Watumishi wa serikali mliwezaje kutoboa, mbona mimi naenda kushindwa

Asante kaka je Kodi ya 100K Kwa huo mshahara ni sahihi maana Niko town niliwaza nipunguze nitafute hata nyumba hata ya ovyo ya 40 Kodi ili nipate muda wa kuutuliza kichwa
Kama mimi ningefanya hivi hama kwenye kodi ya 100K ingia chumba kimoja cha 40K au 30K,so kodi ya kulala 40K baki 60K hii mtumie mama nyumbani ile 100K uliyokuwa umamtumia i-save mpe tu uhalisia wa maisha yako atakuelewa hakuna mzazi anapenda kumuona mwanae akiteseka.

Kingine mtu anayeanza maisha si busara sana kuwa na chumba na sebule hii inakushawishi kununua vitu ambavyo kwa wakati huo huna kazi navyo zaidi unakuwa unachezea hela,umesema hapo juu una kitanda na godoro tu ni kusema vyumba vyote viko wazi kwanini usipange chumba kimoja?
 
Ndugu. Cha kukushauri jiunge na CHAWABATA.
Kuwa bahiri punguza matumiz yasiyo lazma ishi kwa ulefu wa kamba yako..
huko nyumban unawazoesha vibaya kwan hawajiwezi kwa sasa? na wao wajue unafamily na unajitafta, wape pexa kwa shda maalumu, ucpo angalia utatumika vibya kwan ndo jamii zetu(wazaz) wakisomesha hutegemea back up.

tafta pia nyumba ya kawaida tu pia lamwisho danganya umepunguziwa mshahara najua wanakupgia hexabu unachopata nawao wanaona hapo wataponea
 
Pole mwalimu, watumishi wenzako waliopo TRA, BoT, NCAA, MoF na maeneo mengine ya hivyo wametoboa.

Tatizo wewe upo Tamisenga, utachelewa sana huko
Wala Mimi sio mwalimu na Wala siko tamisemi.

Mimi Niko idara ya afya Tena ninaweza kumhudumia hata mzazi wako huku niliko sema umeanza dharau tu
 
Maisha ya sasa hivi si ya kutegemea mkono mmoja kama kipato hakitoshi,

Ushauri mwingine chukua mkopo mdogo muamzishie biashara mkeo awe pia anaingiza kitu, kuna kuumwa kaka au kufa familia itabaki kwa shida.

Angalia fursa yoyote ya kuwekeza ndugu yangu usimie wewe na mkeo

Ukiendekeza ndugu sana utaanguka

Kwa uzoefu wangu watumishiwengiwanaishi kwa nguvu za mikopo.

NB:Usikosee mkopo wa kwanza ukauchezea,ukichezea umetumbukia shimoni maana inakua na riba kubwa sanaa.
 
Mwamba wife wangu ana pigo kama hizo. Hapa nipo najipanga nimfungulie saloon ya kike maana anajua kusuka. Yani mke wa namna iyo mtafutie cha kufanya, asikae anawaza pesa yako tu, lazma ataitumia bila mpangilio maana hajui inavyotafutwa.
 
Ushauri murua huu shangaziii. πŸ™πŸ™πŸ™
 
k
kuwasaidia ni kuwaendekeza.
Kamwe tusije kosea kama hao wazazi omba omba tukaanza sumbua watoto baadae
 
kam wameamua ku mbless wazaz wao wala wasiache huo utaratibu hela ya kutumia freely ina raha yake.mzee nae anajilipa machungu ya ulez na uzaz.msiache kutuma hizo hela.wengine wanataman wawe wanawapa hela wazaz wao ila circumstances tu
machungu gani kwani mtoto kaomba kuzaliwa?
 
Nyama 2kg per month?
Basi mm utajiri nitausahau aiseeee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…