Wazazi acheni uhuni na visingizio, toeni urithi kwa watoto. Elimu sio urithi!



Hii inamgusa yeyote hata niliyeandika.

Shida Wanadamu hawapendi ukweli
 
Anapiga bange huko kwenye metaverse
Hivi anadhani kila mtu ana nyumba zaidi ya moja? Au benki ana billion?

Kwanza elewa kuwa mtu mwenye nyumba zaidi ya moja mjini ni mtu aliyezaliwa kijijini katika umaskini na nyumbani kwao alipokulia waliishi nyumba ya nyasi au matope! Huwezi kukuta mfano mtoto wa Nyerere ana nyumba zaidi ya moja. Mtoto wa mzee ruksa anatawala vizuri Zenji sababu hakuzaliwa katika family za kifukara kama zetu - tamaa na uroho!
Fikiria mtu unaoa ukiwa na 30! Unastaafu mtoto akiwa naye anaoa wewe upo 60! Kiinua mgongo unapata 300M na tunatumai bado una miaka 30 mbele ya kuishi. Hiyo pesa unanunua bondi ili kila mwezi upate million 3, ili maisha yasonge. Huyu mvuta bangi anaona uzigawe kwa watoto ili ule mafi (kichagga)? Ukijaliwa unakufa wakati mjukuu anaoa! Je, urithi wa mtoto una maana kweli?
 
Hivi mzazi wako ana kipi cha ziada ili akurithishe? Au unataka a distributed poverty tu
 

Kwahiyo zawadi ni urithi! Hovyo kabisa.
 
Kuna kina sie ambao tuna hakika hatuna cha kurithi hata itokee mshua kaitwa leo hii na Bwana!mali zote zinarithiwa na watoto wa mama mwingine,
Kwenye uzi inabidi tupite kimyakimya!
 
Mkuu, mzee baba, umepiga pale pale penye tatizo, la umaskini wetu wa fikra. Ni kweli elimu siyo urithi. Mungu akujaze nguvu ya kuzidisha mashambulizi katika ngome ya adui yetu namba moja aitwaye ujinga yaani ukosefu wa maarifa.
 
Mzee akiwa bado hai huo sio urithi ni uvivu wa kufikiri na uzembe wa kutafuta vyako, mzazi kukazaa, kakutunza,amekusomesha kuanzia chekechea mpaka umehitimu chuo kikuu au hiyo form four yako,nenda katafuta mali zako ili uishi maisha yako na umsaidie huyo aliyesababisha ukaweza kuleta huu uzi.
 
Kama kweli aisee yani kanakuja flani hivi ila sema n? kila mtu na familia yake tusizoeane sana
 
Mkishamaliza maliza kuhonga urithi mje kuanza kutusumbua tena tuwapokee na kuwachinjia kama mwana mpotevu, shubaamiti, if they can't make their own money they will waste yours!!!!!
 
hii thread ingependeza mzee wangu aisome[emoji23][emoji23][emoji23]..maana mzee kakaza fuvu hataki kuelewa.


alow mzee baba najua hayupo humu, lkn nitafanya kila njia hii mada imfikie, yaan nitaicopy na kwenda kuipaste kwa simu message inbox yake ilimladi tu aisome[emoji23].

yule mzee navyomjua hatoimaliza kuisoma ataifuta tu[emoji23][emoji23][emoji23]..
 
I couldn't agree more.

Kwa wanao amini maandiko Biblia inasema

Mit 13:22 SUV​

Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki.

Ila hii miafrika huu mstari huwa inajidai haijauona. Wanakufanya mtoto ndo mtaji.

Makampuni makubwa yote kuanzia ndani hadi nje ya nchi ni generational companies walianzisha mababu sasa wajukuu wanaendeleza ila bongo unarithishwa uchawi na madeni tu. Bongo nyoso
 
ndo mana mimi sijawahi kuwa muumini wa kwamba kijana akikua eti akajitafutie wengine mpaka wanawafukuza nyumbani.. KIzazi cha sasa cha ajabu sana wazee wa zamani hata kijana akitaka kuoa wao ndo wanasimamia show nzima mahari na kila kitu unapewa shamba na ngombe ukaanza maisha na mkeo leo hamna hiyo kitu.

Tutafute mali kwa ajili ya watoto wetu kurithi wasome wakimaliza wanarudi kurithi mali zako na kuziendeleza ndo inatakiwa kuwa hivyo.
 
Hivi mzazi wako ana kipi cha ziada ili akurithishe? Au unataka a distributed poverty tu
Hahaaa! Nilisema kabla kwamba wazee wetu tusiwaingize kwenye mjadala huu maana waliamini kila anayesomeshwa atakuwa amerithishwa jambo la kipekee. Ni kweli kwa sasa tukiwadai tutakuwa tunatafuta distributed poverty.
Msisitizo ni kwamba kizazi cha sasa kisipoteze mihela mingi eti kinarithisha elimu bora wakati ajira hakuna.
 
Umepewa elimu pambana kivyako unataka uandaliwe hadi mahari ya kuolea huo utakua uchoko sasa
 
Hangaika na mali yako Acha masuala ya urithi ndipo utaendelea
Utaendelea sawa ila angetoa urithi ingeleta bonding ya kizazi chake mpaka wajukuu wanakuwa na bonding kubwa kati yao maana wanajua nini babu yao alifanya katika familia ni kitu Mungu alitaka mzazi afanye kwa familia yake na ndo maana mtu akifa unasomwa wosia wa kizazi chake maana yake watu watataka kujua kizazi alichoacha kinamwelekeo gani? Au ameacha kizazi dhaifu duniani.
 
Hupewi elimu ili ukaajiriwe, la hasha. Unatafuta elimu ili uweze kupambana na maisha. Ukiona mtu anasema ameelimika ili akaajiriwe (utumwa) jua hajaelimika. Elimu inatengeneza hasslers kama anavyotamba Makamu wa Rais wa Kenya kwa kumpiga kijembe Kenyatta kuwa yeye alirithi lakini Rutto katafuta mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…