Wazanzibar kuongoza Wizara/Taasisi zisizo za Muungano imekaaje kisheria?

Sheria ya uzanzibari ukaazi imetungwa lini?
Naamini kipindi cha mwalimu haikuwepo
 
Binadamu tumeumbwa unique tofauti na wanyama wengine. Tutumie hata common sense Basi. Mzanzibar anaweza kuwa raisi wa Tanzania ambaye anaongoza , wizara zote, mikoa na wilaya. Inakuaje ashindwe kuteuliwa nafasi ya dc au rc? Wakati cheo Hiko Ni kidogo zaidi juu ya nafasi ya uraisi.
 
Katiba mpya, narudia tena katiba mpya.

Zanzibar kuna wizara ya fedha. Masauni anakuwaje tena huku kama waziri wa fedha?

Iko fyongo kwa wizara iliyoko Zanzibar kuwa na waziri au waajiriwa katika wizara ya kufanana huku.

Jipu hili laelekea kubaya.
Mwalimu Nyerere na Karume walikuwa na lengo zuri tu walipounda huu muungano. Shida ilikuja kwa waliopokea kijiti. Viongozi wa Zanzibar wakaanza ubinafsi wa kuilinda Zanzibar yao na viongozi wa Tanganyika wakaanza kuvuna Mali za nchi ili wawe matajiri.
Wote wakasahau lengo la Muungano sasa kilichobaki sijui ni nini?
 
Zanzibar nayo ni Tanzania kumbuka. Kwanini "uzanzibari ukaazi" na sio "utanganyika ukaazi"
 

Hapa kimebaki katiba mpya ya kuyaweka mambo sawa.

Mezani hakuwahi kuharibika jambo.
 
1972 Mwl Nyerere alimchagua Ally Hassan Mwinyi kuwa Waziri wa Afya japo Wizara hiyo haikuwa sehenu ya Mambo ya Muungano

Mwaka 2000 Mzee Benjamin Mkapa alimteua Hussein Ally Hassan Mwinyi kuwa Naibu Waziri wa Afya

Hata Mwana dada Engineer sikumbuki jina lake ambae kwa sasa ndio Katibu Mkuu Kiongozi Znz aliteuliwa na Hayati Dr Magufuli kuwa RAS wa Tanga japo Tamisemi sio sehemu ya Mambo ya Muungano

Kila Mzanzibar ni Mtanzania lakin sio Kila Mtanzania ni Mzanzibar

Hata Hussein Mwinyi alishakuwa Mbunge wa Mkuranga
 
Ndio unastuka leo? Hii nchi inakaribia kuwa ya Wazanzibari pekee na kusilimishwa.

Wabikkah Tawfiq,
 
Ni either tuwe na serikali moja au tuwe na serikali tatu. Hiki kilichopo sasa hivi ni uhuni.
Serikali tatu ni mzigo ,kutaongezea gharama bure kwa ajili ya faida ya wachache, hao wote watajipangia kujengewa mihekalu ya kufa mtu, watajipangia mibenzi, kifupi muungano usiwepo kila mtu achukue 50 zake. Ukisema serikali moja jamaa zetu wabishi watasema watamezwa , wao wanaona kama bara ndio tunawahitaji zaidi kuliko wao wanavyotuhitaji. Pia mimi naona zile sababu za kuwepo muungano kwa wakti huu hazina mshiko, mambo ya vita baridi kati ya nchi za Magharibi na Mashariki hayapo, hatuihitaji Zanzibar kwa ajili ya usalama wa bara!
 
Safari hii ni watanganyika ndiyo mtataka muungano uvunjike tofauti na hapo awali.
Hao Watanganyika ndio kina nani,sisi ni Wanzania tuliopo bara kuanzia tarehe 26 April 1964 ambapo Tanganyika iliishia hapo zaidi ya hapo ni lugha ya kibaguzi.
 
Maajabu ukienda Mtanganyika ukitafuta kazi za serikalini hawakubali ila Wazanzibar kibao wako kwenye taasisi mbali mbali za serikali. Nashindwa kuelewa hapo hizi ni nchi mbili tofauti au ni Jamhuri ya Wadanganyika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo tunajua anaweza. Tatizo wewe unaonaje , imekaa sawa hiyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…