Waumini wa Kanisa Katoliki ni wavumilivu sana

Waumini wa Kanisa Katoliki ni wavumilivu sana

ACHA kukariri.
Nani kakudanganya ukipiga magoti kilichopo mbele Yako unakiabudu kuwa ndio Mungu?
Akili za wapi hizo?

Kwa hiyo nyie mkiwa katika kusali chochote kilichopo mbele yenu mnakiabudu na kukigeuza kuwa Mungu wenu?
Mungu haabudiwi kwa kukariri.
Mkuu asante kwa mawazo yako. Naamini umejifunza kitu. Na mimi pia nimejifunza kitu kutoka kwako
 
Wote wanaakili ndogo. Wanakubali vipi kuwekwa Masanamu kwenye nyumba Ibada, hali ya kuwa tunajua fika hayadhuru wala hayanufaishi ?

Akili iheshimiwe.
Hii ndo akili ndogo sasa tunayoizungumzia. Asante kwa kujitokeza
 
Swala ni kuinama kwenye sanamu au kuipa Sanamu ukuu sawa na Mungu?
Mungu kakataa kuinamia Sanamu au kuzipa Sanamu ukuu SAWA NA MUNGU?.

Mnaona mnavyoteseka Kwa kutoyaelewa maandiko?
Mkuu nashukuru kwa mawazo yako nimejifunza kitu, ni matumaini yangu pia umejifunza kitu
 
Mkuu, wanadamu waliokufa hawawezi kutusaidia katika kupitisha maombi yetu kwenda kwa Mungu. Lakini kama utakua na ushahidi wa Kibiblia ukatupatia nitafurahi maana takua nimejifunza kitu
Ushahidi nimeshakupa SEMA una mafundisho Yako kichwani.

Mfu hawezi kufikisha maombi Kwa sababu kafa.

Kuna madhehebu ambayo ni wafu mfano SDA.Hao hawawezi kumwombea Mtu Kwa sababu ni wafu na ndio maana Yesu alisema tuache wafu wazike wafu wao.

Mtu unaweza kuwa mfu wakati unatembea.

Mkristo sio mfu.hata akiiacha hii dunia anaendelea kuwa hai.

Na wakristo tunashauriwa kuombeana siku zote.

Kwa hiyo Bikira Maria Kwa kuwa ni Mkristo,tunaamini yupo hai natunamshirikisha kwenye maombi yetu.
 
Ukweli ni kwamba ukatoliki siyo ukristo wa kibiblia. Na kuhusu uvumilivu, hata freemason ni wavumilivu japo wanasemwa sana pia, ni kawaida ya waumini ya imani yoyote ile kuvumilia, iwe imani potofu au sahihi.
Uvumilivu ni sifa ya KiMungu.
Mungu ana Kanuni zake alizozirithisha Kwa Kanisa Katoliki.
 
Waislamu siwezi kuwasemea lakini Wakristo wengine wanawashutumu Wakatoliki kwa sababu wanafundisha mambo ambayo ni unbiblical na mambo ambayo yalirithiwa kutoka katika desturi za Dini za Kipagani za Kirumi na Kiyunani
Kama wengine mko sahihi kwanini mgawanyike
 
Hapa penyewe panaonyesha usivyoekewa.
Kumbe Lazaro alipoiacha hili dunia hakufa?
Huoni alikuwa kifuani kwa ibrahimu?.

Hizo hadithi zenu za Mkristo anakufa na hastahili kushirikishwa kwenye maombi yetu mnazitoa kwenye Biblia IPi?
Mkristo anakufa mwili, ila roho haifi, huwa inaenda mahali, na haina direct communication na wenye mwili. i hope hapo umeelewa.
 
Halafu Roman Catholic ni kwaajili ya Italy tu.Mmakonde,Mmachinga,Mmsai,Mchagga au Mnyakyusa na Catholic wapi na wapi !.Umewahi kuona au kusikia Pope Mwafrika au Mungu wa wa Catholic ni Mungu kwaajili ya wazungu pekee yake.
Pope mu afrika,,, fatilia vzuriii ,,, usifanye vitu kwa kurupuka
 
Una uhakika kwamba hakuna padri aliyeponya wagonjwa ?? Sio kweli .,, soma .historia ya padri pio wa petrocina angali akiwa hai na mambo aliyokuwa akiyafanya

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
kitu kimenishindaga tabia kwa wakatoliki ni salamu maria utuombee kwa mungu hivi huwa mna sahau kuwa maria ni binadamu kama ninyi? Japo ali mzaa Yesu kristo. Mimi hapo ndipo ninapo pataga ukakasi kwa sababu naonaga ni kama vile kumkosea heshima Mungu kwanini msimuombe Mungu mwenyewe, why Maria? Ninacho jua mimi Maria ni mwanamke aliye barikiwa kuliko wanawake wote basi na ndio maana alimzaa Yesu. naomba wanao jua zaidi waje wanikosoe hapa na kunielimisha zaidi kuhusu hili.
Vitu vingine ni rahisi tu kuelewa. Mbona we unaenda kwa mchungaji wako unamwambia akuombee? Je yeye sio binadamu wa kawaida? Mbona unamwambia mwenzio akuombee? Je yeye sio binadamu wa kawaida?

Kuomba Maria atuombee wala sio ajabu. Hata we unaweza ukamwambua yoyote akuombee na ukafanikisha
 
Na ndo ilivyo mzee.
Hii nchi tu rais yoyote akitoka upande wa imani ya kikristu lazima awe mkatoliki
Anzia Nyerere,mkapa hadi JPM.
Kwenye deep state RC wamejichomeka vilivyo.

KALENDA UNAYOTUMIA INAITWA GREGORIAN CALENDAR ILIANZISHWA NA POPE GREGORY WA VATICAN.

Taasisi imara inachangiwa h na kudumu muda mrefu pia.

Huwezi fananisha kanisa katoliki na dini za walokole..
Nimemuelewa vile!
Nasikia mchungaji Marehemu Rwakatare huko wanagombea Mali,
Hatari Sana!
 
alikuwa anamwelekeza yohana amtunze/amlee. hata kiswahili cha kawaida kabisa hapo kinaeleweka. maria alikuja kufa, hakufufuka hadi leo. Yesu hakuwa anaelekeza tusali kupitia maria, hakumaanisha maria awe mbadala wake.
Na hakuna mahali kanisa katoliki linafundisha kuwa Maria ni mbadala wa Yesu.
Hebu sali salamu Maria hapa uone kama kuna mahala umeambiwa usimuombe Mungu.
" Salamu Maria,
umejaa neema,
bwana yu nawe,
umebarikiwa kuliko wanawake wote,
Na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Maria mtakatifu,
mama wa Mungu,
Utuombee sisi wakosefu,
Sasa na saa ya kufa kwetu.
Amina."


Wapi umeambiwa umbadili Yesu na Maria?
Jifunze ukatoliki utaelewa kila kitu. Na kila kitu kipo kwa maana
 
Ushahidi nimeshakupa SEMA una mafundisho Yako kichwani.

Mfu hawezi kufikisha maombi Kwa sababu kafa.
Kuna madhehebu ambayo ni wafu mfano SDA.Hao hawawezi kumwombea Mtu Kwa sababu ni wafu na ndio maana Yesu alisema tuache wafu wazike wafu wao.
Mtu unaweza kuwa mfu wakati unatembea.
Mkristo sio mfu.hata akiiacha hii dunia anaendelea kuwa hai.
Na wakristo tunashauriwa kuombeana siku zote.
Kwa hiyo Bikira Maria Kwa kuwa ni Mkristo,tunaamini yupo hai natunamshirikisha kwenye maombi yetu.
Mkuu sote twajifunza tuu hapa. Sijui una maoni gani na maandiko haya:-


Ecclesiastes 9:5
[5]
kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.


Deuteronomy 18:10-11
[10]
Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,
[11]
wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.
 
Bikira Maria anaabudiwa na Wakatoliki, siyo chombo cha kupitisha maombi yaende kwa Mungu pekee. Ndo maana mnapiga magoti kwenye sanamu lake mkiwa mnamuabudu, kama unabisha nenda kanisa la St Joseph pale posta kuna kijumba kina sanamu la Maria na watu huenda pale kuliabudu wanapiga magoti na rozali zao mikononi. Sasa hii si ni ibada ya sanamu hii. Kama kuna mchungaji anapigiwa magoti na kuabudiwa ili maombi yetu yaende naye na kanisa lake ni kundi hilohilo moja na kanisa Katoliki. Wakuabudiwa ni Mungu pekee
Hujui kuabudu wewe.

Kanisa katoliki halimuabudu bikira Maria bali linamuheshimu.

Hayo ndo mafundisho ya kanisa. Hayo mengine ni mawazo yako wala hakun mahali kanisa linafundisha kumuabudu bikira Maria.
 
Na hakuna mahali kanisa katoliki linafundisha kuwa Maria ni mbadala wa Yesu.
Hebu sali salamu Maria hapa uone kama kuna mahala umeambiwa usimuombe Mungu.
" Salamu Maria,
umejaa neema,
bwana yu nawe,
umebarikiwa kuliko wanawake wote,
Na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Maria mtakatifu,
mama wa Mungu,
Utuombee sisi wakosefu,
Sasa na saa ya kufa kwetu.
Amina."


Wapi umeambiwa umbadili Yesu na Maria?
Jifunze ukatoliki utaelewa kila kitu. Na kila kitu kipo kwa maana
Deuteronomy 18:10-11
[10]
Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,
[11]
wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.
 
Back
Top Bottom