The Worst
JF-Expert Member
- Sep 12, 2021
- 6,108
- 21,140
kitu kimenishindaga tabia kwa wakatoliki ni salamu maria utuombee kwa mungu hivi huwa mna sahau kuwa maria ni binadamu kama ninyi? Japo ali mzaa Yesu kristo. Mimi hapo ndipo ninapo pataga ukakasi kwa sababu naonaga ni kama vile kumkosea heshima Mungu kwanini msimuombe Mungu mwenyewe, why Maria? Ninacho jua mimi Maria ni mwanamke aliye barikiwa kuliko wanawake wote basi na ndio maana alimzaa Yesu. naomba wanao jua zaidi waje wanikosoe hapa na kunielimisha zaidi kuhusu hili.
Nitakujibu kama hivi,Eeh Mungu niongoze.
Kwanza ieleweke wakatoliki hatumuabudu Maria bali tunamuheshimu,mtu asije akadanganya kwamba mama Maria anaabudiwa ndani ya Kanisa Catholic ieleweke haabudiwi.
Sala ya salamu Maria inasaliwa na waamini kama kumuomba yeye atufikishie kwa Mungu sala zetu na toba zetu kutokana na ule ukaribu aliokuwa nao na Mungu toka mwanzo Mungu alipomtuma malaika kumpa taarifa za yeye kuteuliwa kumzaa mkombozi kwa sababu tunaamini kwa dhambi zetu na madhaifu yetu hatujui kusali na kuomba kwa usahihi hata Mungu akatusikia.kwa wenzetu wapo watu wanaojikweza kwamba wanajua kusali sana hili kiimani siyo sahihi tumekatazwa kujikweza hakuna anayejua kuwasiliana na Mungu kisawa sawa sometimes mtu anaweza kujiona anasali kumbe anapiga makelele tu.
Kitendo cha Bikira Maria kubarikiwa na kupewa na Mungu uwezo wa kuileta Nafsi yake ya pili duniani moja kwa moja kinamfanya kuwa Mtakatifu na hata sasa Mama Maria yupo na Mungu so kiimani Catholics tunaamini lolote gumu akilibeba yeye anao uwezo wa kulifikisha kwenye kiti cha enzi na likasikilizwa.
Huu muunganiko unahitaji utulivu na neema kuuelewa na kuuamini.