Wazazi acheni uhuni na visingizio, toeni urithi kwa watoto. Elimu sio urithi!

Wazazi acheni uhuni na visingizio, toeni urithi kwa watoto. Elimu sio urithi!

Wazazi wa siku hizi akifikisha 45/50 mwanaye 25-30 hapo Baba miguu juu kila kitu kwa mwanaye, hujasikia kina Baba wanawambia watoto wao wakiume waoe wanawake wenye kazi ili wasaidiane hapo wanapiga hesabu ili matumizi yasipungue kwao.
[emoji23] [emoji23] hii kali
 
Umeongea ukweli mtupu ,kwa life ili lilivyo ni muhimu sana kwa mzazi kumuandalia urithi mwanae ,just imagine kama wazazi wetu wangetuandalia viwanja enzi hizo ina maana kwasasa tusingepanda shida ya kupoteza fedha kwa ajili ya kununua viwanja,hii inawezekana kwasasa ukanunua shamba huko nje ya mji baada ya miaka 25 unamkabidhi mwanao means patakuwa town.

Ukimfungulia hisa kwenye stable company au ukawa na plan ya kumuwekea amount flan kila mwezi kwa muda wa miaka 10 ijayo itakuwa na mpunga mwingi.

kumjenga kibizness zaidi hasa kulima mboga mboga ,kufuga kuku ,kuuza duka etc hata akifikisha 18 anakua na upeo wa biashara,huo ndiyo urithi ,mambo ya elimu ni JAU.
 
Kila mtoto amjengee ya kwake. Wewe ndo huelewi. Mzazi kurithisha wanae urithi ni jukumu la kiungu kwani ndo maagizo ya Mungu. Muwe mnaekewa.
Unaonekana mhaya lakini mawazo ya kichagga! Urithi umewafikisha kwenye vihamba vyenye Mashiba ya migomba matano. Ni umaskini tu! Tafuta vyako vya baba yako ni vyake vimtunze hadi afe. Akivigawa is utamtunza wewe?
Unafikiri watu kama Mo na Manji ni mataji kwa bahati?
Mawazo ya kitoto
 
Hapa twaongelea continuity ya mali, ukiwa na mali lazima muangalizi awepo mapema ili zisipotee.
Ni wangapi wana mali wewe, wote umaskini tu! Njaa ndiyo inawafanya muwe na akili za kitoto ati urithi
 
WAZAZI ACHENI UHUNI NA VISINGIZIO VYA KIPUUZI. TOENI URITHI KWA WATOTO. ELIMU SIO URITHI

Anaandika Robert Heriel.
Yule shahidi kutoka Nyota ya Tibeli.

Andiko hili laweza waumiza wengi. Ikiwa unajihisi unamoyo dhaifu nakusihi usisome. Na ikiwa utasoma basi nisihusike na maumivu na madhara yatakayojitokeza nafsini mwako.

Niite Taikon wa Fasihi, Kuhani katika Hekalu jeusi.

Baba anamajukumu makuu matatu ndani ya familia, nayo ni;
1. Kuhakikisha ulinzi na usalama ndani ya familia(mke na watoto wake)
2. Kuihudumia familia( mke na watoto wake)
3. Kuzalisha Mali na kuandaa Urithi Kwa kizazi chake.

Hivyo Sisi Vijana tunapaswa tutambue mambo hayo matatu, mambo hayo hayana excuse nilazima yafanyike ili heshima ya Baba ilindwe.
Kabla hujaoa na kuzaa watoto lazima ujiulize, je unauwezo wa kumlinda na kumfanya Mkeo na watoto wawe salama?
Pili, unauwezo wankuwahudumia mke na watoto? Mwisho je mipango yako na uwezo wako ukoje katika kuzalisha na kuandaa Mali za Urithi Kwa watoto wako kulingana na nyakati na Zama watoto wako watakazoishi?

Siku za hivi karibuni kumezuka uhuni Fulani hivi Kwa wazazi hasa wababa kuleta visingizio vya kitoto kuhusiana na masuala ya kumuandaa mtoto na ulimwengu.

Wazazi acheni UHUNI, najua hampendi kuambiwa ukweli lakini hakuna jinsi acheni UHUNI. Najua wengine watakuja na maneno Yao ya kipumbavu na kutisha kuhusu laana lakini ukweli ni kuwa acheni uhuni. Hapa hakuna cha laana wala ndugu yake Radhi, huu ni ukweli, mnazingua.

Nawaambiaga Vijana kuwa kama Mzazi wako alishindwa kukupa Urithi usiondoke hapo nyumbani, kaa hapo hapo mpaka akupe kilichochako. Na Kama wazazi wako hawana makazi, muandame kokote mpaka kieleweke.
Vitisho vyao visikuogopeshe havina msingi wowote.

KIJANA ATAONDOKA NYUMBANI KWA BABA NA MAMA YAKE IKIWA HAYA YATAFANYIKA
1. Atapewa Urithi wake,
Na Kama ni mzaliwa wa Kwanza au wamwisho ndiye anayepaswa kurithi Mali kulingana na utamaduni wa kabila Lenu basi huyo atabaki.

2. Endapo atajiweza hata bila kupewa Urithi.
Wapo Vijana ambao wamejaliwa uwezo wankupambana mara wanapokua wakubwa, kijana Kama unajiona unauwezo wa kuendesha maisha yako pasipo Urithi pia inaruhusiwa.

3. Atataka kuoa.
Kijana akitaka kuoa itampasa aondoke nyumbani kwao, wazazi wampe kilichochake, sehemu ya Urithi wake aondoke nao. Na huo Urithi uwe reasonable sio umpe Redio au Feni useme ndio Urithi, Urithi utakaomsaidia mtoto aendeshe maisha yake.
Mara nyingi Urithi wa wazazi Bora hujikita katika nyenzo za uzalishaji Kama vile mashamba, viwanja, visima vya maji au Nyumba, mifugo Kama NG'OMBE au Mbuzi, Miradi ya biashara Kama maduka, viwanda, n.k.
Sio umpe mtoto vitu havieleweki ndio uote Nimempa Urithi, huo ninauita UHUNI.

Siku hizi wazazi wamekuja na visingizio vya hovyo kabisa. Unakuta mzazi anasema, Mimi mwanangu Nimempa Elimu ndio Urithi wake. Pumbavu!
Elimu sio Urithi elimu ni basic need Kwa mwanadamu ambayo mzazi lazima umpe mwanao.

Ni ujinga na upumbavu kusema mtoto wangu namrithisha Elimu, Mimi nilipokuwa naambiwa hivyo nilikuwa nakataa katakata kuwa elimu niendayo kusoma sio Urithi isipokuwa ni sehemu ya basic need kwa binadamu.

Urithi lazima kiwe kitu unachokimiliki, sasa unakuta mzazi hata hajasoma anakuambia nimekupa elimu kuwa Urithi wako, ajabu hii! Elimu ambayo hauna?
Au unakuta mzazi anaelimu kubwa tuu labda ni Daktari, alafu anamuambia mtoto wake ambaye anaelimu ya sheria au Mwalimu, anamwambia, nimekurithisha elimu, sio kweli.

Unaposema Urithi unazungumzia Jambo ambalo unalomilikilulilonalo na unalompa mtu Kwa hiyari au pasipo hiyari. Mfano Mtoto anawezarithi Sura au maumbile ya wazazi wake, sauti, akili, miondoko, magonjwa miongoni mwa mambo mengine. Hiyo tunasema huo ni Urithi.

Elimu sio sehemu ya Urithi labda AKILI inaweza kurithiwa.

Elimu lazima mzazi Ampe mtoto mbali na Urithi ili kumfanya mtoto aweze kuyakabili Mazingira na Mali alizozirithi kutoka Kwa wazazi wake.

Mfano;
Mzazi WA kimasai au kisukuma kabla hajamrithisha mtoto Mali/mifugo ni lazima amfundishe/Ampe elimu ya mifugo na namna ya kuchunga NG'OMBE, Mbuzi na Kondoo. Mtoto akishakua mtu mzima Baba ndio humrithisha mtoto wake Sehemu ya mifugo Kama Urithi na Kwa vile mtoto anaelimu ya mifugo basi haitamsumbua.

Kumbuka mzazi hawezi sema nimekupa Urithi WA elimu ya kufaga NG'OMBE Bali atasema nimekupa Mali/mifugo Kama Urithi, Kwa vile unaelimu ya mifugo basi waweza kutenda Kwa Amani na Mungu akufanikishe.

Mfano wa pili,
Kwa familia za Wakulima,
Mtoto hufundishwa kulima, kutambua magonjwa ya mimea na namna ya kuhifadhi chakula. Kisha akishakua na kutaka kujitegemea Mtoto atapewa Urithi WA mashamba ambayo atayatumia kuendesha familia yake.

Sio umpe mtoto elimu ya kilimo alafu akatafute mwenyewe Shamba huo ni uhuni.
Ni Bora umpe Shamba alafu akatafute mwenyewe Elimu ya kilimo, hivyo ndivyo ilivyo.

Sasa wazazi wa kileo Kwa ujanja ujanja hujiingiza gharama zisizo na maana kumpa mtoto elimu ambayo kimsingi Kama hataajiriwa basi itakuwa haina kazi yoyote.

Unamsomesha mtoto Ada Kwa mwaka milioni mbili Kwa miaka minne mpaka sita alafu akimaliza shule anakosa chakufanya alafu unamuambia asikulaumu, wewe si kichaa tuu.

Mtoto anamaliza shule, humpi hata Urithi WA Shamba au hata kiwanja ambacho kimsingi ungeweza kumnunulia Kwa Ada Ileile aliyosomea.
Yaani umsomeshe mtoto Kwa Ada ya milioni mbili alafu ushindwe kumfurahisha mtoto hata Shamba la laki tano🤣🤣🤣 wewe Kama sio mwendawazimu ni Nani.

Sisemi kuwakamia hapa, najaribu Kueleza na kuamsha akili zetu.

Elimu sio Urithi, Hilo mkae mkilijua.

Mimi pia ni mzazi, siwezi waambia watoto wangu ati nimewarithisha Elimu [emoji3][emoji3]
Kwa kweli waliniona Baba Yao ni mhuni sitawalaumu.

Mzazi Bora ni Yule anayeacha Urithi Kwa watoto wake.
Elimu sio Urithi.

Elimu inatabia ya kubadilika kulingana na wakati. Unamsomesha mtoto hiki Kwa vile wakati huu kinalipa akimaliza kitu hicho kimepitwa na wakati, nazungumzia thamani yake imeshuka, thamani ya elimu inashuka kutokana na kuwa siku hizi kila mtu anaouwezo wa kuipata.

Elimu ya sasa sio elimu ya baadaye.

Lakini ardhi ya sasa, au Shamba la sasa ni hilohilo hata miaka Mia ijayo, tena thamani yake ndio inaongezeka.

Rithisha mtoto viwanja, nyumba, mashamba, viwanda Kama unavyo, visima vya maji, migodi Kama unayo, hotel au lodge, Mifugo sio Sana kwani tabia ya nchi na Hali ya hewa haitabiriki.

Sio mzazi unakazi ya kusumbua watoto wakutumie pesa kisa uliwazaa na kuwasomesha, uliwasomesha vitu visivyoeleweka. Mrithishe mtoto Mradi Kama mashamba au Nyumba au viwanja, ndio umuombe akuhudumie.

Sasa mtoto hata Mradi wankumuingizia kipato Hana, kuishi kwenyewe anaishi Kama Ndege, Kodi inamsumbua, chakula kinamsumbua, bado na wewe umsumbue, Doooh!! Huo unaitwa uhuni hata Kama watoto wanashindwa kutuambia.

Nani asiyejua maisha magumu pasipo kuwa na chakuanzia, Urithi ndio starting point ya mtoto.
Vijana wa sasa wanahangaika kutokana na makosa ya Sisi wazazi. Alafu tunatishia na laana. Pumbavu hakuna laana za hivyo.

Mtoto awaze Kodi.
Mtoto awaze chakula
Mtoto awaze mavazi yake,
Mtoto awaze atapata wapi mahari, alafu unakuta mzazi anakuuliza mbona hauoi utafikiri alikupa mahari, pumbavu.
Mtoto awaze namna ya kwenda ukweni,
Mtoto awaze Harusi,
Mtoto awaze kumhudumia mzazi wake
Mtoto awaze serikali.
Hayo kisa kisingizio cha kumsomesha?

Urithi haupitwi na wakati kwani ni Jambo la miungu, Mungu ndio kaliweka.
Elimu Kwa vile ni man-made lazima ipitwe na wakati.
Ndio maana Kwa miaka ya 90 mtu mwenye elimu alikuwa keshatoboa lakini sio Kwa Zama za sasa.

Wazazi tuache UHUNI, turithishe watoto Mali za uhakika zitakazowasaidia kuzalisha Mali au kuendesha maisha yao.

Ulikuwa nami, Baba mhuni.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Mabwepande, DAR ES SALAAM

Hoja yako ni nzuri sana,actually mimi nina msimamo wangu kuhusu namna itakavyokuwa Kwa wanangu,wataendelea nilipo ishia mimi sio kuanza upya hapana
Chochote ninacho kifanya mimi ni kwa ajili ya vizazi vyangu vingine badae...
Nina mpango hata wasisome sanaa kama mimi ikizidi sana labda degree level then waendeleze mambo yangu Mungu akijalia
Dunia inabadilika kwa sasa elimu ni ya kutoa ujinga tu huu ndio ukweli
Miaka ya 90 hakukua na wasomi wengi hivyo elimu ilikuwa hot cake
Mzazi fikiria unapomsomesha mwanao muandalie nini cha kufanya badae kabisa hii issue ya ajira ndio kwanza imeanza huko mbeleni itakuwa tafrani
 
Sio lazima Kwa wahuni.

Huwezi mzaa mtoto alafu usimpe Fungu lake labda uwe mwendawazimu usiyejitambua.

Wazazi wasiojielewa, masikini wa Mali na akili ndio huwaza hivyo.

Mtoto hata Kama huridhishwi naye unaowajibu wa kumpa Fungu lake, hakukutuma umzae, mpe fungu lake atajua mwenyewe.
Sio ulete Uhuni wako WA kipuuzi.

Sheria za Dini ni lazima kuacha Urithi Kwa watoto wa kuwazaa.
Achana na sheria hizi zinazoweza kutungwa na wahuni walioweza kujipenyeza kwenye uongozi.
Mzazi yeyote mwenye mtoto dhamira yake kuu ni kumrisisha mwanae mali, elimu, mila na desturi za ukoo husika. Hilo lengo hutimia bila hata kuomba iwapo kama mwana ana mwelekeo wa kufuata masharti na vigezo walivyojiwekea wazazi. Kama kijana hakidhi hivyo vigezo, hakuna namna mtu au taasisi itakayo lazimisha mzazi atoe urithi.
 
Mzazi yeyote mwenye mtoto dhamira yake kuu ni kumrisisha mwanae mali, elimu, mila na desturi za ukoo husika. Hilo lengo hutimia bila hata kuomba iwapo kama mwana ana mwelekeo wa kufuata masharti na vigezo walivyojiwekea wazazi. Kama kijana hakidhi hivyo vigezo, hakuna namna mtu au taasisi itakayo lazimisha mzazi atoe urithi.


Muelekeo anautoa mzazi sio mtoto.
 
Hoja yako ni nzuri sana,actually mimi nina msimamo wangu kuhusu namna itakavyokuwa Kwa wanangu,wataendelea nilipo ishia mimi sio kuanza upya hapana
Chochote ninacho kifanya mimi ni kwa ajili ya vizazi vyangu vingine badae...
Nina mpango hata wasisome sanaa kama mimi ikizidi sana labda degree level then waendeleze mambo yangu Mungu akijalia
Dunia inabadilika kwa sasa elimu ni ya kutoa ujinga tu huu ndio ukweli
Miaka ya 90 hakukua na wasomi wengi hivyo elimu ilikuwa hot cake
Mzazi fikiria unapomsomesha mwanao muandalie nini cha kufanya badae kabisa hii issue ya ajira ndio kwanza imeanza huko mbeleni itakuwa tafrani

🙏🙏🙏

Limbukeni WA elimu walioanza kusomesha miaka ya 2000 ndio wanakuambia elimu ni Urithi
 
Umeongea ukweli mtupu ,kwa life ili lilivyo ni muhimu sana kwa mzazi kumuandalia urithi mwanae ,just imagine kama wazazi wetu wangetuandalia viwanja enzi hizo ina maana kwasasa tusingepanda shida ya kupoteza fedha kwa ajili ya kununua viwanja,hii inawezekana kwasasa ukanunua shamba huko nje ya mji baada ya miaka 25 unamkabidhi mwanao means patakuwa town.

Ukimfungulia hisa kwenye stable company au ukawa na plan ya kumuwekea amount flan kila mwezi kwa muda wa miaka 10 ijayo itakuwa na mpunga mwingi.

kumjenga kibizness zaidi hasa kulima mboga mboga ,kufuga kuku ,kuuza duka etc hata akifikisha 18 anakua na upeo wa biashara,huo ndiyo urithi ,mambo ya elimu ni JAU.


Umenena kweli kabisa Mkuu
 
Hoja nzuri lakini ina vinasaba vya upumbavu! Mzazi gani hataki kuwa na mali? mzazi gani hataki wanaye wawe na maisha mazuri? Ukiona hakuacha hivyo vitu jua alipambana akaishia kushindwa.

HILI WAZO LIANZE NA BABA WEWE KWA WANAO

Acha kulilia mali za mwenzako ambazo hana. Hii inatoa ishara mbaya kwa kizazi hiki cha smartphone!
 
Hoja nzuri lakini ina vinasaba vya upumbavu! Mzazi gani hataki kuwa na mali? mzazi gani hataki wanaye wawe na maisha mazuri? Ukiona hakuacha hivyo vitu jua alipambana akaishia kushindwa.

HILI WAZO LIANZE NA BABA WEWE KWA WANAO

Acha kulilia mali za mwenzako ambazo hana. Hii inatoa ishara mbaya kwa kizazi hiki cha smartphone!


Mtu hupata anachokitafuta.

Mtu huvuna alichopanda.

Nafikiri nimeeleweka
 
Back
Top Bottom