Wazazi amkeni, simu mnazowanunulia watoto wenu wanazitumia ndivyo sivyo

Wazazi amkeni, simu mnazowanunulia watoto wenu wanazitumia ndivyo sivyo

Hata wasipokuwa na smart phone watapigana miti tu. Smart phone unazisingizia, tatizo liko vichwani mwao. Ukiona mwanafunzi anatumia simu kutafuta site za ngono ujue asipokuwa na simu atahangaika kutafuta sehemu za kupiga chabo.
Soma Uzi hadi mwisho
 
Amkeni wazazi mnaopeleka vijana vyuoni kwenye upande wa simu za mkononi. Watoto wanawadanganya kuwa bila smartphone masomo hawezi kufaulu mnaanza kuhangaika kwa kununua simu za bei ghali kwa kuamini maneno yao.

Simu wanazotaka watoto wenu wanazitumia kwa:-
1. Kutukana serikali mitandaoni
2. Kujiingiza katika makundi ya ngono na upuuzi mwingine
3. Kufanya biashara nyingine haramu

Kama unataka kumsaidia mtoto anayeenda chuoni mnunulie "laptop" zipo hadi za 250,000 na utakuwa umemsaidia sana.

Endelea kumfuatilia mienendo yake hata akiwa chuoni usijisahau sababu huko ndio wanaenda kuharibika zaidi kimaadili usipomfuatilia.
Soma na uelewe ninacholenga
1. Uwezo wa Kufanya Kazi Nzito za Kielimu
Laptop ina uwezo mkubwa wa kuendesha programu za kitaaluma kama:

Microsoft Office (Word, Excel, PowerPoint)

SPSS, MATLAB, AutoCAD, R, Python, n.k.

Kuandika research papers, reports na presentations

Smartphone inaweza kusaidia, lakini haiwezi kufanya kazi hizi kwa ufanisi mkubwa.

2. Kuandika na Kuhariri Documents kwa Urahisi
Kuandika kazi ndefu kama mijadala, essays, projects au dissertation ni rahisi kwenye laptop.

Keyboard ya laptop ni bora kwa kuandika kwa kasi na usahihi.

3. Urahisi wa Kusoma na Kupitia Materials
Kusoma PDFs, slides, na eBooks ni rahisi zaidi kwenye screen kubwa ya laptop.

Laptop pia inaruhusu multitasking — unaweza kuwa na vitabu, notes na browser vyote kwa wakati mmoja.

4. Mahitaji ya Vyuo na Majaribio
Vyuo vingi vinahitaji wanafunzi wawe na laptop kwa ajili ya ku-submit assignments, kufanya mitihani ya mtandaoni, au kuhudhuria lectures za mtandao (Zoom, Google Meet, n.k.)

5. Uwezo wa Kutunza na Kuratibu Files
Laptop ina storage kubwa zaidi, hivyo unaweza kuhifadhi maelfu ya nyaraka, lectures, videos, n.k. kwa urahisi.
Karibu kwa mwenye hoja
Watu kama hawa ndio wanafanya CCM wazidi kututawala
 
Mimi mmojawapo nilifanya Ivo Tena Kuna safar Mzee alikua anaenda nchi fulan nilimsisitiza utadhan nikikosa simu na laptop napata disco ukweli na Mimi nilitaman kua navyo nilichoka kulingishiwa 😄
 
Back
Top Bottom