umemsahau Saigon alikujaga na msemo wa "ebana dahh!" na alikuwa na hitsong inaitwa "Rudia" alichukuliwa na EATV miaka mingi iliyopita baada ya kurudi kwa muda nchini Bongo kutoka Uingereza alipokuwa kwa ajili ya masomo akawa kwenye kipindi flani cha cha "Street Hip-Hop" baadae akaacha kazi akarudi Ulaya tena akawa hasikiki... mzee wake mmoja alikuwa serikalini ila baada ya kufariki jamaa akarudi Bongo akawa mtu wa Dini ile mbaya!
Sasa hivi ni bonge la Sheikh anatangaza Redio na TV Imaan ila washkaji zake kina balozi bado wapo intouch sana! Kuna siku moja nilikutana nae Sinza msikitini siku ya Eid akaniambia "Sometimes inabidi uachane na njia zisizo na kheir ufuate zenye kheir ingawa utapoteza watu wengi sana na channel za pesa za haraam ila ni bora zaidi kuwa kwenye kheir. Marafiki zangu hawajanisahau wala kunitupa Alhamdulillah naishi kwa support yao kwa kiasi kikubwa na anytime nikitaka kwenda Ulaya au Marekani kutembea nawacheki zinatumwa invitation naruka zangu ila muziki tena NO!... Maisha mafupi sana!"
Maneno mazito sana aliniambia ila hajaacha vituko na uchangamfu ila kiimani na kimuonekano kabadilika kwa kiasi kikubwa sana! [emoji1487]