Watumishi wa Umma waombwa na Hazina kuorodhesha Dini na Kabila zao. Rais Samia na Wasaidizi wako, haya yanafanyika kwa lengo gani?

Kwani uongo?

Hata kwa kuzingatia historia iko hivyo.

Elimu ililetwa na wamisionari (Wakristo), Muslims wachache sana walioamua kwenda kusoma Shule za makafiri ndio wakaanza kuwa wasomi nao wakati huo gap Yani pengo kubwa lilishajiweka baina ya wakristo wasomi na Muslims wasomi mpaka leo.

Muslims wengi wako mwambao wa Pwani ya bahari ya Hindi.

Je huko mwamko na mwitikio wa elimu ukoje?

Jamii zinahamasa ya kupenda kusoma kwa kiasi gani ukilinganisha na kwingine?

Angalia kuanzia Tanga, Morogoro, Pwani , Mtwara, Lindi kuna mwamko kiasi gani ukilinganisha na mikoa ya bara? Hususa kanda ya ziwa? Na magharibi achilia mbali kaskazini ukitoa Tanga ?

Dar es salaam ni ya pekee sababu ya mchanganyiko maalum.
Nikurekebishe hapo,ilikua lazima uwe kafiri ndio upate elimu kwenye shule zao wakati huo,na wapo waliobadili hata majina yao kutoka majina wa waislamu kua na majina ya kikristo ili wapate elimu na kazi pia HILO LIKO WAZI

Na endelea kujidanganya tu kua waislamu hawana elimu na ndio maana kwenye system na ajira mmejazana wakristo
 
Hiyo fomu inajumuhisha mambo mengi, vipi hilo ndio litaharukishe neva zako?!. Kuna mtu aiwahi kusailiwa popote bila kujaza dini na kabila? Tuna mengi ya kutafakari
 
Hizi dini ni utumwa tu
Kelvin...
Inategemea ni dini gani uliyokusudia.
Nakuwekea hapa Uislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika:

Soma makala hii hapo chini inaweza kuwa msaada kwako kuielewa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika na pia kuelewa jinsi Uislam ulivyotumika kuleta umoja wa wananchi katika kupambana na ukoloni:

DINI ILIVYOWAUNGANISHA WATANGANYIKA DHIDI YA UKOLONI: NAFASI YA DUA NDANI YA TANU VISOMO VYA QUR'AN NA DUA ZILIZOFANYIKA WAKATI WA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA: SEHEMU YA NNE

Inategemea watu watakavyoitumia dini.

Dini inaweza kutumika kuwaunganisha watu na pia inaweza kutumika kuwagawa.

Mikutano ya mwanzo ya TANU pale Mnazi Mmoja ilifunguliwa kwa dua na watu wakisoma Surat Fatha na kutikia dua hiyo kwa pamoja.

Aliyekuwa akiongoza dua hii alikuwa Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU.

Leo ni tabu sana kwa mtu kuamini kuwa hali ilikuwa hivi kuwa hata mikutano ya ndani ya TANU pale New Street ilikuwa ikifunguliwa na kufungwa kwa dua na Nyerere akiwapo.

Mwalimu Nyerere katika hotuba yake maarufu kwa Wazee wa Dar es Salaam Ukumbi wa Diamond wakati wa kustaafu urais mwaka wa 1985 alieleza kuhusu dua aliyofanyiwa na akashiriki nyumbani kwa Mzee Jumbe Tambaza.

Hotuba hii imekuwa maarufu sana khasa kipande hiki anachoeleza jinsi yeye Mkristo alivyopokelewa na Waislam wa Dar es Salaam akiwa na vijana wenzake Abdul Sykes na Dossa Aziz.

Hawa vijana wawili Abdul Sykes na Dossa Aziz, marafiki wa Baba wa Taifa ndiyo waliompeleka Mwalimu Nyerere kwa Mufti Sheikh Hassan bin Ameir kumtambulisha na kutaka msaada wake akubalike kwa Waislam na kuanzia siku ile Sheikh Hassan bin Ameir na Nyerere walikuwa wazalendo wawili wakisaidiana katika kudai uhuru wa Tanganyika Sheikh Hassan akiuza kadi za TANU ndani ya misikiti ya Dar es Salaam alikokuwa akidarsisha.

Turejee kwenye visomo na dua wakati wa kudai uhuru.

Lilikuwa jambo la kawaida sana wakati ule kwa Waislam waliokuwa katika mapambano na ukoloni kutanguliza mambo yao yote kutaka msaada wa Allah.

Hili lilikuwa jambo lililokuwa linakuja hata bila ya kufikiri.

Mwaka wa 1949 kabla ya mgomo wa makuli wa Bandari ya Dar es Salaam, walifanya kisoma na dua kubwa na baada ya hapo ndipo walipoingia barabarani kwa maandamano kama ishara ya kuanza mgomo.

Abdul Sykes alihusika sana katika mgomo huu.

Mwalimu Nyerere kwa hiyo hakuwa kiongozi wa kwanza katika harakati kufanyiwa kisomo na Waislam.

Mwalimu Nyerere yeye haya hakuyajua kwani alizikuta harakati katikati.

Abdul Sykes alikuwa Market Master Kariakoo Market nafasi kubwa sana wakati wa ukoloni na yenye wasaa na fursa za kutosha.

TANU ilipoanza Abdul Sykes akawa anauza kadi za TANU pale sokoni na Nyerere alikuwa hapungui ofisini kwake.

Special Branch wakiwafuatilia na siku moja Abdul Sykes akavamiwa na mkubwa wake Mzungu, Town Clerk ambae soko lilikuwa chini yake.

Abdul na huyu Mzungu walipambana kwa maneno makali Abdul akidai kuwa TANU kilikuwa chama halali na si kosa kuwa na kadi zake.

Hofu iliyotanda pale sokoni ilikuwa Abdul atafukuzwa kazi.
Abdul wakati ule Abdul alikuwa kijana wa miaka 30.

Wazee wafanyabiashara pale sokoni akina Sharif Mbaya Mtu, Mshume Kiyate, Shariff Abdallah Attas, huyu alikuwa mfanyakazi wa soko, mkusanyaji ushuru wa nafaka pale sokoni walijikusanya na pakafanyika dua kubwa ya kisomo na wakachinja mnyama.

Hii ilikuwa ndiyo dua ya kwanza kwa TANU kufanya kisha zikafuata dua aliyofanyiwa Rashid Ali Meli na ile ya Nyerere.

Rashid Ali Meli yeye alikuwa mweka fedha wa Dar es Salaam Municipal Council.

Rashid Ali Meli alifungua safe yake ofisini akatoa fedha kuikopesha TANU akamkabidhi Iddi Faiz Mafungo aliyekuwa Mweka Hazina wa TANU ili aziingize katika mfuko wa safari ya Nyerere UNO.

Siku ya pili wakaguzi wakaja ofisini kwake kufanya ukaguzi bahati nzuri hawakuanza na kukagua fedha taslimu.

Ilikuwa wazi kuwa endapo wakaguzi watagundua kuwa kuna upungufu wa fedha Rashid Ali Meli atashtakiwa kwa wizi na atafungwa.

Taarifa hizi ziliipofika ofisi ya TANU kitu cha kwanza kabisa ikawa pafanywe dua.

Baada ya kisomo hiki cha Rashid Ali Meli kikafuatia kisomo cha Lindi alichofanyiwa Baba wa Taifa na Sheikh Mohamed Yusuf Badi mwaka wa 1956 kisha ikafuatia dua ya Mnyanjani, Tanga kabla ya kwenda Tabora kwenye mkutano wa Kura Tatu uliotishia kuigawa TANU katika mapande mawili.

Picha hizo hapo chini ni Mkutano wa TANU Mnazi Mmoja miaka ya mwanzo ya TANU, picha ya pili ni kushoto Sheikh Suleiman Takadir, John Rupia na Julius Nyerere.

Picha ya tatu ni Soko la Kariakoo kama lilivyokuwa katika miaka ya 1950 na picha ya nne ni Shariff Abdallah Atttas.

Picha ya mwisho kulia ni Lawi Sijaona, Abdul Sykes, Julius Nyerere na Dossa Aziz katika hafla Ukumbi wa Arnatouglo kumuaga Nyerere safari ya pili UNO 1957.

Namaliza kwa kusema kuwa hivi ndivyo Waislam walivyoitumia dini yao katika kuleta umoja wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika umoja ambao hivi sasa haupo tena kwani uhuru ulikuja na changamoto zake na moja ya changanoto kubwa ikawa kuzuka kwa uadui dhidi ya Uislam ikawa chochote kinachowahusu Waislam hakiangaliwi kwa jicho la kheri na wale walioshika madaraka ya serikali.

Taratibu hata historia hii ya wazalendo hawa waliopigania uhuru ikawa haitakiwi na zikafanyika juhudi kubwa na za makusudi kuwafuta mashujaa hawa katika historia ya Tanganyika.

Wazee wetu wameonyesha kuwa dini inaweza kutumika kuwaunganisha watu.
Bahati mbaya sana leo dini inatumika kuwabagua watu.

MWISHO

1643430505003.png
 
Nikurekebishe hapo,ilikua lazima uwe kafiri ndio upate elimu kwenye shule zao wakati huo,na wapo waliobadili hata majina yao kutoka majina wa waislamu kua na majina ya kikristo ili wapate elimu na kazi pia HILO LIKO WAZI

Na endelea kujidanganya tu kua waislamu hawana elimu na ndio maana kwenye system na ajira mmejazana wakristo

Ni kama umekubaliana na ukweli nilielezea.

Sasa unazani hayo maamuzi ya kuanza kubadili dini ili kwenda Shule za wamisionari kusoma na kuajiriwa unazani kwa waislam ilikuwa ni rahisi kuitikia?

Swala la kubadili dini huwa si jepesi.

Hata ningekuwa mimi huenda nisingeikitikia kwa wepesi vile vile.

Sasa wakati waislam wanajiuliza waende kwenye hizo Shule kusoma na kubadili dini au wasiende wenzao wakristo walikuwa wako mashuleni wanasoma .

Mpaka waislam wachache wanakuja kuanza kupiga moyo konde na kuamua kubatizwa tayari kulishaweka pengo kubwa la walosoma wakristo na waislam.

Sasa haiwezi tokea kuja kuwa Sawa kutokana na hiyo historia.
 
Wakristo mnateseka sana katika hili,naona mnavojaribu kupindisha pindisha sentence
Nani apindishe waislamu akiwa Rais muislamu wasumbufu kwa Hugo raising hulazimisha vitu vya ajabu ajabu

Raising mwinyi alitandikwa makofi na mwislamu mwenzie kwenye shughuli ya kiislamu

Hakuna Mkristo aliwahi mtandika makofi raisi muislamu
 
Ni kama umekubaliana na ukweli nilielezea.

Sasa unazani hayo maamuzi ya kuanza kubadili dini ili kwenda Shule za wamisionari kusoma na kuajiriwa unazani kwa waislam ilikuwa ni rahisi kuitikia?

Swala la kubadili dini huwa si jepesi.

Hata ningekuwa mimi huenda nisingeikitikia kwa wepesi vile vile.

Sasa wakati waislam wanajiuliza waende kwenye hizo Shule kusoma na kubadili dini au wasiende wenzao wakristo walikuwa wako mashuleni wanasoma .

Mpaka waislam wachache wanakuja kuanza kupiga moyo konde na kuamua kubatizwa tayari kulishaweka pengo kubwa la walosoma wakristo na waislam.

Sasa haiwezi tokea kuja kuwa Sawa kutokana na hiyo historia.
Now days waislamu wenye master's degrees wako kibao tu,PhD holders wapo ajabu bado 80 kwa 20 tu

Kwann hamtaki 50/50?
 
Haya mambo haya mtu usipotumia akili vizuri ni rahisi kuharibu kbs,narahisi kuona kabila fulani linapendelewa au dini fulani inapendelewa lakini sio kweli.

Mfano utataka usawa bila kuzingatia idadi ya kundi lenyewe
Unaangalia idadi ya
Wasukuma mawaziri
Vs
Wazaramo mawaziri
Automatically lazima wasukuma watakuwa wengi kutokana na wingi wa watu kwenye kabila hilo lililozaa wawakilishi wengi bungeni hiyo ndiyo logic sasa utafosi vp iwe sawa ?

Na ukitumia akili sawasawa mfano malalamiko ya 20:80 ya Wakristo Vs waislam hayana maana
Coz idadi ya wakristo ni kubwa sana mfano tuu kwenye watanzania mil 60 waislam mil 9
Na wakristo mil. 51 hapo unashangaa vipi kuona waliowengi kiidadi wakiwa wengi pia kwenye ajira ni simple logic

Kwahiyo kama kuna kiongozi anatumia nguvu kusawazisha hiyo nature anataka kuharibu zaidi kuliko kutengeneza.
 
Akili...
Si kweli kuwa shule zimekuja na ukoloni.
Bahati mbaya unaandika kitu usichokuwa na ujuzi nacho.

Watu wa mwanzo kujua kile kinachoitwa 3Rs na wataalamu wa elimu ni Waislam, yaani Reading, Writing and Arithmetic.

Elimu yote hii ikisomeshwa katika madrasa na irabu zilizotumika zilikuwa za Kiarabu.
Wakoloni kwa hasad wakapiga marufuku matumizi ya irabu za Kiarabu na kuingiza za Kirumi.

Shule za wamishionari zilikuja baadae sana baada ya Berlin Conference 1884.

Kuna paper ya Ishumi unaweza kuipata Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kaeleza haya kwa kirefu.

Bahati mbaya jina na mwaka nimesahau.
Mimi nina p:aper mbili kuhusu Elimu na Waislam:

The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2003).

Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000’ (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15th – 17th 2003).

Nimekuwekea hizo paper hapo juu kukuzindua kuwa unazungumza na mtu aliyetafiti.
Nimeona jinsi unavyoandika unahitaji kusoma zaidi ili ulijue somo unalochangia.

Kwa kusoma ulichoandika ni kwamba unaafiki kile nilichoandika mimi.

Kwamba ni kweli gap au pengo la walosoma wakristo na waislam sababu zake ni za kuhistoria.

Sasa kama unasema elimu ya irabu ilifutwa na wakoloni wakaingiza za kirumi na baadae kuja wamisionari na masharti ya anayetakiwa kusoma awe Mkristo au abadili dini anatizwe ili asome na kupata kazi unazani kwa waislam ilikuwa rahisi kuitikia hilo kwa wakati?

Kwa hiyo ni wazi kwa wakristo ilikuwa rahisi kwa wao kwenda kusoma na kupata kazi kutokana na kwamba waendeshaji walikuwa wa imani moja.

Sasa kwa nini hamtaki kukubali ukweli badala yake mnaleta nongwa?!

Sasa mnawalaumu watanzania wenzenu ambao ni wakristo kana kwamba wao walikuwa sehemu ya wakoloni walokomesha elimu ya kiarabu ?

Je wakristo wakitanzania ndio waloweka masharti ya kimisonari ya kubatizwa?

Hizo zilikuwa external forces ambazo ilikuwa kuziitikia kwa kukubali na kupata matunda au kukataa usipate matunda yake.

Nani wa kulaumiwa.?!
 
Now days waislamu wenye master's degrees wako kibao tu,PhD holders wapo ajabu bado 80 kwa 20 tu

Kwann hamtaki 50/50?

Kadiri wasomi waislam wanavyoongezeka kuwa wengi fahamu kuwa wasomi wakristo wanaongeza kuwa wengi maradufu .
Kutokana na ile historia ilivyokuwa.

Wewe unaposema waislam wasomi phd , masters n.k wapo kibao ni wazi kwa wakristo wapo kibao zaidi maradufu kutokana na historia.

Labda ifike mahali ikatazwe wakristo waache kusoma kwanza kufidia gap Yani pengo lililopo ambalo ni la kihistoria sijui itachukua karne au miongo mingapi kisha idadi ikishakuwa sawa ndipo Wakristo waruhusiwe kuanza kwenda kusoma tena.

Lakini bila hivyo wakristo wataendelea kuwa na wasomi wengi zaidi kuliko waislam kutokana na sababu za kihistoria .
 
Haya mambo haya mtu usipotumia akili vizuri ni rahisi kuharibu kbs,narahisi kuona kabila fulani linapendelewa au dini fulani inapendelewa lakini sio kweli.

Mfano utataka usawa bila kuzingatia idadi ya kundi lenyewe
Unaangalia idadi ya
Wasukuma mawaziri
Vs
Wazaramo mawaziri
Automatically lazima wasukuma watakuwa wengi kutokana na wingi wa watu kwenye kabila hilo lililozaa wawakilishi wengi bungeni hiyo ndiyo logic sasa utafosi vp iwe sawa ?

Na ukitumia akili sawasawa mfano malalamiko ya 20:80 ya Wakristo Vs waislam hayana maana
Coz idadi ya wakristo ni kubwa sana mfano tuu kwenye watanzania mil 60 waislam mil 9
Na wakristo mil. 51 hapo unashangaa vipi kuona waliowengi kiidadi wakiwa wengi pia kwenye ajira ni simple logic

Kwahiyo kama kuna kiongozi anatumia nguvu kusawazisha hiyo nature anataka kuharibu zaidi kuliko kutengeneza.
Unamaanisha usukumani kuna wingi wa majimbo kuliko dar es salaam, halafu hii propaganda mnayoeneza kua eti wakristo ni wengi kuliko waislamu tnzania Siku mtaahindwa ficha sura zenu
 
Kadiri wasomi waislam wanavyoongezeka kuwa wengi fahamu kuwa wasomi wakristo wanaongeza kuwa wengi maradufu .
Kutokana na ile historia ilivyokuwa.

Wewe unaposema waislam wasomi phd , masters n.k wapo kibao ni wazi kwa wakristo wapo kibao zaidi maradufu kutokana na historia.

Labda ifike mahali ikatazwe wakristo waache kusoma kwanza kufidia gap Yani pengo lililopo ambalo ni la kihistoria sijui itachukua karne au miongo mingapi kisha idadi ikishakuwa sawa ndipo Wakristo waruhusiwe kuanza kwenda kusoma tena.

Lakini bila hivyo wakristo wataendelea kuwa na wasomi wengi zaidi kuliko waislam kutokana na sababu za kihistoria .
Nilichomaanisha ni kwamba kuwe na 50/50 kwenye hizi fursa,ukizungumzia usomi hata waislamu wanasoma na wamesoma after that

Sasa hoja ya kusema kwamba Christians wako wengi kwenye nyadhifa mbalimbali eti kwa sababu wao wana wasomi wengi kuliko waislamu hiyo ni rubbish
 
Kwa kusoma ulichoandika ni kwamba unaafiki kile nilichoandika mimi.

Kwamba ni kweli gap au pengo la walosoma wakristo na waislam sababu zake ni za kuhistoria.

Sasa kama unasema elimu ya irabu ilifutwa na wakoloni wakaingiza za kirumi na baadae kuja wamisionari na masharti ya anayetakiwa kusoma awe Mkristo au abadili dini anatizwe ili asome na kupata kazi unazani kwa waislam ilikuwa rahisi kuitikia hilo kwa wakati?

Kwa hiyo ni wazi kwa wakristo ilikuwa rahisi kwa wao kwenda kusoma na kupata kazi kutokana na kwamba waendeshaji walikuwa wa imani moja.

Sasa kwa nini hamtaki kukubali ukweli badala yake mnaleta nongwa?!

Sasa mnawalaumu watanzania wenzenu ambao ni wakristo kana kwamba wao walikuwa sehemu ya wakoloni walokomesha elimu ya kiarabu ?

Je wakristo wakitanzania ndio waloweka masharti ya kimisonari ya kubatizwa?

Hizo zilikuwa external forces ambazo ilikuwa kuziitikia kwa kukubali na kupata matunda au kukataa usipate matunda yake.

Nani wa kulaumiwa.?!
Akili...
Mjadala si huo

Mjadala unahusu dhulma iliyodumu toka uhuru hadi leo tuko 20:80.
 
Tena kwa bahati nzuri wakristo hawanaga tabia ya kuoendeleana kama waislam [emoji108] kwenye mambo mbali mbali.

Waislam wanapendeleana sana.

Mpaka wanakauli zao za kusema “ Muislam mwenzio ni ndugu yako “ maneno ya kufanana na hayo ngoja nitayaulizia vizuri.

Actually maneno kama hayo yanaweza kutafsiriwa kama yenye kubeba ubaguzi na upendeleo.

Kwamba asiye Muislam mwenzio siyo ndugu yako?

Wengine hadi kwenye taasisi wanaanzisha vikundi whassap group lao lakini wakristo hawanaga Habari na mambo ya udini kabisa.

Tupendane sisi ni watanzania sote.

Wengine tumechanganya upande wa mama Kuna wajomba waislam au kwa upande wa baba kuna mashangazi waislam n.k.
 
Kelvin...
Inategemea ni dini gani uliyokusudia.
Nakuwekea hapa Uislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika:

Soma makala hii hapo chini inaweza kuwa msaada kwako kuielewa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika na pia kuelewa jinsi Uislam ulivyotumika kuleta umoja wa wananchi katika kupambana na ukoloni:

DINI ILIVYOWAUNGANISHA WATANGANYIKA DHIDI YA UKOLONI: NAFASI YA DUA NDANI YA TANU VISOMO VYA QUR'AN NA DUA ZILIZOFANYIKA WAKATI WA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA: SEHEMU YA NNE

Inategemea watu watakavyoitumia dini.

Dini inaweza kutumika kuwaunganisha watu na pia inaweza kutumika kuwagawa.

Mikutano ya mwanzo ya TANU pale Mnazi Mmoja ilifunguliwa kwa dua na watu wakisoma Surat Fatha na kutikia dua hiyo kwa pamoja.

Aliyekuwa akiongoza dua hii alikuwa Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU.

Leo ni tabu sana kwa mtu kuamini kuwa hali ilikuwa hivi kuwa hata mikutano ya ndani ya TANU pale New Street ilikuwa ikifunguliwa na kufungwa kwa dua na Nyerere akiwapo.

Mwalimu Nyerere katika hotuba yake maarufu kwa Wazee wa Dar es Salaam Ukumbi wa Diamond wakati wa kustaafu urais mwaka wa 1985 alieleza kuhusu dua aliyofanyiwa na akashiriki nyumbani kwa Mzee Jumbe Tambaza.

Hotuba hii imekuwa maarufu sana khasa kipande hiki anachoeleza jinsi yeye Mkristo alivyopokelewa na Waislam wa Dar es Salaam akiwa na vijana wenzake Abdul Sykes na Dossa Aziz.

Hawa vijana wawili Abdul Sykes na Dossa Aziz, marafiki wa Baba wa Taifa ndiyo waliompeleka Mwalimu Nyerere kwa Mufti Sheikh Hassan bin Ameir kumtambulisha na kutaka msaada wake akubalike kwa Waislam na kuanzia siku ile Sheikh Hassan bin Ameir na Nyerere walikuwa wazalendo wawili wakisaidiana katika kudai uhuru wa Tanganyika Sheikh Hassan akiuza kadi za TANU ndani ya misikiti ya Dar es Salaam alikokuwa akidarsisha.

Turejee kwenye visomo na dua wakati wa kudai uhuru.

Lilikuwa jambo la kawaida sana wakati ule kwa Waislam waliokuwa katika mapambano na ukoloni kutanguliza mambo yao yote kutaka msaada wa Allah.

Hili lilikuwa jambo lililokuwa linakuja hata bila ya kufikiri.

Mwaka wa 1949 kabla ya mgomo wa makuli wa Bandari ya Dar es Salaam, walifanya kisoma na dua kubwa na baada ya hapo ndipo walipoingia barabarani kwa maandamano kama ishara ya kuanza mgomo.

Abdul Sykes alihusika sana katika mgomo huu.

Mwalimu Nyerere kwa hiyo hakuwa kiongozi wa kwanza katika harakati kufanyiwa kisomo na Waislam.

Mwalimu Nyerere yeye haya hakuyajua kwani alizikuta harakati katikati.

Abdul Sykes alikuwa Market Master Kariakoo Market nafasi kubwa sana wakati wa ukoloni na yenye wasaa na fursa za kutosha.

TANU ilipoanza Abdul Sykes akawa anauza kadi za TANU pale sokoni na Nyerere alikuwa hapungui ofisini kwake.

Special Branch wakiwafuatilia na siku moja Abdul Sykes akavamiwa na mkubwa wake Mzungu, Town Clerk ambae soko lilikuwa chini yake.

Abdul na huyu Mzungu walipambana kwa maneno makali Abdul akidai kuwa TANU kilikuwa chama halali na si kosa kuwa na kadi zake.

Hofu iliyotanda pale sokoni ilikuwa Abdul atafukuzwa kazi.
Abdul wakati ule Abdul alikuwa kijana wa miaka 30.

Wazee wafanyabiashara pale sokoni akina Sharif Mbaya Mtu, Mshume Kiyate, Shariff Abdallah Attas, huyu alikuwa mfanyakazi wa soko, mkusanyaji ushuru wa nafaka pale sokoni walijikusanya na pakafanyika dua kubwa ya kisomo na wakachinja mnyama.

Hii ilikuwa ndiyo dua ya kwanza kwa TANU kufanya kisha zikafuata dua aliyofanyiwa Rashid Ali Meli na ile ya Nyerere.

Rashid Ali Meli yeye alikuwa mweka fedha wa Dar es Salaam Municipal Council.

Rashid Ali Meli alifungua safe yake ofisini akatoa fedha kuikopesha TANU akamkabidhi Iddi Faiz Mafungo aliyekuwa Mweka Hazina wa TANU ili aziingize katika mfuko wa safari ya Nyerere UNO.

Siku ya pili wakaguzi wakaja ofisini kwake kufanya ukaguzi bahati nzuri hawakuanza na kukagua fedha taslimu.

Ilikuwa wazi kuwa endapo wakaguzi watagundua kuwa kuna upungufu wa fedha Rashid Ali Meli atashtakiwa kwa wizi na atafungwa.

Taarifa hizi ziliipofika ofisi ya TANU kitu cha kwanza kabisa ikawa pafanywe dua.

Baada ya kisomo hiki cha Rashid Ali Meli kikafuatia kisomo cha Lindi alichofanyiwa Baba wa Taifa na Sheikh Mohamed Yusuf Badi mwaka wa 1956 kisha ikafuatia dua ya Mnyanjani, Tanga kabla ya kwenda Tabora kwenye mkutano wa Kura Tatu uliotishia kuigawa TANU katika mapande mawili.

Picha hizo hapo chini ni Mkutano wa TANU Mnazi Mmoja miaka ya mwanzo ya TANU, picha ya pili ni kushoto Sheikh Suleiman Takadir, John Rupia na Julius Nyerere.

Picha ya tatu ni Soko la Kariakoo kama lilivyokuwa katika miaka ya 1950 na picha ya nne ni Shariff Abdallah Atttas.

Picha ya mwisho kulia ni Lawi Sijaona, Abdul Sykes, Julius Nyerere na Dossa Aziz katika hafla Ukumbi wa Arnatouglo kumuaga Nyerere safari ya pili UNO 1957.

Namaliza kwa kusema kuwa hivi ndivyo Waislam walivyoitumia dini yao katika kuleta umoja wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika umoja ambao hivi sasa haupo tena kwani uhuru ulikuja na changamoto zake na moja ya changanoto kubwa ikawa kuzuka kwa uadui dhidi ya Uislam ikawa chochote kinachowahusu Waislam hakiangaliwi kwa jicho la kheri na wale walioshika madaraka ya serikali.

Taratibu hata historia hii ya wazalendo hawa waliopigania uhuru ikawa haitakiwi na zikafanyika juhudi kubwa na za makusudi kuwafuta mashujaa hawa katika historia ya Tanganyika.

Wazee wetu wameonyesha kuwa dini inaweza kutumika kuwaunganisha watu.
Bahati mbaya sana leo dini inatumika kuwabagua watu.

MWISHO

View attachment 2099044
Hii historia inapaswa idumishwe na ienziwe.
Tatizo hatusomi historia.
ahsante mkuu kwa kutukumbusha.
 
Tena kwa bahati nzuri wakristo hawanaga tabia ya kuoendeleana kama waislam [emoji108] kwenye mambo mbali mbali.

Waislam wanapendeleana sana.

Mpaka wanakauli zao za kusema “ Muislam mwenzio ni ndugu yako “ maneno ya kufanana na hayo ngoja nitayaulizia vizuri.

Actually maneno kama hayo yanaweza kutafsiriwa kama yenye kubeba ubaguzi na upendeleo.

Kwamba asiye Muislam mwenzio siyo ndugu yako?

Wengine hadi kwenye taasisi wanaanzisha vikundi whassap group lao lakini wakristo hawanaga Habari na mambo ya udini kabisa.

Tupendane sisi ni watanzania sote.

Wengine tumechanganya upande wa mama Kuna wajomba waislam au kwa upande wa baba kuna mashangazi waislam n.k.
Akili...
Mjadala si huu.

Soma fikra zangu kote katika mjadala huu utaelewa nini nazungumza.
 
Dhuluma kwa namna gani @ Kaka?

Inaweza kuthibitishwa hiyo dhuluma?
Akili...
Inaelekea wewe ni mgeni hapa.
Si kitu.

Inabidi uanze kusoma alif kwa kijiti.
Hapa JF kuna post nyingi sana nimeandika na nyingine kuchangia.

Anza kusoma hizo nyingine zinakwenda nyuma miaka 10.
 
Back
Top Bottom