Pole! Jitahidi kuishi nao kwa akili sana namaanisha sana.
Kwani kuona marafiki ni tatizo ni kosa lako la kutojua maana ya urafiki. Wengi hutaka wanachowafanyia marafiki nao wawafanyie, jambo hilo hupelekea magomvi makubwa na ni kitu ambacho hakiwezekani.
Kumbuka urafiki huunganishwa na jambo moja, mfano, urafiki wenu unaweza kuunganishwa na kufanya kazi au tabia inayofanana kama biashara, kilimo, wezi, kuvuta bangi n.k.
Igawa mambo mengine havitafanana kabisa, Mfano
1. Wewe unapenda kupiga simu lakini rafiki yako yeye anapenda kutuma sms.
2. Wewe usipopigiwa simu unaumia lakini mwingine umpigie usimpigie wala siyo tatizo.
................................
Kwa kifupi usiwekeze muda wako mwingi kwa marafiki.