Wazazi acheni uhuni na visingizio, toeni urithi kwa watoto. Elimu sio urithi!

Umesema ukweli kabisa
Waache visingizio urithi sio elimu
Shenzy urithi mkipewa mnakuwa walevi mbwa.Mi.mwanangu nimepanga asome mwisho form four nauza nyumba anaenda kusomea MAGIC aje kufanya maonesho tupige hela Africa bado kuja wehu wengi
 
Shenzy urithi mkipewa mnakuwa walevi mbwa.Mi.mwanangu nimepanga asome mwisho form four nauza nyumba anaenda kusomea MAGIC aje kufanya maonesho tupige hela Africa bado kuja wehu wengi



🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Kumbe mchaga, nilijua tu nyie wazee ndio mana mnapigwa ndele na watoto/wake zenu kisa roho mbaya za ubinafsi zilowajaa.
Wazee wengi wa kichaga wana roho mbaya sana tena za uchoyo hasa wale waliozaliwa ama kukulia huko uchagani ndio mana hawanaga maelewano mazuri na watoto wao pamoja na wake zao mifano ninayo mingi sana, waze wa kule ni kavu sana.
 
Shenzy urithi mkipewa mnakuwa walevi mbwa.Mi.mwanangu nimepanga asome mwisho form four nauza nyumba anaenda kusomea MAGIC aje kufanya maonesho tupige hela Africa bado kuja wehu wengi
🤸🏼‍♀️😂
 
Tatizo hata mtoto akipewa urithi, inapofikia hali ya mzazi anahitaji msaada mtoto hudai yeye ana majukumu ya kuangalia familia yake (yaani wajukuu wa mzazi) hivyo siyo kipaumbele.

Kuna wazazi wameshuhudia wenzao wakipitia hali ngumu huku watoto waliopewa mali wakitanua mjini, hivyo wameamua heri kila mtu ashinde vita vyake.
 
Usikimbilie kurithi mali tu,
Madeni nayo pia hurithiwa,
Ila elimu unaipata hata kabla ya kufariki wazee so hiyo sio urithi ni haki yako na ni lazima kuipata na ikitokea ukaikosa utataabika ingawa unaweza ukawa tajiri wa mali lakini masikini wa elimu
 
Anapiga bange huko kwenye metaverse
Ni kweli, hizi kama sio bangi basi ni kuchanganyikiwa. Badala ya kijna kuwaza amepata mtaji wa elimu atafute mali yake mwenyewe, yeye anang'ang'ania urithi kutika kwa wazazi? Kwani mzazi yeye amepata wapi mali? Na mawazo kama haya ni sumu kwa vijana, matokeo yake ni vijana kuwaua wazazi wao ili waweze kurithi mali
 
Katika wazazi wabinafsi nadhani wa Tanzania wanaongoza kwa kuwa na msimamo wa eti mtoto atafute chake mfano mzuri mtoto wa Magu akuwaipewa gari kuendesha cha ajabu mzee kaondoka mali ndio zimebaki kwake sasa anafanya atavyo lakini mzee angeweza kumjenga jinsi yakuzutumia akiwa hai no wonder mali za urithi zinatumiwa vibaya sababu ya visasi na chuki.

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 


Kosa bado linabaki Kwa mzazi
 


Ogopa kitu inaitwa uvivu na Kupenda Dezo
 
Usikimbilie kurithi mali tu,
Madeni nayo pia hurithiwa,
Ila elimu unaipata hata kabla ya kufariki wazee so hiyo sio urithi ni haki yako na ni lazima kuipata na ikitokea ukaikosa utataabika ingawa unaweza ukawa tajiri wa mali lakini masikini wa elimu


Unafikiri mzazi akifa madeni yake yanalipwa na Nani?
 
Ogopa kitu inaitwa uvivu na Kupenda Dezo
Uvivu ni character inayojengwa once motivation ikiwepo uvivu hauwezi kuwepo so ni jinsi unavyo mlea na misingi unayoweka kwa vijana wako..Leo hii Jack Chan kadeclare mali zake zote akifa zienda kwa yatima kitu ambacho watu awajui hamna mtu mwenye mentality ya kibabylon kama huyo Jack japo anasababu ya msingi baada ya mtoto wake kuwa na skendo za madawa akasema kama nikiwa hai ameshindwa tumia mali zangu ata nikifa hataweza zitumia vizuri bora niwape yatima zote...

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
 
Uko sahihi Elimu inaweza isiwe Urithi.

Kwangu mimi mambo ya urithi naona ni ujinga unaofanya familia zizidi kuwa masikini hivyo hakuna kitu nakichukia kama urithi kwenye mambo ya familia.

Urithi unafanya watoto wabweteke wasichangamshe akili kutafuta vyao na kutengeneza mategemezi, hii inapelekea familia kuwa masikini zaidi sababu watoto watakaa kusubiria ufe wachukue chao (kama mzazi ulivyowaaminisha).

Na urithi wa mali ni mpaka mmiliki afe au kama wakikurithisha wakati yeye yupo hai then atabaki na nini?
Pia urithi wa mali unagawanya familia sababu kila mtu atakuwa anachomoa chake na kuondoka na kama hakuna umoja na ushirikiano then hakuna familia wala hakuna nguvu tena.

Na wewe umeshawahi kujiuliza kwanini baba yako haishi kwa wazazi wake?
Unajua jinsi gani baba yako alipata alivyonavyo sasa hivi? Je alitegemea urithi?
Kama hakutegemea urithi kwanini wewe ulilie urithi?

Maana ya Familia ni kukusanyika pamoja ili kuleta ushirikiano na umoja ili kuzalisha nguvu.
Kama ule msemo maarufu wa "umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu"..

Sasa badala ya wazazi kugawa urithi.
Cha kufanya ni kumwambia kila kima mmoja atafute chake na baada ya hapo basi aende kuongezea kwenye mali za familia.
Hii italeta umoja na ushirikiano kwenye familia na kwenye umoja na ushirikiano kuna Nguvu.
Nguvu hii itatumika na itafanya Familia izidi kuimarika kila uchwao badala ya kugawanyika na kudhoofika baada ya kugawana urithi.

Mtu unayempa ugali kila siku lazima atakuja kwako kila siku kufuata ugali, badala ya kumpa ugali mpe njia ulizotumia kuupata huo ugali ili atafute wake.

Mtu ukimpatia urithi haijarishi ni kiasi gani cha mali basi hazitofika popote lazima zitapotea tu na kuisha kabisa.
Sababu hajui jinsi gani umezipata au mangapi umepitia na kuhangaika kiasi gani, hana uchungu nazo wala hajui moto wa jiwe.
Na hiyo ndio sababu familia tajiri huwa masikini ghalfa baada ya mmiliki kufa na kurithisha mali kwa watoto.

Lakini ukimwambia na kumfundisha njia ulizopita mpaka kupata vya kwako na yeye apite hizo'hizo mpaka kupata vya kwake.
Basi lazima atakuwa na uchungu wa mali zake kutokana na msoto aliopitia na atakuwa na nidhamu nazo na kamwe hatojaribu kuzichezea na kuzipoteza kizembe. hivyo hata zile za kwako atakuwa na uwezo wa kuziendeleza.

Kulilia Urithi ni dalili ya Uvivu wa kimwili, kufikiri na kiakili na ni vibaya zaidi ukimfundisha hivi mtoto wa kiume sababu ataamini ni haki yake kupewa now that's really bad.
Sababu mtoto wa kiume anatakiwa afundishwe kupambana na kutafuta vyake mwenyewe no matter what.

Wanangu nitawaambia jinsi ya kupamba na maisha na kuwa adaptable na mazingira yoyote huku wakiendeleza nilichokianzisha kwa kuongeza vya kwao juu yake haijalishi ni wakike au wakiume wote nitawakazia kibabe ila wakiume itakuwa more severe..
Ni kufight till you drop dead hakuna cha bure hata kama nilikuzaa.
 
Uko sahihi Elimu inaweza isiwe Urithi.

Kwangu mimi mambo ya urithi naona ni ujinga unaofanya familia zizidi kuwa masikini hivyo hakuna kitu nakichukia kama urithi kwenye mambo ya familia...
Urithi ungekuwa ujinga hii nchi ingekuwa Yenu?

Itashangaza mtu ni msomi asielwe concept ndogo niliyoieleza, pia itashangaza Kama mtu anaumri wa zaidi ya miaka 25 asielewe mantiki ha kile kilichozungumzwa hapa.
 
Urithi ungekuwa ujinga hii nchi ingekuwa Yenu??

Itashangaza mtu ni msomi asielwe concept ndogo niliyoieleza, pia itashangaza Kama mtu anaumri wa zaidi ya miaka 25 asielewe mantiki ha kile kilichozungumzwa hapa.
Sidhani hata kama umemaliza kusoma nilichokiandika.
Post nilipost dk 4 zilizopita na wewe umejibu dk 3 zilizopita.

Means umesoma andiko lote ndani ya dk 1 that's impossible.
 
Sidhani hata kama umemaliza kusoma nilichokiandika.
Post nilipost dk 4 zilizopita na wewe umejibu dk 3 zilizopita.

Means umesoma andiko lote ndani ya dk 1 that's impossible.
Nimesoma Mkuu.

Nimekuelewa,

Ninachojaribu Kueleza hapa ni kuwa wazazi tuhakikishe tunaacha Urithi Kwa watoto, nchi kubwa hivi ushindwe kuacha Urithi Kwa kweli itakuwa uzembe.

Labda sababu za Maradhi makuu, na kifo yaingilie kati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…