Wazabuni wa Taasisi za Serikali tunapata tabu sana kulipwa madai yetu

Wazabuni wa Taasisi za Serikali tunapata tabu sana kulipwa madai yetu

jojipoji koromije

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2017
Posts
1,127
Reaction score
1,635
Hivi najiuliza hawa viongozi wa taasisi za umma wanaotoaga order za mahitaji kwa wazabuni, wanadhani wazabuni wana visima vya pesa.

Hawajali kabisa kulipa kwa wakati!! Nakumbuka Magufuli aliwahi kuwaambia hizi taasisi za umma kama huna hela usiagize bidhaa kwa mzabuni, ila sasahivi Jamaa kama wanatukomoa!! Labda niulize wazabuni wengine hizi changamoto za kucheleweshewa malipo mnashughulika nazo vp??

Maana marejesho yatatuoa roho. Majibu yao Jamaa ni rahisi tu, wanakwambia hawajapata hela!! Sasa mliagiza bidhaa ili iweje? Kwa kweli hizi taasisi ndo zinafilisi wazabuni.

Huwezi kupiga hatua kwa biashara ya namna hii ambayo mtu anakulipa kadri anavyojisikia. Basi wafanye biashara na SUMA JKT sisi raia waseme kabisa haturuhusiwi.

Ina kera sana 😬😬😬
 
Hivi najiuliza hawa viongozi wa taasisi za umma wanaotoaga order za mahitaji kwa wazabuni, wanadhani wazabuni wana visima vya pesa. Hawajali kabisa kulipa kwa wakati!! Nakumbuka Magufuli aliwahi kuwaambia hizi taasisi za umma kama huna hela usiagize bidhaa kwa mzabuni, ila sasahivi Jamaa kama wanatukomoa!! Labda niulize wazabuni wengine hizi changamoto za kucheleweshewa malipo mnashughulika nazo vp?? Maana marejesho yatatuoa roho. Majibu yao Jamaa ni rahisi tu, wanakwambia hawajapata hela!! Sasa mliagiza bidhaa ili iweje? Kwa kweli hizi taasisi ndo zinafilisi wazabuni. Huwezi kupiga hatua kwa biashara ya namna hii ambayo mtu anakulipa kadri anavyojisikia. Basi wafanye biashara na SUMA JKT sisi raia waseme kabisa haturuhusiwi. Ina kera sana.
😬😬😬
20250511_182058.jpg
Huyu Mzee Hadi alipiga ngolo lakini wapi?
 
Ukiwa mzabuni na una mtaji wa kuunga unga unaweza kuyumba sana ama kufilisika kabisa ! Mfumo wa malipo na marejeleo unachukua mda sana, sasa ukute ulijichanganya ukaenda kukopa Bank, hakuna rangi utaacha kuona ! Japo utakuja kulipwa late
 
Back
Top Bottom