Watumishi wa serikali mliwezaje kutoboa, mbona mimi naenda kushindwa

Hii kitu huwa inanishangaza sana yani ukisema tu kuwa upo mkoani watu wanaamini upo shamba ni vituko kwakweli
 
Ile ya za kuambiwa changanya na zako ina apply mpaka kwenye salary.
 
Chunguza mkeo hachezi michezo yao ile kweli ya vikoba kweli? Hmmh? Matumizi ya mboga kwa siku 5000? Mnakula nusu ya nyama kila siku nini [emoji23][emoji23]

N'way big mistake nyingine huenda uliyoifanya ni kumwambia mkeo kipato chako unacho ingiza chote hadi posho huenda usha mwambia, so anajua hela hiyo ni nyingi....
 
Kuna kanuni moja inafanya Sana Kazi kwangu,Mimi nikiwa bahili maisha yanakuwa magumu kila kitu kinakwama,lakini nikitoa Sana/kutumia Sana pesa Kwa furaha kila kitu kinafunguka kila ninachogusa Ni mibaraka tu inatirirrika🤓🤓🤓🤓🤓
Kwa familia yako ya watu watatu naweza kuiendesha Kwa 300,000 Kwa mwezi wakala vizuri wakavaa mahitaji Yao yote muhimu wakapata!
 
N'way big mistake nyingine huenda uliyoifanya ni kumwambia mkeo kipato chako unacho ingiza chote hadi posho huenda usha mwambia, so anajua hela hiyo ni nyingi....
kuna mama mmoja alikua analalamika mumewe analipwa hela nyingi lakini hahudumii familia ipasavyo akaulizwa analipwa tsh.ngapi akasema Laki na 40🤓🤓🤓🤓
Sasa imagine huyu mama ndo angekuwa kaolewa na mtoa mada akajua analipwa Laki 6 Si balaa hilo😀😀😀😀
 
Kama mke wako anajitambua kopa uazishe mradi utakao kupa hela. Lkn zingatia kama anajitambua. Na isiwe mbali na wewe.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Duuh! Angeolewa na huyu mwamba angeona sasa maisha sindo haya mumewe ana fwedha mingi [emoji1]
 
Huo mshahara unatumaje nyumbani laki 1 zima waambie ukweli wewe bado lazima wajue mazingira yako ya kazi bado ujakaa sawa..

Kingine Watumishi wenzio wanaiba ndio maana unaona wanatoboa.

Ila kwa mshahara huo kweli kutoboa ngumu gharama za maisha kwa sasa ni kubwa sana.. najua situation yako mpambanaji!
 
Tuliishi maisha ya kujibana 1990s licha ya wazazi kuwa watumishi wa umma, tulikua nane, nyama kula mara mbili mshahara ukitoka,wazazi hawakusaidia familia zao,na hawakuwa na tamaa za kupiga hatua, tatizo vijana mnataka mwaka tu uwe na nyumba,gari nk, serikalini siyo pa hivyo,chukua mkopo fanya biashara,lima
 
huyo mkeo mshukuru sana bado anaonekana anajitahidi sana tsh 5000 kwa siku ya mboga? Ni mboga gani kwanza ya asubuhi na jioni? Ni mate mbele au maharage kila siku?

Punguza pesa unazotuma home kila mwezi.tuma nusu hiyo nusu save
 
Hio laki home wagonjwa ?
 
Halafu watakuja kumla au ataanza Kiburi biashara ikichanganya, wanaume tumeumbiwa tabu walai vile
Mkuu wakimla akiwa idle nyumbani? Hivi unajua ni rahisi mtu asiyejishungulisha kuliwa?

Kuhusu kiburi (biashara siyo yake ni ya familia) yeye anajilipa mshahara mapato yakibaki ni ya familia. Huwezi fuga mtu nyumbani mzee kuna kesho na kesho kutwa!
 
Nnacho amini ukifikisha mwaka kazn utajitafakari wewe mwenyew huhitaji hata ushauri.

Kwanza ondoka hapo ulipopanga tafuta unafuu wa Kodi.

Maji, taka na umeme lipa mwenyewe.

Vyakula kweli vina Bei kwa sasa ila kama una posho hatakama sio costant hiohio ndio iwe mhimili wa chakula .

Anza saving kwa malengo ya biashara au uwekezaji mdogo unaoweza .

Mwisho wa mwaka huu utajiona walau una ahueni flan itakayokupa nguvu zaidi .
 
Pole mwalimu, watumishi wenzako waliopo TRA, BoT, NCAA, MoF na maeneo mengine ya hivyo wametoboa.

Tatizo wewe upo Tamisenga, utachelewa sana huko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…