Watumishi wa serikali mliwezaje kutoboa, mbona mimi naenda kushindwa

Wengine hata 100k msosi wa mwezi haifiki, licha ya kuwa na access ya kutumia zaidi.
 
Achana nayo. Security wakati unakufa njaa.
 
Hivi Una mchumba?😆😊
 
Safi.
 
Huna mdogo ako wa kike mwenye akili kama wewe? unipasie
 
Mama anaupiga mwingi
 
Pole sana Mkuu.
Ushauri wangu ni kuwa
1.Simamia manunuzi yote mara upatapo mshahara,nakusudia nunua nyama,samaki,maharage weka kwenye friji katika vifurushi vidogo vidogo
Mfano:
Mchele 10kgs, Sembe 6kg
Nyama 4kgs weka parcels 12
Samaki wa 30,000, weka parcels 10
Maharage 3kg chemsha yote kwa mkaa aweke parcels 9 hadi 10. Umeme 20,000. Usiku kuleni vyakula vyepesi ndizi,viazi. Bana matumizi kiasi kwamba bills zote zisizidi 250,000.

Wazee watumie 50k. Achana na kulipia visimbuzi vya TV. Weka akiba 150k. Hii akiba ni lazima. Matibabu najua mna bima ya Afya.

Kila la kheri Mkuu
 
Sasa kama ndio unaanza kazi, unapata 613,000 unalia,

Siku ukikopa ukaanza kupata mshahara wa laki na nusu kwa mwezi mbona utajiua kabisa.

Najua wewe ni CO, na hiyo ndio tske home.

Mimi napata salary 260 000.

Nilikuwa na mshahara kama wako.

Nilikopa bank, nikaenda kununua viwanja nikatapeliwa.

Sasa hivi nalipa deni na kiwanja sina. Nimepambana lakimi nchi hii huwezi kupata haki, unadhulumiwa na aliyekudhulumu yupo anadunda na huna cha kumfanya.

Na nina mke na mtoto.

Na sijafa. Nipo tu natuliza moyo maisha mengine yaendelee.

Ushauri wangu.

Kama 613,000 take home haikutoshi, usije kukopa tena mkopo wa muda mrefu, maana bank za sasa zinakopesha mpaka mika 10, utakufa kabisa, maana utaanza kupata 200,000 wakati deni lako la bank halitaisha.

Na kama una passion ya biashara na uko mkoa mzuri au mkeo jichange ufanye kitu. Au kama una passion ya kilimo na mkoa unaruhusu lima.

Mimi niko Kilimanjaro, huku huwezi kulima hata bustani, kufuga wala biashara.

Naishi hivyo hivyo na 260,000 changu kwa kujibana.

Na usije ukawa na matumizi makubwa, sana, kadi yako ya bank itaishia kwa wakopeshaji wahuni wa mtaani, utashindwa kulipa kodi ya nyumba, itaonekana daktari njaa kali kinomaaa.

Na option ya madaktari huwa ni kuanza kupiga dili haramu, kama kutibu wagonjwa nje ya mfumo, kutoa mimba, na kuuza dawa kimchongo maisha yaende.

Utakuha kuanza kypata migogoro na wakuu wa wilaya, waganga wafawidhi, waganga wakuu wa wilaya na TAKUKURU. Utaanza kuhamishwa hamishwa vituo vya kazi kwa adhabu na Utapoteza focus na utaona kazi chungu.

Option kwa kipato kidogo huwa ni 2:
  • Kubana matumizi ya kipato ulicho nacho (njia rahisi) au
  • Kuongeza kipato chako (njia ngumu)

Pambana kujibana katika matumizi yako.
 
Hapo hutoboi, nunua chakula mda huu wa mavuno mahindi gunia 60k, mpunga gunia 60k x 2 = 120 hapo utakula mwaka mzima. Nunua mboga kama dagaa na maharagwe weka ndani wife kazi yake iwe kupika tu mtafutie na kijishughuli kimshughulishe kwenye hiyo 300k ya chakula umpaka hapo ushaokoa 200k hom tuma 50k na zinazobaki save ufungue biashara
 
Asante boss mawazo mazuri sana mkuu nimeyapokea
Shukrani.
Tupo pamoja.
Nyongeza:-
Siyo lazima kuchangia kila shughuli hasa za harusi na send-off.
Sehemu ya kutembea kwa miguu usipende kutumia usafiri wa kukodi au wa umma, tembea kwa miguu.
Kwa kipato chako usijipe majukumu ya kuhudumia nyumba ndogo. Michepuko ina gharama.
Usinunue chakula cha kwenda kupima kwa kilo kila siku au baada ya siku chache.
Kama unanunua sembe chukua kiroba cha 25kg bei ya jumla utaokoa pesa ya nyanya.
Ukifika wakati wa mavuno nunua mchele, maharagwe, kunde, choroko au mbaazi nyingi bei ikiwa ndogo tunza ndani.
Mafuta ya kula pia usinunue ya kupima kanunue kidumu cha Lita 3 au 5 utapumzika muda mrefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…