Wazaliwa wa mkoa wa Tanga tukutane hapa

Wazaliwa wa mkoa wa Tanga tukutane hapa

KOROGWE BUS STAND
IMG_2388.JPG
 
Ni muda muafaka sasa wa viwanda vyote vya Tanga vianze kufanya kazi maana ni mji ambao ulikuwa unaongoza kwa kuwa na viwanda vingi sema sasa vimekufa vingi. Fursa nyingi za ajira zitatolewa kupitia mradi wa Chongoleani vijana ambao mpo Tanga msikubari fursa hii ikawapita.
 
Eti watu wa Tanga nao wanawaita Watu wa Mikoani ,,wa kutoka Bara", hili lilinishangaza sana, nilifikiri ni msemo wa watu wa Dar tu!
Hata Morogoro wanawaita hivyohivyo watu kutoka mikoa mingine wakiwatofautisha na watu wanaotoka Morogoro na mikoa ya pwani
 
Tuliooa dada zenu haturuhusiwi kupitia humu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ruksa. Kama mmeoa dada zetu basi nyie ni walowezi au walowezi watarajiwa wa Tanga.

Usipite tu bali weka maskani humu jamvini. Tuulize yale unayoshindwa kumuuliza mkeo. Bali kuna ushuru wake. Shemeji lazima anunuliwe chupa kadhaa za mnazi au boha na supu ya makongoro.

Baada ya hapo tutakuonyesha mizungu yote pamoja na namna ya kuvifanya vufuu vya nazi vitembee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom