Wauza migahawa acheni upumbavu, hakuna chai bila majani ya chai.

Wauza migahawa acheni upumbavu, hakuna chai bila majani ya chai.

Kila kitu ulichoandika hapa umetumia usemi kwenu hivi kwenu vile kana kwamba kwenu ndio dunia nzima ilipo.

Sasa kama ulikuwa hujui hapa yanaongelewa Maharagwe ambayo asubuhi yanauzwa kama supu watu wanakula na chapati au maandazi na siyo maaharagwe mboga ya kula na ubwabwa hakuna anayeweka mboga sukari, ingawa mimi hata hayo maharagwe ya asubuhi siwezi kuweka sukari.

Kitu chochote kile kina ubunifu wake kila sehemu, wengine maeneo yao nyama ya mbuzi wanakula na kususio wengine wanakula na kichuri, usikariri unachojuwa wewe tu ndio kila kitu.
Kati ya ubunifu wa hovyo ni huo wa kuweka sukari kwenye maharage na tambi.
 
Umeelewa kilichoandikwa hapo?
Tea is a hot or cold aromatic drink made by steeping the processed or fresh leaves of the Camellia sinensis evergreen shrub in water.It is the second most consumed drink in the world after water.
 
Tea is an aromatic beverage prepared by infusion of hot or boiling fresh water with fresh or cured leaves of Camellia sinensis.
Tea is a drink made by steeping plant material in hot water.
In the strict botanical sense, “true tea” comes from the leaves and buds of the Camellia sinensis plant. This includes:
Black tea
Green tea
White tea
Oolong tea
Pu-erh tea
However, in everyday language, “tea” can also refer to herbal infusions made from other plants, such as ginger tea, mint tea, or hibiscus tea. These technically aren't true tea because they don't contain Camellia sinensis.
 
Sasa utakuwa umeelewa kuna chai OG na chai fake. Nategemea mgahawani ukisema unataka chai wazo la kwanza la muhudumu iwe ni chai halisi "true tea" na sio hizo mbwembwe nyingine.
 
Sasa utakuwa umeelewa kuna chai OG na chai fake. Nategemea mgahawani ukisema unataka chai wazo la kwanza la muhudumu iwe ni chai halisi "true tea" na sio hizo mbwembwe nyingine.
Unachopaswa kujiuliza kwa nini herbal tea ndio imepata mashabiki kuliko hiyo chai nyingine?

Waulize maduka ya Mangi pita migahawani ni chai gani inayouza?
 
Unachopaswa kujiuliza kwa nini herbal tea ndio imepata mashabiki kuliko hiyo chai nyingine?

Waulize maduka ya Mangi pita migahawani ni chai gani inayouza?
Sidhani kama herbal tea imepata mashabiki wengi, ninachojua wabongo wengi ni don't care, hata ukiwapa maji ya moto tu bila kitu ukawaambia ni chai watakunywa tu wakiona mwingine naye anakunywa.
 
Huwa napatwa na hasira sana nikiagiza chai halafu naletewa maji ya moto ya viungo sijui ya tangawizi, mdalasini, hiliki, lemon grass, majani ya mapera n.k ndio ninywe kama chai.

Chai lazima iwe na majani ya chai ( tea leaves-Camellia sinensis), hivyo vingine ni vikorombwezo tu na sio chai.
Ok
 
Kila sehemu kuna mapishi yake, kama unaona hujaridhishwa na upishi wa hapo unahamia kwenye mgahawa mwingine.
Pia unaweza ukaamua uwe unajipikia mwenyewe nyumbani kwa standards unazozitaka wewe.
Kama haina majani ya chai hiyo siyo chai hata uweke nini. Wangesema hawana Chai kuliko kusema wanauza Chai halafu wanawapa wateja vitu visivyoeleweka
 
Tunauziwa hadi chai ya nazi. I want my tea plain ,like once upon a time my parents were alive.
 
Mkuu chai ya Mgahawani unataka ulete amri iwe kama unavyoipenda wewe

Kila sehem kuna namna watu wanavyoishi na Utamaduni wao
 
Sidhani kama herbal tea imepata mashabiki wengi, ninachojua wabongo wengi ni don't care, hata ukiwapa maji ya moto tu bila kitu ukawaambia ni chai watakunywa tu wakiona mwingine naye anakunywa.
Wewe una msimamo wako ulioshiria lakini herbal tea ndio habari ya mjini kuanzia ladha mpaka manufaa ya kiafya.
 
Kila kitu ulichoandika hapa umetumia usemi kwenu hivi kwenu vile kana kwamba kwenu ndio dunia nzima ilipo.
Ni kweli. Nimetumia neno "huku kwetu" kumtanabahisha mleta mada kwamba kuna utofauti katika uelewa wa jambo na utofauti katika maeneo. Sio wote wasomaji wake wanaishi Dsm - tupo tunaoishi mikoani pia.
Sasa kama ulikuwa hujui hapa yanaongelewa Maharagwe ambayo asubuhi yanauzwa kama supu watu wanakula na chapati au maandazi na siyo maaharagwe mboga ya kula na ubwabwa hakuna anayeweka mboga sukari, ingawa mimi hata hayo maharagwe ya asubuhi siwezi kuweka sukari.
Ni Sahihi. Kila mbuyu na shatani wake au sio.
Kitu chochote kile kina ubunifu wake kila sehemu, wengine maeneo yao nyama ya mbuzi wanakula na kususio wengine wanakula na kichuri, usikariri unachojuwa wewe tu ndio kila kitu.
Nimekuelewa.
 
Kwahiyo ni wajibu wangu kukufungulia Oxford dictionary au ni wajibu wako wewe ambaye hujui chai ni nini na bado unabisha?
Mkuu; Siihitaji dictionary; naielewa chai kama kinywaji kinachochangamsha (Stimulate) kutokana na uwepo wa Caffeine ndani yake na mti wake unaoitwa Chai(Camellia sinensis) unastawishwa sana huko maeneo ya Mufindi, Njomb n.k. lakini nimeonesha pia kwamba kwa Lugha ya Waswahili; chai inaweza kuwa na maana zaidi ya hapo.
Sijakubishia ila nimepanua wigo. Nadhani nimejieleza.
 
Unachopaswa kujiuliza kwa nini herbal tea ndio imepata mashabiki kuliko hiyo chai
nyingine?
Herbal tea inapigiwa debe(promo) sana eti inasafisha damu, inatibu figo, inadhibiti presha na makorokoro kibao ambayo kisayansi hayajathibitishwa. Pamoja na hayo; hata hivyo haijapata mashabiki wengi ikilinganishwa na chai ya Majani ya chai Og.
Waulize maduka ya Mangi pita migahawani ni chai gani inayouza?
Chai ya rangi ambayo ndo hiyo huandaliwa kwa kutumia majani ya chai halisi yatokanayo na mti Camellia sinensis.
 
Wewe una msimamo wako ulioshiria lakini herbal tea ndio habari ya mjini kuanzia ladha mpaka manufaa ya kiafya.
Sio kweli. Hizo "Chai" za huko mjini; huku vijijini ambako ndiko kwenye watu wengi ; chai ni ile ya majani ya chai Og. Wanaweza kuweka vikorombwezo e.g. Iliki, pilipili manga, tangawizi, mdalasini lakini kimsingi lazima yawekwe majani ya chai(Tea leaves). Hata hii chai ya majani ya chai ina manufaa ya kiafya.
 
Upo karne ya ngapi mzee, mpaka leo unahangaika na majani ya chai?
 
Upo karne ya ngapi mzee, mpaka leo unahangaika na majani ya chai?
Oh! Kumbe tufanyeje? Hayo machai yenu eti ni ya kisasa cjui? iko siku mtakunywa majani ya Devil's Apple (Datura stromonium)eti ni herbal tea.
 
Back
Top Bottom