Kwa bahati unajadiliana na mtu ambaye sio kama yule Laila ila ....
Umesema tuache habari za tuzo za Nobel na haikuwezekana tumerudi kule kule. Na mimi nililposema
Nobel Nyengine zinatlewa kirushwa na hata kwa wapumbavu sikubainisha kuwa ni zile za kisayansi au za nyanja nyengine kama za akina Obama. Kama umepata picha kuwa hizo zawadi za Nobel si jambo kubwa katika dunia na zinaweza kutolewa kwa malengo kama nilivyosema hapo juu. Sasa usishikilie kuwa hizo Nobel za wanasayansi kama ni wa kiyahudi au wengineo ndizo safi na tukufu sana. Mimi hizi nazo pia hazinishtui.Najua wengi wanaopewa hawastahiki kupewa sifa na kutukuzwa mpaka tukamsahau Mwenyezi Mungu.
Aliyepewa zawadi ya Nobel atakuwaje mtu wa maana iwapo katika hicho alichokiona hakumtaja Mungu hata nukta moja kama kwamba yeye ndiye aliyekiumba.
Nani katika binadamu atakayejichukulia sifa kwa kujua namna electron na chembechembe nyingi zisizoonekanaa zinavyojipanga na kupita maeneo yasiyoonekana na kusababisha mabadiliko yanayowafaa watu na bila kumtaja Mwenyezi Mungu. Hicho alichokiona Einstein mbinguni alichangia nini kukipa mpangilio na athari zake.Wavumbuzi wa namna hii ndio binadamu wanawapa sifa na wako wanaowadharau waislamu eti hawaoni vitu kama hivyo na kujaribu kutoa picha kuwa ni milki ya wayahudi na wakristo,
Waislamu wavumbuzi wakubwa hawapati zawadi kama hizo ilhali wao wangepaswa sifa hizo kwa haki kabisa kwa vile wakivumbua huwa wanamtaja Mwenyezi Mungu katika uvumbuzi huo.