A
Anonymous
Guest
Mimi ni mtumishi wa Tanzania Forest Services (TFS), Kanda ya Magharibi, nikiwa katika ngazi ya chini kabisa ya kuanza utumishi. Nimeamua kueleza changamoto zinazotukabili baadhi ya watumishi katika eneo letu la kazi.
Kuna hali ambayo inaonekana kuwepo ya kutokuwepo kwa usawa katika malipo ya posho za safari na majukumu ya kikazi. Baadhi ya viongozi wanaposafiri kwa ajili ya kazi hujilipia posho kamili (full per diem), huku sisi watumishi wa ngazi za chini tunapokwenda kutekeleza majukumu ya kikazi tukilipwa nusu ya posho (half per diem), na wakati mwingine hatulipwi kabisa kwa maelezo kwamba majukumu hayo ni sehemu ya kazi zetu.
Vilevile, tunapotekeleza majukumu yanayozidi muda wa kawaida wa kazi, malipo yanayotokana na majukumu hayo huonekana kukadiriwa kwa kiwango cha chini, licha ya kwamba mara nyingi sisi ndio tunatekeleza kazi nyingi za field-oriented. Tunapohoji, tunaambiwa tusubiri mwaka mpya wa fedha, jambo ambalo limekuwa likitumika mara kwa mara kama sababu ya kuchelewesha au kutolipa stahiki hizo.
Changamoto nyingine ni katika idara ya uhasibu, ambapo kuna idadi kubwa ya watumishi, wakiwemo wengi walio kwenye mikataba. Pamoja na uwepo wa wahasibu wa kutosha, bado kuna malalamiko kwamba baadhi ya watumishi hushirikiana katika michakato inayosababisha fedha za shughuli tunazotekeleza kutolipwa kwa wakati au kupungua.
Hali hii imeongeza ukiritimba na malalamiko miongoni mwa watumishi, hasa wale wanaotekeleza majukumu ya uwanjani.
Tunaomba mamlaka husika ichunguze kwa kina mfumo wa malipo ya posho, stahiki za watumishi, pamoja na taratibu za usimamizi wa fedha katika ofisi hiyo, ili kuhakikisha kuna uwazi, usawa na uwajibikaji katika matumizi ya fedha za umma.
Watumishi wa ngazi za chini nao wana haki ya kupata stahiki zao kwa mujibu wa taratibu na kanuni za utumishi. Hatutaki upendeleo; tunataka usawa, uwazi na haki.