Watumishi wa UMMA kuweni makini na mikopo ya muda mrefu pamoja na baadhi ya taasisi

Watumishi wa UMMA kuweni makini na mikopo ya muda mrefu pamoja na baadhi ya taasisi

Kuna mdau kailaumu ccm hapo.

Loan literacy siyo ishu ya kusubiri serikali ikufundishe.

Unaona kuna taasisi ina riba 40% halafu wana insurance 5% wakati nyingine riba 16% na insurance 1% kwanini usiulize ili ueleweshwe?

Benki kazi yao ni kuuza pesa. Na wanatengeneza faida zaidi ikiwa utataka kulipa pesa waliyokupa kwa kipindi kirefu. Kama ni hivi kwanini wasikushawishi ulipe kwa muda mrefu? Wakijenga hoja kwamba kulipa mkopo kwa muda mrefu inakupa comfortability.

Na kama haujui utaamini kweli
Of course ukirejesha kwa miaka 10 ni sawa au zaidi ya wateja 5 wa miaka miwili miwili; nani angependa kupoteza hiyo opportunity ya kupata mteja wa kudumu kwenye biashara yake? Wanavuna pesa taratiiibu!
 
Habarini za wakati huu!

Kumekuwa na utitiri wa taasisi nyingi za ukopeshaji zikiwalenga watumishi wa umma, wakitumia njia mbalimbali kuwarubuni watumishi kukopa ktk taasisi zao huku wakijinadi kuwa mikopo yao ni ya riba nafuu halafu unapata ndani ya masaa 24.

Ingawa sijajua wanatoa wapi taarifa binafsi za watumishi hao, mfano namba za simu, majina pamoja na taasisi wanazofanyia kazi lakini wamekuwa ni kero sana kutuma meseji na kupiga simu.

Shida iliyopo ni kwenye gharama zao, kuwa juu kupita maelezo, mfano mtu anachukua 2M wataku force uilipe kwa muda mrefu mf. 12 months, ukikokotoa utajikuta unalipa mpaka 4M, hii nimeshaipiga kwny taasisi fulani ina jina la vitu vinavyochimbwa,

Rafiki yangu alichukua 4M for 10yrs, ukipiga hesabu ya pesa atakayolipa ni 24M, na mshahara atakaokuwa anapokea umebaki kadogo sana, nimemshauri awalipe tu.

Na wakijua unataka kuwalipa wanakuzungusha ajabu.

Binafsi nimeshindwa kujua taasisi kama BOT wanaozisimamia hizi taasisi ni kuwa hawahusiki na hizi riba wanazojiwekea au wameshindwa ku regulate hizi microfinance?

Kama mnavyojua hali ya maisha ni ngumu so wao wanatumia huo mwanya kuwahadaa watumishi na kufanikiwa kuwaingiza mkenge ambao mwisho wa siku wengi hujutia.

Jamani jamani watumishi, kama umebananishwa ni vyema muende kwenye mabenki (commercial banks) angalau wao riba zao zipo chini from 14 to 17 siyo hizo za 40, na ukichukua mkopo angalau usizidishe 3 to 4 years ikizidi san 5 but not 10 years.

Nimeona tusanuane, ikikufaa take it

Hizo Taasisi mnazijua so sina haja ya kuzitaja hapa

Unawezaje kukaa kwenye utumwa wa deni kwa miaka 5?
 
Well said mkuu, nadhani hizi taasisi za umma zitoe elimu kwa watumishi wake somehow itasaidia
Watumishi wa umma *******, Elimu yakifedha ni elimu binafsi watu hawataki kujifunza acha wapingwe. Ukimwambia soma hata page moja ya kitabu cha Richdad Poor dad anaona mzigo maanina wananitia hasira.
 
Kuna benk nilienda kukopa kwa miezi 6, wakanigomea, nikaenda Benk nyingine nayo wakaanza kunizungusha, mwisho wa siku nilikomaa wakanipa ila kwa mbinde karibia 2weeks, wanataka uchukue kwa muda mrefu hasa wakiiona salary slip yako.
 
Tumieni mfumo wa utumishi,mkopo unachukua hata wa miezi mi3
Na ni ndani ya saa 1, maximum 24hrs
 
Kuna mdau kailaumu ccm hapo.

Loan literacy siyo ishu ya kusubiri serikali ikufundishe.

Unaona kuna taasisi ina riba 40% halafu wana insurance 5% wakati nyingine riba 16% na insurance 1% kwanini usiulize ili ueleweshwe?

Benki kazi yao ni kuuza pesa. Na wanatengeneza faida zaidi ikiwa utataka kulipa pesa waliyokupa kwa kipindi kirefu. Kama ni hivi kwanini wasikushawishi ulipe kwa muda mrefu? Wakijenga hoja kwamba kulipa mkopo kwa muda mrefu inakupa comfortability.

Na kama haujui utaamini kweli
Umenena vyema, hii imewatafuna sana watumishi kabla ya ess kuanza.
 
Back
Top Bottom