Basi ngoja nikupe mwanga kidogo.
Kuna katuni na animation
Katuni zinazoonyeshwa kwenye Chanel za watoto kaa vile Disney Junior, Cartoon Network, Da Vinci learning, KidCo, Nickelodeon, hizi mara nyingi hua zimewalenga Watoto 2-10. Kwakweli sijawahi kuzitilia mashaka hizi cartoon na hizo Chanel nilizotaja hapo juu nimezitazama sana. Sijui kwa sasa mambo yamekuaje.. ila naona kuna PJ mask disney junior sio mbaya.
Sasa kuna hizi animation mara nyingi tunaziita Adult swim mfano wake ni kama zinazotengenezwa na studio kubwa za muvi kama vile Warner Bros animation, Dreamworks,Pixar,Bluesky, Disney, nk hizo ni zawatu wakubwa kuanzia 13. Kwa huku afrika miaka 13 bado Mtoto mdogo
Sasa kuna hizi animation hua zinawekwe kwenye streaming chanel kama vile Amazon, Netflix, Disney+, Etc hiz ndio mabaya kabisa mfano kuna Cartoon inaitwa The Invincible imetoka mwaka huu ni ya superhero ila ina umwagaji wa damu na ushoga humo.