Waumini wa Kanisa Katoliki ni wavumilivu sana

Kwa nini siyo ibada ya sanamu? Au nyoka wa shaba siyo sanamu?
Ngoja nikufundishe kidogo.
Ibada ya Sanamu ni kuitegemea Sanamu na kuifanya ndio Mungu.

Nyoka wa Shaba enzi za Musa hakufanywa Mungu Kwa hiyo haikuwa Ibada ya Sanamu.
 
Mkuu mimi nafahamu , baada ya kuja Yesu taratibu za ibada zilibadilika. Hatutazami tena nyoka wa shaba( mfano mnavyotazama ma misalaba na masanamu ya Maria kanisani) maana Yesu ndiyo nyoka wetu wa shaba aliyeinuliwa , pia hatutoi sadaka za damu tena kwa maana Yesu alimwaga damu tayari kwa ajili yetu
 
Ule ni mwili wake kweli.
Someni maandiko vizuri.

Luka 22:19-38
Halafu akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa akisema,

“Huu ni mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu.

Fanyeni hivi kwa kunikumbuka.”
Hapa tuko sawa mkuu, hata mimi leo Padri aweza kunikomunisha. Lakini kunipigisha magoti ibadani mbele ya masanamu na misalaba hapana
 
Kwa nini siyo ibada ya sanamu? Au nyoka wa shaba siyo sanamu?
Kwa akili ya namna hii utadai hata Musa kupiga mwamba maji yakatoka ni ibada ya Sanamu,
Maajabu yote aliyofanya Musa Kwa pharaoh mpaka wakaruhusiwa utadai ni ibada ya Sanamu.

Get up man.
Toka huko Kwa wajanjawajanja wanaowapiga sadaka Kwa mahubiri feki.
 
Kuna sehemu Mungu alisema watu wasali Jumamosi?.
Mimi siyo msabato, hoja yangu ni kwamba mfalme alibadili ibada kutoka Jmosi kwenda Jpili. Maana ulisema nikupe jambo moja ambali hao ma kaizari walibadili ktk ibada.
Karibu
 

Hiyo misingi ya kimaandiko ni ipi mkuu tujifunze maana maandiko yanasema

Mathayo : 3 : 16 - Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake;

Yesu ambaye ni kiongozi wetu baada ya kubatizwa alipanda kutoka majini. Kwa nini kanisa katoliki likaanzisha msingi wa kunyunyiza tofauti na alivyofanya Bwana wetu Yesu Kristo.
 
Kwanza Kabisa unatakiwa ukubali kwamba huelewi kitu.

Taratibu za ibada kabla ya Yesu zilikuwa hazihusiani na masanamu yaliyokuwepo hekaluni.

Ibada ya ondoleo la dhambi ilihusiana na umwagikaji wa damu ya wanyama.
Walikuwa hawaabudu Sanamu hata kidogo ijapokuwa zilikuwepo kwenye nyumba zao zaibada na hata kwenye sanduku la agano.

Damu ya Yesu ndio imekuja kuondoa habari za Damu na makafara ya Wanyama.

Vipi kuhusu Sanamu zilizokuwepo kwenye mahekalu?

Hakuna popote kwenye agano la kale Mungu alipogawa utukufu wake kwenye sanamu.

Mwambie mchungaji wako asome vizuri Biblia.
 
Yesu alibatizwa ubatizo wa Yohana mbatizaji.
Unataka na sisi tubatizwe ubatizo wa Yohana mbatizaji.
 
Hapana mkuu, rudi unisome vizuri.
John 3:14
[14]And as Moses lifted up the serpent in the wilderness, even so must the Son of man be lifted up:
Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa;

Tunamuabudu mwana wa Adamu ambaye aliyeinuliwa kama maandiko yasemavyo hapo juu amefananishwa na nyoka wa shaba wa Musa means kwamba nyoka wa shaba pia aliabudiwa
Nyoka wa shaba=mwana wa Adamu(Yesu)
 
Mimi siyo msabato, hoja yangu ni kwamba mfalme alibadili ibada kutoka Jmosi kwenda Jpili. Maana ulisema nikupe jambo moja ambali hao ma kaizari walibadili ktk ibada.
Karibu
Sio kweli.
Waliokuwa wakifanya ibada Jumamosi ni Wayahudi.
Wakristo walikuwa wanakusanyika Jumapili tangu enzi za Mitume.
 

Roman Catholic
 
Kila jambo lina historia yake.
Ukatoliki ni mfumo kamili unaotumia Dola kutawala Dunia.
Kuna nchi Moja ilitaifisha Mali za dini nyingine na Wafanyabiashara Kwa mahesabu makali sana.
Kwanza, serikali hiyo ilijua fika kuwa wasomi wengi walioajiriwa Serikalini ni waRumi. Hivyo serikali ikidhoofisha mifumo ya kujiajiri kwenye biashara na taasisi za dini nyingine waRumi hawataathirika wataibuka kupitia ofisi za umma na kutoa ajira Kwa watoto wao. Ndicho kilichotokea.

Matajiri wengi tangu enzi za mkoloni walikua ni WA dini ya kiislam na waanglikana na Wale wafuasi wa Martini. Baada ya uhuru mahesabu yakapigwa na watawala wasomi ambao wengi walikua ni waRumi wakatafuta namna ya kushika uchumi na siasa ikabidi watangaze kutaifisha Mali za watu Kwa kuwaita mabepari.

Wakati muingereza anaondoka kwenye nchi Fulani kanisa la la Anglikana lilikua na nguvu kubwa kiuchumi na kitaasisi.
Mali zao zote ziliraifishwa na kuliacha likiwa hoi ukizingatia watawala walioibukia walitaifisha Kwa mahesabu ya mbali sana.

Kule Kwa Uganda aliibuka Dada mmoja akataka kutaifisha Mali za wafanyabiasha wa kigeni kama alivyofanya wa nchi Ile lakini alikutana na mguvu ya Dola la kirumi.

Ni mahesabu na uvumilivu TU. Ukiona vinaelea vimeundwa
 
Unachanganya mambo mengi mno Kwa wakati mmoja.
Haupo consistent.
Mfanano wa kuinuliwa nyoka wa Shaba na Kuinuliwa Kwa Yesu haupo kwenye muktadha wa Ibada.
Ibada zilikuwa zinafanyika hekaluni ambapo palikuwa na masanamu.
Huko ndipo wanyama walichinjwa na damu iliyomwagika ilikuwa ni Kwa ajili ya ondoleo la dhambi.

Damu ya Yesu kumwagika nalo ndio ondoleo la dhambi kwetu.

Point kubwa ni kwamba Mungu hakuwahi kuwaambia waziabudu Sanamu.

Huu ni uongo wa wazi unaotakiwa ukamfafanulie mchungaji wako.

Sanamu zilikuwepo,zipo na zitaendelea kuwepo maana hazijawahi kufananishwa na Mungu.
 
Hapa tuko sawa mkuu, hata mimi leo Padri aweza kunikomunisha. Lakini kunipigisha magoti ibadani mbele ya masanamu na misalaba hapana
Lazima uone fahari Kwa msalaba uliotumika kukukomboa.

Galatians 6:14 .
But God forbid that I should boast
except in the
cross of our Lord Jesus Christ,
by whom the world has been crucified to me, and I to the world.
 
Nazungumzia kitu halisi na wala sina haja wala nia ya ubishi... Nazungumzia maneno yanayotamkwa kila kukicha na wakatoliki kwamba "Mtakatifu fulani UTUOMBEE" . Sina haja ya kufuatilia hoja za CATHOLIC ANSWERS waniambia nini maana ya neno UTUOMBEE kwasababu hakuna neno linaloweza kutumika mbadala ya lingine halafu halina maana ile iliyokusudiwa....
 
Ufafanuzi wa haya umetoa wapi? Weka hata chanzo cha uongo.


1 Wakorintho

25 Kwa maana huu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi kuliko hekima ya wanadamu, na ’udhaifu’ wa Mungu una nguvu ipitayo nguvu ya wanadamu.
Ufafanuzi wa nini wakati umempinga mpaka binadamu yake muhammad

Aya ipo wazi walikuwa wanamtengenezea masanamu

Koran 64:13. Walikuwa wakimfanyia alipendalo, kama mihrabu, na masanamu, na madeste makubwa kama mahodhi, na masufuria makubwa yasiyo ondolewa mahala pake. Enyi watu wa Daudi! Fanyeni kazi kwa kushukuru. Ni wachache katika waja wangu wanao shukuru
 
Endelea kukata viuno kanisani. Ikiwa biblia hamuelewi Kwa kuwekwea hadi movie ya 'Brian Deacon'. Nimekuuliza lete ufafanuzi wa hiyo ya msikitini kuwekwa masanamu. Hata hiyo reference uliyoingizwa chaka hakuna mahali masanamu yalikuwa yanajengwa msikitini. Usilazimishe tuwe sawa na
nyie makafiri



1 Wakorintho

25 Kwa maana huu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi kuliko hekima ya wanadamu, na ’udhaifu’ wa Mungu una nguvu ipitayo nguvu ya wanadamu.
 
Ufafanuzi wa haya umetoa wapi? Weka hata chanzo cha uongo.


1 Wakorintho

25 Kwa maana huu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi kuliko hekima ya wanadamu, na ’udhaifu’ wa Mungu una nguvu ipitayo nguvu ya wanadamu.
Koran34:12. Na Suleiman tuliufanya upepo umtumikie. Safari yake ya asubuhi ni mwendo wa mwezi mmoja, na safari yake ya jioni ni mwendo wa mwezi mmoja. Na tukamyayushia chemchem ya shaba. Na katika majini walikuwako walio kuwa wakifanya kazi mbele yake kwa idhini ya Mola wake Mlezi. ...

Yani mnajifanya hamnazo kabisa

Jibu kwa nini Allah alituma majini yakatengeneza masanamu na kuyaweka msikitini?
 
Suleiman ni dini gani? Kwa mujibu wa allah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…