Wauza magari wa bongo, wengi hawapaswi kuwa car dealers hawayajui magari kabisa

Wauza magari wa bongo, wengi hawapaswi kuwa car dealers hawayajui magari kabisa

Screen Shot 2026-08-19 at 10.54.12.png

Hawa jamaa wanayajua magari haswa...


Cc: Mahondaw
 
Kuna mtu kaposti gari namuuliza hii ina injini gani? Ananijibu huoni nimeandika injini cc 2000 boss 🤣🤣🤣.

Nikaona sio kesi nikamwelewehaa mfano toyota kuna 1GD kuna 1HZ na zinginezo. Sasa hii BMW unayouza ina engine gani N47 au B47. Hapo sasa akanivunja mbavu, akasema boss gari imenyooka injini kinanda ya kuwasha na kuondoka.

Wauza magari nendeni hata short course jamani ni aibu. Msiuze ili mpate hela ukikutana na mteja anaejua anataka nini ndio mnaaza kusema mteja mjuaji kumbe mmekwama kumuuzia takataka.

Anyway kama kuna dealer humu lazima ujue napokuuliza injini gani siulizi kwa sababu ya kuuliza tu. Hapana kuna engine zinajulikana pasua kichwa toka kiwandani.

Mnaweza wote mkawa na Subaru forester ila zikawa na injini tofauti kabisa.
biashara ya za kuuza kwa wabongo wengi hawana ujuzi sio tu kwenye magari hata electronics utasikia ina watt 3000 halafu jomba anachukua akijua kuna mziki wapi wewe .
 
biashara ya za kuuza kwa wabongo wengi hawana ujuzi sio tu kwenye magari hata electronics utasikia ina watt 3000 halafu jomba anachukua akijua kuna mziki wapi wewe .
Nilinunua soundbar kipindi nipo bongo naambiwa ina watts 1000 wakati mimi nimeiona amazon ina watts 225 tu, na hata offical site wameandika ina watts 225.
 
Tatizo watanzania tunajua vitu vingi sana hata havina msaada wowote katika Taifa linaloyajua magari na Engine zake ni Watanzania njoo sasa magari wanayotumia ni vituko vitupu..Zimbabwe wanamaliza hybrid car huko Japan na zinapita hapo hapo Daslm hizi wachache ndio wanaagiza wakizijua usumbufu utaanza kwa wauzaji wakati sio wanunuzi kabisa..
Mtanzania anajua Toyota Land Cruiser ya 2025 kwenye gari zao wameweka aina zipi za Engine ila kwenye kijiji anachokaa hakuna hata gari moja kama hiyo..
 
Back
Top Bottom