Wazabuni wa Taasisi za Serikali tunapata tabu sana kulipwa madai yetu

Dah Kuna mzee mmoja mtaani kwetu amefikisika Kwa mambo hayahaya,jamaa alikuwa na hardware kubwa tu Kwa level za wilayani,Sasa hizi shule za serikali hizi zikaanza jengwa na jamaa akawa mzabuni wa materials zote isipokuwa tofali tu na mafundi,ebhana eeh,huu ni mwaka wa7 hivi saiz mzee wa watu ni machinga,mtaji haufiki hata laki5,wazee haya mambo yapo msichukulie poa,usijethubutu kuikopesha serikali
 
Mnapenda kudhulumika,serikali ya Tanzania kila mtu tapeli,Kuna mzee kafariki mwaka 2023,chanzo Cha kifo msongo wa mawazo,presha. Nyumba imeuzwa na Bank,kisa??Wana duka la spare za magari kubwa tu,siku zote wanafanya kazi na tamesa,..mara ya mwisho anawadai Milion 150,vikaanza vipengere karibu miaka mitatu hadi mzee kafariki... RIP Shirima.

Mke wake now ana duka dogo hata Milion 10 halifiki
 
Tena sku izi wanakitu inaitwa nest wao hawataki kuibiwa ila ukisuppy tu kulipwa ndo msala

Sa sjui iyo nest imewekwa kumsaidia nani maana wazabuni tunaumia na wao kutoa malipo ni kazi

Nest watu tunaomba na tunashindanishwa mtandao hii inasababisha wafanya biashara tunaweka bei ndogo ili tushinde tenda zeni mwisho wa sku umesaply af malipo yanakaa miezi
Zaman zile cotatio turikua tunaongeza bei kidogo tunaamini ata malipo yakichelewa nmeongeza bei bas ita cover ila saiv ni hasara.

Nimeanza kuona tenda zinatangazwa adi mara 3 na watu hawa apply sabu hawaoni faida yake zaidi ya hasara na tunakoelekea nest itaferi au serikal itapata tabu sana kupata ma sapplya
 
Mimi nko Arusha imetokea kuna ujenzi wa shule tenda inawekwa nest maana yake mimi mfanyabiashara wa arusha inabidi nipambane na wafanyabiashara wengne toka dar na mikoa mingne ya jiran,

Sasa inakubidi uweke bei ndogo sana ili hiyo tenda isiende kwa wafanyabiashara wa dar afu mwisho wa sku unashinda tena unasapply malipo yanachelewa wanakulipa wanavyo taka

Kutia tu signature kwenye cheque mtu alipwe utaambiwa mara mkurugenzi yuko dodoma vikao mara mkurugenzi au DC wako kwenye ziara unakaa miezi hujalipwa
 
Nafkri mkiungana mka dai kwa pamoja mtalipwa
 
Pole sana,mimi niliachaga zamani,na sasa ni vizuri kushiriki agenda ya NO REFORMS NO ELECTION
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…