Watumishi wa serikali mliwezaje kutoboa, mbona mimi naenda kushindwa

Wewe safi🫡 unapiga spana haswaa
 
Anza kupunguza hiyo ela unayotuma kwenu,huo uwezo hujafikia
Hata hiyo unayompa wife nayo punguza,badala yake uisave umfungulie hata genge hapo nyumbani
Mana ukiweza kusave 50k kila mwezi kwa miezi hata 6 unapata laki 3 inatosha kabisa kwa genge especially uko mkoani!
 
Mpeleke mkeo short course VETA.. mambo ya kuoka...keki,mikate,ice cream etc... akimaliza kwa kuwa uko na ajira serikalini wewe kopa nunua jiko dogo la kawaida halafu mkeo awe anatengeneza hizo bites...atafute tenda kwenye maofisi..keki za birthday na harusi etc...kufunga ice cream kwa watoto wa shule..
 
Tushaishi kwa mshahara wa laki 3 na mambo yakaenda poa, kikubwa ni hisabati tu, jifunze kutataa ndugu wewe sio mzazi wao tuma pesa where necessary usiwalemaze kwamba wakutegemee wewe
 
Binafsi natumia "the 50-30-20 rule" ,
Ambayo ipo hivi:
Mahitaji ya msingi 50%: Hakikisha unalipa mahitaji yote muhimu mwanzoni mwa mwezi.

Matamanio 30%: Furahia maisha lakini kuwa na mipaka ili usiharibu akiba yako.

Akiba 20%: Kila mwezi weka pesa kwenye akiba na uwekezaji, hata kama kidogo.

NB:
Kama gharama za lazima zitapanda, kata matumizi ya starehe kwanza, sio akiba. Kama utakua una-make more unaweza adjust budgets zako.
 
Shida inanzia unapata mwanamke ambae kwenye bzness ni zero au mvivu.
 
Hapa nimekupata mkuu
 
Tushaishi kwa mshahara wa laki 3 na mambo yakaenda poa, kikubwa ni hisabati tu, jifunze kutataa ndugu wewe sio mzazi wao tuma pesa where necessary usiwalemaze kwamba wakutegemee wewe
Asante ila adui wa kwanza wa maisha yangu ni mke wangu

Mimi naona yeye ndie anayenitia umasikini ni mtu ambaye naona kabisa Wala haniulumii maana yeye ni mfujaji wa mambo.aisee.
 
Ili wazo zuri ngoja mwezi niende veta nikufuatulie course zao wanazotoa nimlipie ada tu akajifunza hata kushona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…