Watumishi wa serikali mliwezaje kutoboa, mbona mimi naenda kushindwa

Lakin 6 ni ndogo mtu ukiwa na familia. Yaani mm nachukua hiyo hiyo lakini maisha yanakimbiza mpaka sasa sina hata saving shilingi 10.
Utamlaumu tu wife anamatumizi mabaya ila hiyo pesa ni ndogo. Kikubwa tafuta njia mbadala ya kuongeza kipato
Embu tupe na ww mchanganuo wako wa hyo 6 inavyotumika huenda kuna sehemu na ww unakosea, 6 si ndogo khvyo
 
Sa si usimpe hiyo laki na 50,kwani usipompa atakufanya nini
 
Embu tupe na ww mchanganuo wako wa hyo 6 inavyotumika huenda kuna sehemu na ww unakosea, 6 si ndogo khvyo
Ninafamilia ya mkee na mtoto mmoja
Nina mtoto wa njee na hudumia
Nyumbani mama ananitegemea kula mwisho wa mwezi.
Kuna wadogo zangu nao wananipiga vizinga.
Nimepanga dar kama unavyojua gharama za maisha ya huko.
Nilikuwa nafanya starehe kidogo kidogo lakini nimeacha kabisa.
Na hapo mimi kila kitu ofisi inanigharamia kuanzia chakula usafiri hadi malazi na sikai na familia narudi tu likizo.
Sema matumizi ya watoto ndio imekuwa chanzo cha kutohifadhi pesa.
Mfano hapa nipo huku job uganda sijapokea hata pesa ya mshahara lakini nimeshatafutwa na wategemezi nikigawa naweza baki hata na 100k
 
Kwakweli ni changamoto, kwahyo kwny savings zako hauna kiasi chochote kabisa yani.?
 
Asante sana aisee
 
Ndo unaanza maisha, huwezi tatua shida zote za familia yenu au ukoo wenu... ongea na wife apunguze matumizi yasiyo ya lazima... weka malengo yako ndani ya miaka kadhaa Mungu yupo utafanikiwa tu...

Hebu jiulize haya maswali...
1. Kabla hujapata kazi hao nduguzo waliishije?
2.kabla hujapata hiyo kazi.. matumizi ya nyumbani na wife yalikuwaje?

Ukiweza kujibu hayo maswali, hebu chukua maamuzi...
 
Mpe kwa siku mkuu
 
Thanks.
Hongera rafiki kwa kufyeka kichaka cha medal 🏅 ya CAF.
Chukueni kabisa ubingwa deni liwe kwetu italeta ushindani na kukuza ligi yetu.
Asante sanaaaa
Kabisa rafiki yangu...
 
Hiyo 150k unayompa wife mwezi ujao usimpe usave.

Wanawake wana matumizi mengi ya hovyo yasiyo na maana yoyote.

Mpe hela anapohitaji siyo unakata kwenye chanzo kikuu Cha mapato yako kumpa ajihudumie anavyotaka.

Wazazi wako watumie hela wanapokuwa na shida siyo kila mwezi.
Inaweza kuona hapo haraka haraka unapata 250k inazagaazagaa.

Chakula nunua kwa mkupuo mmoja mfano debe la maharage, gunia la mahindi, debe tatu za mchele ukinunua hivyo unaweza kukaa miezi sita hujanunua nafaka. Hata mafuta na chumvi nunua kwa mkupuo.

Miezi mitatu tu utaona utofauti mkubwa sana.
 
naam naam , factos
 
Pole!

Kwa take home ya laki 6 huo ni mshahara mkubwa sana kwa serikali! Wengi wapo kwenye tune la laki 4.

Sasa kwanza ulianza vibaya maisha kwa kupanga nyumba ya laki 1, nadhani hii ilichagizwa na watu wanaokuzunguka hapo kazini lakini pia na wewe kutochukua tahadhali. Kujishusha chini ya hapo itakuwa ngumu kwa kuona aibu watu watakavyokusema!

Hivyo cha kufanya waeleze ndugu zako hali halisi unayopitia na sitisha mara moja fedha za kutuma nyumbani. Najua kutakuwa na negative reaction kutoka nyumbani lakini huna namna. Baada ya hapo angalia hiyo laki 1 inaweza kufanya nini katika kuongeza mapato yako kwa kufanya biashara hata ya kuuza maji na juisi.

Ili uweze kuuza maji na juisi chukua mkopo usiozidi milioni 2 nunua freezer ndogo na mkeo ajifunze kupika keki na biscuits. Fanya tathmini baada ya miezi 6.
 
ushauli wako ni mzuri sana
 
inaonekana mke wake ni wale wale, wabadilisha kucha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…