Samcezar
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 13,095
- 22,731
So unaishi kisela na mkeo na watoto. Wageni wakija mnaishi nao vipi?!Humu kuna wachangiaji wengi ni kula kulala tena wengine wanaishi kwa shemeji zao hamna walijuwalo.
Kwa mfano mimi binafsi hawa tunaowaita wadada wa kazi wamenisumbuwa sana achilia mbali kuwabadirisha au anakuja huyu anakaa wiki anataka kuondoka kumbe ulitumioa tu kumleta mjini na saa nyingine unatuma nauli unaliwa vilevile, sasa nimeamuwa hivi.
Watoto wakubwa wako boarding, mtoto mdogo yupo day lakini anashinda shuleni anarudi jioni kabisa kwahiyo nyumbani tunapika usiku tu au nanunuwa take away hakuna kupika.
Sihitaji wala sifikilii kuleta house girl, usafi ni mara moja kwa wiki anakuja dada anafuwa anaosha vyombo anapiga deki nyumba namlipa cash yake anatambaa, siku za kawaida kufagia nyumba hakunishindi nafagia mimi au wife yeyote atakayehisi kuna michanga ndani.
Kwahiyo kwangu wala hatuhitaji mpishi na wakubwa wakirudi likizo wanapika wenyewe mchana au mama yao kabla ya kwenda job akiamka mapema awapikie ubwabwa full suti, binafsi kama nakuwa home vyakula vyangu ni michemsho tu wala havina mambo mengi ni nyama au samaki viazi ndizi na viungo unachanganya pamoja unakadiria maji, unaweka chumvi unatia na mafuta machache unawasha gesi ngoma inajipika yenyewe, hivi hapo shida iko wapi? Ukiona mimi nanunuwa chips ujuwe ni dharura tena ni usiku inanibidu tu.
Sent using Jamii Forums mobile app