Expensive life
JF-Expert Member
- May 2, 2020
- 2,971
- 9,437
Inasikitisha sana kuona wazazi wanazaa tu kisha kuacha watoto wajilee wenyewe.
Dunia ya sasa imeharibika, hii imetokea juzi nikiwa nimelala zangu mchana majira ya saa saba, nikiwa kwenye usingizi mzito nasikia sauti ya mtoto mdogo akilalama aachiwe.
Sikutilia manani nikahisi huenda labda naota bahati nzuri wife alikuwa macho akaniamsha baba kuna mtoto hapa anafanyiwa kitu kibaya, ikanibidi niamke kweli nikasikia sauti ya mtoto mdogo wa kiume umri wake miaka minne akilalama.
Nikafungua pazia taratibu nakulikuta njemba likiwa limembania mtoto ukutani huku likiwa limemvua nguo, nikitoka kwa jazba kisha nikawajulisha majirani wengine wanusaidie tumkamate ni ajabu wamebaki tu wananishangaa.
Nikazunguka mwenyewe nyuma ya nyumba lile njemba lilipo niona likakurupuka na kumuachia mtoto kisha tukaanza kukimbiza huku nikiita mwizi, kwa kweli sikupata sapoti yeyote kutoka kwa raia wananitizana tu inaonekana huyu kijana anatoka mazingira yale wanamfahamu hivyo wameamua kumlinda.
Sikufanikiwa kumkamata hii kitu imeniuma sana, nilipeleka taarifa kwa wazazi wa mtoto wamejaribu kumuangali wanadai hakufanikiwa kumfanya chochote, nimewaachia wao hii kesi waifuatilie huyu kijana pale mtaani anafahamika.