Wauza migahawa acheni upumbavu, hakuna chai bila majani ya chai.

Wewe ndio akili huna, unapoagiza kitu wewe ndio unapaswa kutowa order yako unataka nini.

Hotel nyingi za level ya kati vymbani wanaweka jagi la kuchemsha maji, tea bags na coffee pamoja na sukari.

Kama hivyo vyote huitaji ni wajibu wako kupiga simu restaurant au reception kuwaeleza choice yako.
 
Aisee watu mmejipata..yani mchana huu mnakunywa chai ya mapera
 
Acha kutetea upuuzi. Watu wa Dar ni wahamiaji.
 
Wewe una akili za kimama, hivyo vyote ulivyovitaja ni hiyari ya mtu.

Wanatumia sukari inawasaidia kupunguza gesi kwenye Maharagwe, na wanapaka ndimu na chumvi kwenye mahindi ni kuongeza ladha.

Labda huko kwenu mnakunywa supu bila limao na pilipili.
Wewe Dr feki acha kuandika upuuzi
 
Mkuu Yoda; Kama nimekusoma vizuri umesema waache Upumbvu. kUMBKUKA Mpumbavu ni kilema i.e. hafundishiki. Haiwezekani tena kumfundisha. Kumfundisha Mpumbavu ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu. Sasa ; mbona unajisumbua hivyo? Tafuta wale wauza migahawa abao ni Wajinga; hao ndo Uwape Ushauri/Uwafundishe.
 
Chai ni majani ya chai, hiyo 'herbal tea' nayo ni kitu tofauti ndio maana ikaongezewa neno 'herbal'. Kwani mtu akiagiza kahawa ataletewa viungo visivyokuwa na kahawa? Au ukiagiza ndizi za kupikwa unaletewa rojo ya nyanya, vitunguu hoho nk kwa kuwa vinatumika kuunga ndizi
 
Acha kutetea upuuzi. Watu wa Dar ni wahamiaji.
Hao wahamiaji wamejifunza kutoka kwa wenyeji,
mbona huko mikoani walikua hawafanyi hivyo?
When in Roma,do as the Romans do,

Yani unawaita watu wapuuzi kisa tu wana andaa vyakula vyao tofauti na wewe?
Ukienda nchi kama China si ndioutachanganyikiwa kabisa?
 
Rafikii umeanzaje siku yako leo? mbona umekasirika hivyo mpaka kupandisha uzi?🤣🤣🤣🤣🤣 hutaki koo liwashewshe shehe mimi ni napenda sana chai yenye viungo sana iwe ya maziwa hasa na vitumbua pembeni,chapati za kusukuma au za mayai,keki,kiporo cha wali maharagwe,sambusa,mihogo,kiazi kitamu nk huwa nikila hivyo buruduni sana
 
Unanibishia mimi?
 
Kitu hujui halafu bado unashupaza shingo, unajuwa maana ya herbal?

Kwahiyo Colgate herbal siyo Colgate?
 
Wewe una akili za kimama, hivyo vyote ulivyovitaja ni hiyari ya mtu.

Wanatumia sukari inawasaidia kupunguza gesi kwenye Maharagwe, na wanapaka ndimu na chumvi kwenye mahindi ni kuongeza ladha.
Duh! Mahindi yasiyo na ladha eti ni mpaka yaongezewe. Hayo ni mahindi Feki.
Huku kwetu hindi likichomwa nyumba ya jirani harufu yake hifichiki.
Halafu tena linaongezwa ndimu na chumvi! Kha sasa hilo ni mhindi au kachumbari?
Sipati picha eti maharagwe yanatiwa sukari! mwemwe, mweee. Hayo maharagwe yanaliwaje? ni mboga au ni Kitafunwa? Duh! Kazi kwelkwelii.
Huku kwetu maharagwe yanatiwa chumvi. Kama kuna mlwaji ansumbliwa na gesi kwa kula maharagwe huyo anaweza kupewa kipande cha ndizi iliyoiva au kwa uhakika anapewa magadi yale ya asili (emakat, mbala)alambe kidogo tu.
Labda huko kwenu mnakunywa supu bila limao na pilipili.
Oiyeyai! Supu huku kwetu au nyama-choma esp. minadani haiongezwi chochote. Ukitaka chumvi au pilipili unaomba upewe kivyako.
 
Umesema Neno stahiki la chai.(Tea) -ni sawasawa. Lakini kwa Waswahili na Wabongo kwa ujumla wetu, chochote kinachotumika asubuhi kama kifungua kinywa; imezoeleka kwa jina la "Chai" i.e. Breakfast. Kwa mantiki hiyo, neno chai kwa mapana yake mtu anaweza kumaanisha Mtori, Uji, Supu na wale jamaa zetu wa visungura. Kwa hiyo usimshangae mtu akasema nataka chai ya mchaichai au chai ya mashona-nguo n.k. Wewe umwelewe ivo-ivo tu. Lugha ya Kiswahili ina mapungufu mengi.
 
Hii kweli inawezekana ni tatizo la lugha, Waswahili wanafikiria kila kinachonywewa asubuhi ni chai tu.
 
Kwahiyo ni wajibu wangu kukufungulia Oxford dictionary au ni wajibu wako wewe ambaye hujui chai ni nini na bado unabisha?
 
Kwahiyo ni wajibu wangu kukufungulia Oxford dictionary au ni wajibu wako wewe ambaye hujui chai ni nini na bado unabisha?
Tea is an aromatic beverage prepared by infusion of hot or boiling fresh water with fresh or cured leaves of Camellia sinensis.
 
Kila kitu ulichoandika hapa umetumia usemi kwenu hivi kwenu vile kana kwamba kwenu ndio dunia nzima ilipo.

Sasa kama ulikuwa hujui hapa yanaongelewa Maharagwe ambayo asubuhi yanauzwa kama supu watu wanakula na chapati au maandazi na siyo maaharagwe mboga ya kula na ubwabwa hakuna anayeweka mboga sukari, ingawa mimi hata hayo maharagwe ya asubuhi siwezi kuweka sukari.

Kitu chochote kile kina ubunifu wake kila sehemu, wengine maeneo yao nyama ya mbuzi wanakula na kisusio wengine wanakula na kichuri, usikariri unachojuwa wewe tu ndio kila kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…