Wazanzibar kuongoza Wizara/Taasisi zisizo za Muungano imekaaje kisheria?

Aisee,
Mkuu hivi ndo ilivyokaa ama umeamua wewe?
Mambo ambayo siyo ya Muungano ni mambo yanayohusu Tanganyika japo yatakuwa chini ya Rais wa muungano na hayahusu Zanzibar. Inakuwaje Mzanzibar ni Mtanzania lakini Manganyika si Mtanzania wakat Zanzibar ni sehemu ya Tanzania.
 
Mkuu kwani hujui kuwa 1+1=2
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Tatizo zaidi ni uwezo wao kushinda uzanzibari.

Huyo naibu wizara ya afya anaedili na mambo ya jamii inabidi aangalie activities za hizi asasi za jamii.

Swala la ulinzi wa watoto ni sensitive na hiyo ni vita ya serikali kwenye preventive measures na inataka ushiriki wa polisi, ustawi wa jamii na kujua unawapeleka wapi wahanga wa abuse kabla ujaingilia kati.

Sasa hizi taasisi zinazoanzisha vilabu na kuita kuzungumza na jamii waelezee changamoto za abuse zao; halafu baada ya mtu kumchongea abuser wake anarudi kuishi kwenye nyumba ile ile bila ya polisi involvement au ustawi wa jamii kumchukua kama ni mtoto.

Mjomba hizo taasisi wanawatengenezea hao watu mazingira magumu ya kuishi kuliko waliyokuwa nayo awali.

Vitu vingine sio kukurupuka na kudandia kama huna elimu navyo. Waziri inabidi aangalie hizi taasisi zinaweza kuwa na nia njema, ila intervention za social services ni technical sio mambo ya kukurupuka bila ya kujipanga.
 
Makubwa, mkuu maana nyingine wazanzibar wamenyonga Watanganyika , wao ndo wanafaidi Sana muungano kuliko Watanganyika , alafu wanapenda kulalamika , ili kutupumbaza Watanganyika
 
Mkuu Gagi, hili liko straight forward wala halihitaji tafsiri yoyote ya kisheria. Muungano wetu ni muungano very unique. Kwa upande mmoja, kitaifa na kimataifa, muungano wetu ni union, hivyo Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye rais mmoja, rais wa JMT, uraia mmoja tuu, uraia wa JMT, na raia wote wa JMT wana haki sawa. Lakini ndani ya muungano, muungano wetu ni federation, wenye nchi mbili, marais wawili na uraia wa aina mbili. Raia wa JMT na Ukaazi wa Zanzibar. Wazanzibari wote ni Watanzania na haki zote za uraia, ikiwemo kuajiriwa kuteuliwa kuongoza taasisi yoyote. Ila kwa upande wa Zanzibar, wenye haki ya kuajiriwa ni Wazanzibari wakaazi pekee.
P
 
Hatujipendekezi bali muungano ni kama ndoa, japo baba ndio kichwa cha nyumba, mke wako ndiye mtawala wa jikoni, na chumbani, japo mahari umelipia mwenyewe, na kuoa, umeoa wewe, lakini unapotaka zile huduma, lazima uombe, na ukubaliwe atakapojisikia yeye, na unaweza kunyimwa na magoti ukapiga.

Zanzibar ni sehemu ya JMT yenye haki zote za uraia wa JMT.
P
 
Kila Mzanzibari ni Mtanzania, ana haki zote za uraia wa Tanzania kama Mtanzania mwingine yeyote, ila kwa upande wa Zanzibar, haki hiyo ni kwa Wazanzibari wakaazi pekee.
P
 
Waliapa kwa Vitabu vya Dini katiba ya Muungano kwa kuifuata na kuitekeleza so kama wanaivunja hukumu yao ipo ni vizuri kuwakumbusha kama ni wacha Mungu au Wanaomcha Maulana
 
Wewe kuna thread ya Mtu kasema Raisi afuate Sheria ukasema unamuunga mkono and then unaongea nini hapa ebo!
 
Kila Mzanzibari ni Mtanzania, ana haki zote za uraia wa Tanzania kama Mtanzania mwingine yeyote, ila kwa upande wa Zanzibar, haki hiyo ni kwa Wazanzibari wakaazi pekee.
P
Nimejikuta nikicheka Kama kichaa, Yani kwa lugha nyepesi TANGANYIKA ni koloni la Zanzibar ndani ya Muungano , wao kila pembe ya nchi Katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ruksa, ila Mtanganyika Zanzibar tumewekewa vitanzi , unaingia Zanzibar Kama vile unaenda USA,

Zanzibar tupeni Tanganyika yetu, vinginevyo twende sawa kwenye Muungano,
 

..Rais Samia Suluhu ndiye waziri wa Tamisemi.

..Je, suluhisho ni kuundwa kwa serikali ya Tanganyika?
 
Nini mantiki ya kuweka kwenye katiba yale mambo 22 ya muungano?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…