Waweke hapa Wasanii wa Bongo Waliozaliwa / Kuishi Familia za Kishua

Waweke hapa Wasanii wa Bongo Waliozaliwa / Kuishi Familia za Kishua

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Wasanii wengi wametoka kwenye maisha magumu ya kuishi chumba kimoja familia nzima tena hapo wamepanga. Wengine wametoka mikoani wamekuja Dar hawana pa kulala wanalala stendi, mitaroni, Kariakoo shimoni au wakibahatika ndio ile wanaishi maisha ya ghetto chumba kimoja mtu sita, yaani kifupi wametaabika sana hadi kufika hapo walipo.

Licha ya hivyo kuna wasanii wachache ambao angalau wazazi / walezi wao walikuwa na nafasi ya kuwahudumia vizuri mfano kuwasomesha shule binafsi zenye ada kubwa, milo mitatu kwa siku ya uhakika a.k.a mboga saba, n.k. Yaani kifupi kwenye ukuaji wao hawajakumbana sana na suluba za maisha.

Vanessa Mdee
Baba yake alikuwa kwenye ubalozi Marekani, karudi Tanzania akiwa na miaka 12 anatema yai sio mchezo (aliwahi kuwa mtangazaji MTV), pia Kifaransa anaichapa vizuri tu.

Kukulia kwenye mazingira ya kidini kulimfanya kuwa msanii alejitahidi angalau kwenye nidhamu.

1639777005597.png


Makamua
Alisomeshwa Feza Boysys na St Mary's, ada ya Feza ni kama milioni 6.

1640101926598.png


Jux
Shule aliyosoma ni private ya gharama kimtindo, chuo kasomea nje ya nchi. Pesa ya studio + video ya wimbo wake wa kumtambulisha kweye game alilipiwa na mzazi wake, mama yake alikuwa anafanyia kazi bandarini.

1639775589966.png
 
Hicho ulichoandika kwa wanamuziki wengi wa Bongo sio kweli, yaani hali zao kiuchumi ni kawaida sana kwa mfano kua afisa wa ubalozi unakua wa kishua kivipi?
Tafsiri ya ushua ina mitazamo tofauti mkuu, kwako afisa ubalozi sio ushua kwa mwingine kupaka blu bendi kwenye mkate ni ushua tosha 😂
Labda tutafute consensus ya maana ya ushua alafu ndio tuendelee na mada
 
Back
Top Bottom