Wawili niliowabakisha kama marafiki nao nimewafuta!

Wawili niliowabakisha kama marafiki nao nimewafuta!

Mimi nina marafiki 3 na tunaweza tusiwasiliane hata miezi 6 na hatuwaziani tukiwa na shida tunatafutana tunaweka ushirikiano tunatatua zaidi ni kuangalia status,ku comment kwenye social network imeisha

Kwasababu mi huwa sina muda wa kumpigia mtu na kumsalimia nikikupigia simu tunaongea mishemishe sio salamu na ndugu na wazazi.wangu walishanizoea sipendi kuongea kwnye simu
dah we upo kama mimi. yaani mimi sina tabia ya kuwapigia watu cm. mpaka ndugu wanasema dah. ila mara moja moja sana ila wakipiga cm kama kuna changamoto natatua.

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Ukiachana na wale wa mbali kidogo kama washikaji ambao huibuka mara kadhaa pale tu wanapokuwa na shida, nilibakisha watu wawili ambao niliamini ni wa kweli ila sasa nimefikia hatua ya kuwafuta pia.

1. Huyu wa kwanza yeye huwa karibu sana pale anapokuwa na matatizo ya kifedha, atakuwa na mawasiliano ya mara kwa mara hata kuja nyumbani na vitu kama hivyo, uchumi ukikaa sawa anapotea na inafika wakati hata ukipiga simu mchana atakuja kutafuta usiku kabisa au atume tu text ya "Vipi kaka?" hapo imeisha.

2. Huyu wa pili yeye ana matatizo kwenye ndoa yake, huwa anavurugikiwa sana anapokuwa na changamoto za kimahusiano, basi huwa anakupigia simu hata mara 10 kwa siku mjadili na umsaidie mawazo jinsi ya kutatua matatizo yake. Mimi humpa full support lakini yeye nikijaribu kumueleza yangu kwanza anayadogolesha na hana muda wa kuyasikiliza, anakejeli pia.

Sasa nimeona msela wangu atakuwa mke wangu tu. Jambo ambalo sitaweza kuongea nalo nitabaki nalo mimi mwenyewe. Kwasasa mimi sina rafiki zaidi ya mke wangu.
Perfect
 
Ila Mkuu watu tunazaliwa na roho nyeupee nzuri....binadamu ndo wanatubadilisha.....wanajeruhi huwezi Amini ..watu ni wanafiki wa kutosha wabinafsi....hawataki upate hata mia.....Nimeona Kwa watu wa karibu sana aisee Cheka na watu ila usiwaamini
 
Rafiki anayekuomba hela huyo Mwambie ukweli kuwa ajitafakari Sana kuhusu MAISHA yake .

Usitengeneze urafiki wa kuomba hela kwa watu au Bali Kazi tu ukitaka kukupa kopa katika taasisi au mkope mtu ambaye amekuzidi kipato mara 20

Kiufupi mtu anayeomba hela anakua anahitaji kuvunja urafiki
 
Kuna muda na ww unawazingua..au una mirengo ya kihafidhina....hahhahahah
 
Ila wanasema kwamba rafiki wa kweli ni yule unayemwona kwenye kioo ukijitazama. Lil wayne ft bruno mars .Mirror on the world. Pia G Eazy ft bebe rexha .Me myself and I.
 
Mimi nina marafiki 3 na tunaweza tusiwasiliane hata miezi 6 na hatuwaziani tukiwa na shida tunatafutana tunaweka ushirikiano tunatatua zaidi ni kuangalia status,ku comment kwenye social network imeisha

Kwasababu mi huwa sina muda wa kumpigia mtu na kumsalimia nikikupigia simu tunaongea mishemishe sio salamu na ndugu na wazazi.wangu walishanizoea sipendi kuongea kwnye simu
Wewe ni mimi kabisa. Yaani mimi nilishashidwa hii hali ya kupigiana simu mara kwa mara na kuchat. Tutaonana kwenye changamoto na mambo muhimu yanayotaka ushirikiano.
 
Nshafanyaga hardrest ya circle yangu ya karibu sema kuna kichaa moja anatukio lake personal alilifanya kona ya kuingia mlimani city ukitokea mawasili kuna mama alikua anaendesha pickup manual anatokea mawasiliano anaingia mlimani city sisi tuko nyuma yake sasa bi mkubwa kaweka reverse gear bila kujua kakanyaga mafuta gari ikawa inatufata jamaa alifungu mlango katoka anaenda kuzuia gari kwa kuisukuma was funy bt stupid kuna watu ukifanya hardreset lazima utawarudisha wengine hawana msaada ila kwaajili ujinga ujinga tu ila maisha yangu coz kuna muda hutakiwi kua serious sana just have funy
 
......Sasa nimeona msela wangu atakuwa mke wangu tu. Jambo ambalo sitaweza kuongea nalo nitabaki nalo mimi mwenyewe. Kwasasa mimi sina rafiki zaidi ya mke wangu.
HAhahaha
Say it again
 
Back
Top Bottom