Wazazi acheni uhuni na visingizio, toeni urithi kwa watoto. Elimu sio urithi!

Wazazi acheni uhuni na visingizio, toeni urithi kwa watoto. Elimu sio urithi!

Unauza nchi ununue Teknolojia uite akili kubwa? Utaishi wapi nyumbu wewe?

Uza Rasilimali ukiwa unazonyingi, lakini unahiyo hiyo moja unauza kisa elimu si Utaonekana Mpumbavu?

Huwezi uza simu ununue vocha, au uuze Baiskeli ununue Kengele, labda uwe kichaa.

Unapofanya Jambo lolote usisahau akili na maarifa.
Nimecheka sana, mtu anauza gari ili anunue matairi ya gari😂
 
Tatizo wengi wenu hamna mawazo ya Kifalme mna mawazo ya kitumwa.
Unapoamua kuzaa ni wazi utazingatia suala la urithi, tatizo linakuja pale ambapo uliyemzaa haelekei wala hataki kuhangaika, mtoto anayedai urithi kwa nguvu kisa hakuomba kuzaliwa anapataje huo urithi?.
 
Mpe mtoto Urithi atajiwezesha mwenyewe.

Hata hii nchi tumeirithi Kwa Mababu zetu, tumia akili ndogo Mzee.

Wanasiasa wanakufanganya elimu ni Urithi WA mtoto nawe unalidaka Kama lilivyo, wakati wao wanahodhi Maeneo na kujilimbikizia Mali za watoto na vitukuu vyao.

Sijui kama unanielewa
Wanasiasa ndio zao hizo, unafikiri zile tilion kadhaa ambazo hazionekaniki zimeibiwa kwa ajili gani?

Leo hii vijana wote wenye jina la JPM hawawezi kufa maskini sababu mzigo uliopigwa pasu umewaacha kila mmoja akiwa vizuri sana!
 
Unapoamua kuzaa ni wazi utazingatia suala la urithi, tatizo linakuja pale ambapo uliyemzaa haelekei wala hataki kuhangaika, mtoto anayedai urithi kwa nguvu kisa hakuomba kuzaliwa anapataje huo urithi?.
Hahahhaha mtoto huyo kiazi haswa sema una wajibu wa kummegea kipande chake akafie mbele.
 
Ndio uwape watoto Urithi usilete uhuni wako hapa.

Wewe sio Kwa vile ulikuwa na uwezo wa ku-fight ukadhani hata watoto wako au wajukuu watakuwa hivyo. Kama unafikiri hivyo jua akili zako zinamashaka,

Ninapoandika hapa simaanishi Mimi nategemea Urithi Hasha! Isipokuwa najaribu kuangalia Wale wenzangu na miye wasio na uwezo wa kupambana na maisha.
Unakuta mzazi alifikia Ukurugenzi ila watoto hawana ajira
 
Wanasiasa ndio zao hizo, unafikiri zile tilion kadhaa ambazo hazionekaniki zimeibiwa kwa ajili gani?

Leo hii vijana wote wenye jina la JPM hawawezi kufa maskini sababu mzigo uliopigwa pasu umewaacha kila mmoja akiwa vizuri sana!



🤣🤣🤣🤣

Mwanasiasa anakuambia jiajiri alafu yeye na watoto wake wameajiriwa.

Mwanasiasa anakuambia elimu ndio Urithi hivyo uza hata Mali zao mtoto apate Elimu.

Wakati yeye anafanya kila mbinu apate Mali za kurithisha Watoto.
 
Muelekeo anautoa mzazi sio mtoto.
Swadakta!... Mzazi siku zote ana lengo la kumrithisha mtoto, hapa nina maana ya mtoto aliyezaliwa kufuatia mipango rasmi ya ndoa.

Katika makuzi mzazi atatekeleza vipengele viwili vya Mwanza ulivyoviainisha.

Changamoto itakuja kwenye hicho cha tatu, kijana akianza kusigana na wazazi wake na mbaya zaidi kudai apewe urithi.... Hakuna mahali popote mzazi atalazimika kutoa urithi.
 
Nimecheka sana, mtu anauza gari ili anunue matairi ya gari😂


Si ndio hapo sasa.

Elimu sio kitu cha kushikika, kipo akilini.

Ndio maana watu walipigania nchi zipate Uhuru wapate ardhi ya kuishi wao na kizazi Chao.

Nchi hii tumeirithi Kwa Wazee wetu.
Sasa katika level ya kifamilia lazima mzazi apiganie Uhuru wa familia na kizazi chake kipate ardhi na Maeneo ya kuendesha maisha yao
 
Swadakta!... Mzazi siku zote ana lengo la kumrithisha mtoto, hapa nina maana ya mtoto aliyezaliwa kufuatia mipango rasmi ya ndoa.

Katika makuzi mzazi atatekeleza vipengele viwili vya Mwanza ulivyoviainisha.

Changamoto itakuja kwenye hicho cha tatu, kijana akianza kusigana na wazazi wake na mbaya zaidi kudai apewe urithi.... Hakuna mahali popote mzazi atalazimika kutoa urithi.


Kidini na kiroho analazimika.

Mtoto lazima apewe Urithi hata Kama ni mwehu kiasi gani.

Ni moja ya majukumu makuu ya Mzazi.

Wazazi wa kileo hasa waliozaliwa miaka ya 1950 ndio wameanza kucheza Rafu zao ndio maana hata heshima imeshuka.

Mungu kama Mzazi Mkuu ametuachia dunia Kama Urithi wetu Sisi Wanadamu.

Bila kujali tunaitumia vipi, bila kujali tunamkosea au hatumkosei.
Angekuwa Mungu mhuni tuu Kama angekuwa na mawazo ya kipumbavu ati asitoe Urithi kisa hatumtii au kufuata anachotaka.

Nafahamu wazazi wengi WA sikuhizi hawajafundwa tangu wakiwa wadogo, hivyo hawawezi elewa nazungumzia nini hapa
 
Unapoamua kuzaa ni wazi utazingatia suala la urithi, tatizo linakuja pale ambapo uliyemzaa haelekei wala hataki kuhangaika, mtoto anayedai urithi kwa nguvu kisa hakuomba kuzaliwa anapataje huo urithi?.
Tatizo hatulei watoto kama warithi.Mrithi anaandaliwa,mrithi sio tu mmiliki,mrithi anajukumu kubwa la kutunza na kuendeleza mali aliyorithi mpaka pale atakapo ikabidhi iyo mali kwa kizazi kinachofuata.
 
Kidini na kiroho analazimika.

Mtoto lazima apewe Urithi hata Kama ni mwehu kiasi gani.

Ni moja ya majukumu makuu ya Mzazi.

Wazazi wa kileo hasa waliozaliwa miaka ya 1950 ndio wameanza kucheza Rafu zao ndio maana hata heshima imeshuka.

Mungu kama Mzazi Mkuu ametuachia dunia Kama Urithi wetu Sisi Wanadamu.

Bila kujali tunaitumia vipi, bila kujali tunamkosea au hatumkosei.
Angekuwa Mungu mhuni tuu Kama angekuwa na mawazo ya kipumbavu ati asitoe Urithi kisa hatumtii au kufuata anachotaka.

Nafahamu wazazi wengi WA sikuhizi hawajafundwa tangu wakiwa wadogo, hivyo hawawezi elewa nazungumzia nini hapa
Hahahahah watoto wanabaguliwa sikuhizi!
 
Ndugu Maisha ni muendelezo wa kizazi na mali.Sasa kila kizazi kikiwa kinaanza kutafuta upya ni lini koo/familia zitatoka kwenye lindi la umasukini.Hapa ndipo Wahindi na Waarabu walipo tushinda.Suala la Uchumi sio la mtu binafsi,ni suala la familia/ukoo.
Watoto wa kihindi na kiarabu kama Mutaleeb “sema tena” ni ma Don toka zama zile wanamiliki basi za SadiQ Line ila utajiri ulianzia kwa familia. Wamesoma shule tulizosoma sema tu exposure ya biashara walianzishiwa toka primary!

Wakaurithishwa mbinu sahizi wana pesa na kizazi kifuatacho pia kitakuwa na pesa zaidi! Siku wabongo wakijifunza kuwa pesa ndio huleta pesa ingine watajikomboa katika umaskini! Tuna la kujifunza toka uchagani 😅!

Maswala yale ya kujitutumua uonekane una hela ukoo mzima na kuvimba huku wanao unashindwa kuwapa njia nao watoboe ndio yale unakufa watu wanabaki dah baba yao alikuwa na pesa sana!
 
Kidini na kiroho analazimika.

Mtoto lazima apewe Urithi hata Kama ni mwehu kiasi gani.

Ni moja ya majukumu makuu ya Mzazi.

Wazazi wa kileo hasa waliozaliwa miaka ya 1950 ndio wameanza kucheza Rafu zao ndio maana hata heshima imeshuka.

Mungu kama Mzazi Mkuu ametuachia dunia Kama Urithi wetu Sisi Wanadamu.

Bila kujali tunaitumia vipi, bila kujali tunamkosea au hatumkosei.
Angekuwa Mungu mhuni tuu Kama angekuwa na mawazo ya kipumbavu ati asitoe Urithi kisa hatumtii au kufuata anachotaka.

Nafahamu wazazi wengi WA sikuhizi hawajafundwa tangu wakiwa wadogo, hivyo hawawezi elewa nazungumzia nini hapa
Sawa kinadharia ni hivyo! Lakini unadhani utekelezaji wake unawezekana?... Hata mahakama zinategemea kuwe na "testament" ...kama mzazi hakuacha urithi kwa makusudi unafanyaje?.

Hii changamoto ya urithi nimeiona Ulaya. Pamoja na kupanga uzazi mtoto anageuka kuwa tegemezi jumla, kisa? Hakuomba kuzaliwa na hivyo wewe mzazi jukumu lako ni kumtunza hâta kama ni mtu mzima. Wengine wanafikia hata kupanga mauaji ili wapate urithi.
 
Nimesomesha na ninasomesha wanangu kwa shida halafu niwaachie mashamba wao pesa zao kwanini wasinunulie mashamba kama wanataka? Au unataka wanangu pesa zao ziishie kwenye ulevi,ngono nk?
Mm sasa nakula bia tamu kwa kwenda mbele.
Akili za kijima hizi! Kwahio Mo Dewji hela na makampuni alioachiwa aendeshe na baba yake zile mali anatombea na kulewea bia?
 
Tatizo hatulei watoto kama warithi.Mrithi anaandaliwa,mrithi sio tu mmiliki,mrithi anajukumu kubwa la kutunza na kuendeleza mali aliyorithi mpaka pale atakapo ikabidhi iyo mali kwa kizazi kinachofuata.
Sasa unamuaandaaje mrithi wako kama sio kupitia malezi? Mpaka kufikia kuandika na kutoa urithi, kuna mchakato ambao maamuzi yake yako kwa mzazi kwa asilimia mia..
 
WAZAZI ACHENI UHUNI NA VISINGIZIO VYA KIPUUZI. TOENI URITHI KWA WATOTO. ELIMU SIO URITHI

Anaandika Robert Heriel.
Yule shahidi kutoka Nyota ya Tibeli.

Andiko hili laweza waumiza wengi. Ikiwa unajihisi unamoyo dhaifu nakusihi usisome. Na ikiwa utasoma basi nisihusike na maumivu na madhara yatakayojitokeza nafsini mwako.

Niite Taikon wa Fasihi, Kuhani katika Hekalu jeusi.

Baba anamajukumu makuu matatu ndani ya familia, nayo ni;
1. Kuhakikisha ulinzi na usalama ndani ya familia(mke na watoto wake)
2. Kuihudumia familia( mke na watoto wake)
3. Kuzalisha Mali na kuandaa Urithi Kwa kizazi chake.

Hivyo Sisi Vijana tunapaswa tutambue mambo hayo matatu, mambo hayo hayana excuse nilazima yafanyike ili heshima ya Baba ilindwe.
Kabla hujaoa na kuzaa watoto lazima ujiulize, je unauwezo wa kumlinda na kumfanya Mkeo na watoto wawe salama?
Pili, unauwezo wankuwahudumia mke na watoto? Mwisho je mipango yako na uwezo wako ukoje katika kuzalisha na kuandaa Mali za Urithi Kwa watoto wako kulingana na nyakati na Zama watoto wako watakazoishi?

Siku za hivi karibuni kumezuka uhuni Fulani hivi Kwa wazazi hasa wababa kuleta visingizio vya kitoto kuhusiana na masuala ya kumuandaa mtoto na ulimwengu.

Wazazi acheni UHUNI, najua hampendi kuambiwa ukweli lakini hakuna jinsi acheni UHUNI. Najua wengine watakuja na maneno Yao ya kipumbavu na kutisha kuhusu laana lakini ukweli ni kuwa acheni uhuni. Hapa hakuna cha laana wala ndugu yake Radhi, huu ni ukweli, mnazingua.

Nawaambiaga Vijana kuwa kama Mzazi wako alishindwa kukupa Urithi usiondoke hapo nyumbani, kaa hapo hapo mpaka akupe kilichochako. Na Kama wazazi wako hawana makazi, muandame kokote mpaka kieleweke.
Vitisho vyao visikuogopeshe havina msingi wowote.

KIJANA ATAONDOKA NYUMBANI KWA BABA NA MAMA YAKE IKIWA HAYA YATAFANYIKA
1. Atapewa Urithi wake,
Na Kama ni mzaliwa wa Kwanza au wamwisho ndiye anayepaswa kurithi Mali kulingana na utamaduni wa kabila Lenu basi huyo atabaki.

2. Endapo atajiweza hata bila kupewa Urithi.
Wapo Vijana ambao wamejaliwa uwezo wankupambana mara wanapokua wakubwa, kijana Kama unajiona unauwezo wa kuendesha maisha yako pasipo Urithi pia inaruhusiwa.

3. Atataka kuoa.
Kijana akitaka kuoa itampasa aondoke nyumbani kwao, wazazi wampe kilichochake, sehemu ya Urithi wake aondoke nao. Na huo Urithi uwe reasonable sio umpe Redio au Feni useme ndio Urithi, Urithi utakaomsaidia mtoto aendeshe maisha yake.
Mara nyingi Urithi wa wazazi Bora hujikita katika nyenzo za uzalishaji Kama vile mashamba, viwanja, visima vya maji au Nyumba, mifugo Kama NG'OMBE au Mbuzi, Miradi ya biashara Kama maduka, viwanda, n.k.
Sio umpe mtoto vitu havieleweki ndio uote Nimempa Urithi, huo ninauita UHUNI.

Siku hizi wazazi wamekuja na visingizio vya hovyo kabisa. Unakuta mzazi anasema, Mimi mwanangu Nimempa Elimu ndio Urithi wake. Pumbavu!
Elimu sio Urithi elimu ni basic need Kwa mwanadamu ambayo mzazi lazima umpe mwanao.

Ni ujinga na upumbavu kusema mtoto wangu namrithisha Elimu, Mimi nilipokuwa naambiwa hivyo nilikuwa nakataa katakata kuwa elimu niendayo kusoma sio Urithi isipokuwa ni sehemu ya basic need kwa binadamu.

Urithi lazima kiwe kitu unachokimiliki, sasa unakuta mzazi hata hajasoma anakuambia nimekupa elimu kuwa Urithi wako, ajabu hii! Elimu ambayo hauna?
Au unakuta mzazi anaelimu kubwa tuu labda ni Daktari, alafu anamuambia mtoto wake ambaye anaelimu ya sheria au Mwalimu, anamwambia, nimekurithisha elimu, sio kweli.

Unaposema Urithi unazungumzia Jambo ambalo unalomilikilulilonalo na unalompa mtu Kwa hiyari au pasipo hiyari. Mfano Mtoto anawezarithi Sura au maumbile ya wazazi wake, sauti, akili, miondoko, magonjwa miongoni mwa mambo mengine. Hiyo tunasema huo ni Urithi.

Elimu sio sehemu ya Urithi labda AKILI inaweza kurithiwa.

Elimu lazima mzazi Ampe mtoto mbali na Urithi ili kumfanya mtoto aweze kuyakabili Mazingira na Mali alizozirithi kutoka Kwa wazazi wake.

Mfano;
Mzazi WA kimasai au kisukuma kabla hajamrithisha mtoto Mali/mifugo ni lazima amfundishe/Ampe elimu ya mifugo na namna ya kuchunga NG'OMBE, Mbuzi na Kondoo. Mtoto akishakua mtu mzima Baba ndio humrithisha mtoto wake Sehemu ya mifugo Kama Urithi na Kwa vile mtoto anaelimu ya mifugo basi haitamsumbua.

Kumbuka mzazi hawezi sema nimekupa Urithi WA elimu ya kufaga NG'OMBE Bali atasema nimekupa Mali/mifugo Kama Urithi, Kwa vile unaelimu ya mifugo basi waweza kutenda Kwa Amani na Mungu akufanikishe.

Mfano wa pili,
Kwa familia za Wakulima,
Mtoto hufundishwa kulima, kutambua magonjwa ya mimea na namna ya kuhifadhi chakula. Kisha akishakua na kutaka kujitegemea Mtoto atapewa Urithi WA mashamba ambayo atayatumia kuendesha familia yake.

Sio umpe mtoto elimu ya kilimo alafu akatafute mwenyewe Shamba huo ni uhuni.
Ni Bora umpe Shamba alafu akatafute mwenyewe Elimu ya kilimo, hivyo ndivyo ilivyo.

Sasa wazazi wa kileo Kwa ujanja ujanja hujiingiza gharama zisizo na maana kumpa mtoto elimu ambayo kimsingi Kama hataajiriwa basi itakuwa haina kazi yoyote.

Unamsomesha mtoto Ada Kwa mwaka milioni mbili Kwa miaka minne mpaka sita alafu akimaliza shule anakosa chakufanya alafu unamuambia asikulaumu, wewe si kichaa tuu.

Mtoto anamaliza shule, humpi hata Urithi WA Shamba au hata kiwanja ambacho kimsingi ungeweza kumnunulia Kwa Ada Ileile aliyosomea.
Yaani umsomeshe mtoto Kwa Ada ya milioni mbili alafu ushindwe kumfurahisha mtoto hata Shamba la laki tano🤣🤣🤣 wewe Kama sio mwendawazimu ni Nani.

Sisemi kuwakamia hapa, najaribu Kueleza na kuamsha akili zetu.

Elimu sio Urithi, Hilo mkae mkilijua.

Mimi pia ni mzazi, siwezi waambia watoto wangu ati nimewarithisha Elimu 😀😀
Kwa kweli waliniona Baba Yao ni mhuni sitawalaumu.

Mzazi Bora ni Yule anayeacha Urithi Kwa watoto wake.
Elimu sio Urithi.

Elimu inatabia ya kubadilika kulingana na wakati. Unamsomesha mtoto hiki Kwa vile wakati huu kinalipa akimaliza kitu hicho kimepitwa na wakati, nazungumzia thamani yake imeshuka, thamani ya elimu inashuka kutokana na kuwa siku hizi kila mtu anaouwezo wa kuipata.

Elimu ya sasa sio elimu ya baadaye.

Lakini ardhi ya sasa, au Shamba la sasa ni hilohilo hata miaka Mia ijayo, tena thamani yake ndio inaongezeka.

Rithisha mtoto viwanja, nyumba, mashamba, viwanda Kama unavyo, visima vya maji, migodi Kama unayo, hotel au lodge, Mifugo sio Sana kwani tabia ya nchi na Hali ya hewa haitabiriki.

Sio mzazi unakazi ya kusumbua watoto wakutumie pesa kisa uliwazaa na kuwasomesha, uliwasomesha vitu visivyoeleweka. Mrithishe mtoto Mradi Kama mashamba au Nyumba au viwanja, ndio umuombe akuhudumie.

Sasa mtoto hata Mradi wankumuingizia kipato Hana, kuishi kwenyewe anaishi Kama Ndege, Kodi inamsumbua, chakula kinamsumbua, bado na wewe umsumbue, Doooh!! Huo unaitwa uhuni hata Kama watoto wanashindwa kutuambia.

Nani asiyejua maisha magumu pasipo kuwa na chakuanzia, Urithi ndio starting point ya mtoto.
Vijana wa sasa wanahangaika kutokana na makosa ya Sisi wazazi. Alafu tunatishia na laana. Pumbavu hakuna laana za hivyo.

Mtoto awaze Kodi.
Mtoto awaze chakula
Mtoto awaze mavazi yake,
Mtoto awaze atapata wapi mahari, alafu unakuta mzazi anakuuliza mbona hauoi utafikiri alikupa mahari, pumbavu.
Mtoto awaze namna ya kwenda ukweni,
Mtoto awaze Harusi,
Mtoto awaze kumhudumia mzazi wake
Mtoto awaze serikali.
Hayo kisa kisingizio cha kumsomesha?

Urithi haupitwi na wakati kwani ni Jambo la miungu, Mungu ndio kaliweka.
Elimu Kwa vile ni man-made lazima ipitwe na wakati.
Ndio maana Kwa miaka ya 90 mtu mwenye elimu alikuwa keshatoboa lakini sio Kwa Zama za sasa.

Wazazi tuache UHUNI, turithishe watoto Mali za uhakika zitakazowasaidia kuzalisha Mali au kuendesha maisha yao.

Ulikuwa nami, Baba mhuni.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Mabwepande, DAR ES SALAAM
fanya kazi na wewe watoto wako uwape urithi acheni kupenda vya bure
 
Acha hadithi za vijiweni Budah!

90% matajiri wamerithi Mali kutoka Kwa Baba au Babu.

Wewe kalia hapo hadithi za kufikirika.

Unafikiri sheria za mirathi zipo Kwa ajili ya nini??

Ninyi ndio hawa wazazi wahuni ninaowazungumzia hapa.

Waarabu, wahindi, wayahudi, wachina, Wazungu wote wanajua nikisemacho Ila wewe Kwa vile umelemazwa na kusomea ujinga hujui nijazungumzia nini.

Elimu sio Urithi
Anafikiri williamson alikuja africa kwa miguu 😂😂😂 au kina Vasco Da Gama
 
Back
Top Bottom