Tetesi: Wazanzibari wengi wanautweza Utanzania, shida ipo wapi?

Hakuna shida wanatukuza Taifa lao.
 
Umenena
 
Wajitoe tuu, na Tanganyika nayo itabaki huru bila uwepo wao! au kuna maslahi kwako kwa uwepo wao?
 
Siyo kweli, mimi naamini kwamba wao wameamua kuusimamia unzanzibar wao kama ambavyo the late Rev Mtikila siku zote alijinasibu yeye ni Mtanganyika. Pia hili ni wake up call kwamba huu Muungano bado kero zake zinawakwaza.
 
Bepari mkubwa wewe unajua maana ya Zenj wewe.unajua Ibn Bathuta alipotoka Oman kuja kuzuga huku alikuta watu gani. Ndo maana nikasema shule shule shule shule nibmuhimu. Muoman kuja kuvamia na kuacha vinasaba vya kutafuta Kwa darubini Kali hakukupi uhalali wa kujinasibu kuwa ni ndugu na umkabidhi kila kitu akili ya kitumwa inakusumbua
 
Kumbe wa Znz wengi NI Wana asili ya bara...nilibahatika kumsikia msanii mmoja wa taarabu toka Znz alisema mama yake ana asili ya usukuma na anaongea kisukuma pia baba yake ana asili ya kilwa ....
 
Walifikaje Zanzibar hao watu unaowataja? Nimeshakupa somo kwamba hawakuwepo wakati wa visiwa vinamegeka miaka milioni iliyopita. Sasa walivukaje bahari mpaka Zanzibar?
 
Wewe mayala ni mtanganyika kwanza kabla ya kuwa mtanzania!! Utanzania unapata uhalali wake kugoka kwa utanganyika na uzanzibari!! bila utanganyika hakuna utanzania!!!!
 
Muscat ilipo inatosha siyo lazima ilingane na Dubai.
Basi Zanzibar ilipo inatosha siyo lazima ilingane na Muscat/Oman.
BTW, hujanielewa mantiki ya mfano au swali langu.
Nilitaka kukuonesha hata kama Zanzibar ingepata uhuru hadi leo siyo lazima ingepata maendeleo kiwango cha Oman alikotoka sultan aliyetawala Zanzibar.
 
Labda urudie kusoma huu uzi wote ndiyo ungenielewa. Pointi yangu ni kuwa Zanzibar ingejiunga na Oman badala ya nchi fukara iliyokuwa inaitwa Tanganyika, Zanzibar leo ingekuwa kama Muscat. Utajiri wa mafuta walioupata Oman ungenufaisha na Zanzibar pia kama ingekuwa ni sehemu ya Oman. UAE na Oman hawajaungana kwa hiyo sitegemei Muscat kuwa kama Dubai. Ni vitu tofauti na Zanzibar kuungana na Oman.
 
Kuna nchi ndogo ndogo vingine visiwa kama vya Zanzibar ambavyo vimeungana ua vipo chini ya France vingine chini ya UK lakini havina maendeleo kama France au UK.
That's my point...
 
Kuna nchi ndogo ndogo vingine visiwa kama vya Zanzibar ambavyo vimeungana ua vipo chini ya France vingine chini ya UK lakini havina maendeleo kama France au UK.
That's my point...
Tofautisha makoloni na nchi zilizoungana. Visiwa vya Hawaii vimeungana na Marekani, vina maendeleo kama sehemu zingine za Marekani. Makoloni huwezi kulinganisha kimaendeleo na nchi zinazoyatawala. Zanzibar ingeungana na Oman kama kihistoria ndiyo ingenufaika na maendeleo ya Oman.
 
Ha ha haaa...
Naona unafunika kichwa kwenye mchanga ukijifariji kila kitu kipo sawa kama udhaniavyo.

Zanzibar haijawahi kuwa koloni la Oman Sultanate?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…