaomba uhamisho bila kuwa makini Kuna sehemu kutakuwa na upungufu wa wafanya kazi.
Binafisi nashauri uhamisho wa wafanyakazi uzingatie uhitaji na msawazo wa wafanyakazi.
 
Suala la upungufu wa watumishi si la mtumishi , ni la serikali kwa maana ndio yenye kuajiri. Mimi nimeshatumikia zaidi ya miaka 7 kituo fulani. Kuhama kwenda mahala ninapostahili ni haki yangu.
 
Afanye uhakiki wa watumishi tena maana ripoti ya CAG inaonesha bado Kuna watumishi hewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…