pamoja na yote yanayojiri, ikiwa ni pamoja na kutetea kwa hoja umuhim wa muungano, uwepo wa serikali mbili au 3, hadi kufikia malumbano makubwa katika bunge la katiba na hata mitaani
tuongee ukweli kabisa bila kubabaisha maneno kwa kujiuliza mbona bara tunaonekana kuutaka sana mungano ukilinganisha na wazanzibari?imefikia kiasi cha kuugaramia kwa mapesa mengi, inasemekana wazanzibar wamekuwa wakitegea kulipia garama za muungano lakini bara tunalipia tu tena bila kinyongo
hilo dogo, kubwa ni hili hapa, miaka ya 1980s kuzungumzia habari za muungano ilikuwa sawa na kuweka reheni kibarua chako kama ilivowatokea akina abou jumbe, si hivo tu kuweka rehani kibarua bali pia hata hatari ya kupoteza uhai kisa tu, umehoji swala la muungano, speech alio itoa tundu lissu,bungeni kuhusu muungano asingesubutu miaka ya sabini na themanini, sasa jiulize jambo gani jema liendeshwe on that way
siku ya muungano, naona katika picha palichanganywa mchanga wa bara na visiwani, na inasemekana (sijui kweli) eti ule mchanga ulienda mwagwa baharini, sijui kama kweli na kama ni kweli kulikuwa na sababu gani?
kama kweli zile ni hati sahihi za muungano, ukitaka kuona kihoja tuombe na nakala iliyopelekwa UNO nauhakika zitakuwa tofauti kabisa, maana kama hii iliyoletwa inakasoro hasa katika sahihi ya karume, swali la kujiuliza kama muungano ni very crucial na una muhimu na faida pande zote iweje bara tuonekane ndio tunaojua zaid kuliko hao zanziba?sikatai kuwa kuna wazanzibar wanotaka muungano,ki ukweli wapo lakini tunaangalia wimbi kubwa.
tusidanganyane muungano unajambo, jambo lenyewe hatulijua, wapo wnao lijua akina government officials, ni mtazamo tu jamani