Kaka tafadhali utumie ubongo kidogo. Kati ya wanasanyansi bora duniani waliopokea Tuzo ya Nobel takriban asilimia 20 ni Wayahudi, ingawa Wayahudi wenyewe ni kundi ndogo , si asilimia 1 ya binadamu wote.
Ukifika hospitali na kupata tiba nzuri, ni shauri ya kazi ya wataalamu wengi pamoja na hao Wayahudi.
Machoni pangu mtaalamu anayefanya utafiti kwa manufaa ya watu wote anajitolea akichangia jambo muhimu kwa binadamu wote.
Asilimia 20 ni Wayahudi 8ilhali Wayahudi wote ni kama milioni 15 pekee duniani kati ya bilioni 7.
Wayahudi wanasisitiza elimu kwa watoto wao, kushinda jumuiya nyingi za dunia. Kama wote wangeisisitiza vile, tungekuwa mbele zaidi. Zao moja ya juhudi hiyo ni idadi kubwa ya wataalamu wanaopokea Tuzo ya Nobel kwa kazi bora ya kisayansi.
Ukipenda kuwajua kwa undnai zaidi, tafuta habari za hao wanaNobel Wayahudi waliopokea Tuzo ya Nobel ya Tiba:
Élie Metchnikoff, Robert Bárány, Otto Fritz Meyerhof, Karl Landsteiner, Otto Heinrich Warburg, Otto Loewi, Joseph Erlanger, Ernst Boris Chain, Hermann Joseph Muller, Gerty Cori, Tadeusz Reichstein, Selman Waksman, Hans Adolf Krebs, Joshua Led