Wazazi mmekuwaje?

Wazazi mmekuwaje?

Hizi dharau ndio kitu sipendi. Kim Jong Un anakutana na Trump DMZ na wanabonga safi tu. Sembuse mimi chalii na wewe mmatumbi/mmwera?
Kwa lugha gani! Nitaambiwa nimepeleka mvuta bhangi
Ongea maneno yaliyonyooka
 
Habari!

Nilipomaliza chuo nilipatwa na mkasa. Ile nimemaliza tu mitihani nikamtaarifu mama, tukaongea tu vizuri kwa muda mfupi chumbani kwake, sasa wakati natoka nje akaniuliza swali 'kwahiyo ushapata mtu wa kukuoa?' moyo ulishtuka halafu chap nikaendelea na safari hapo nikajifanya sijamsikia.

Ikawa wimbo anaoupenda 'ushapata wa kukuoa? Nikawa namwambia sipo tayari kwa sasa nikimjibu hivyo anaanza kutoa risala 'unajua inabidi uolewe mimi najisikia vibaya kukuona tu hapa nyumbani'

Siku moja nikamwambia mimi sijapata hata wa kunioa, akasema 'uzuri wote huo hakuna aliyesema anataka kukuoa' ilibidi tu nicheke mimi nilikuwa nishasoma akili yake kwamba uoga wa maisha unamsumbua.

Ishapita miaka 3 tokea kisa hiki kitokea, juzi nikasema acha niwaulize wenzangu kama wanakutana na maswahibu kama yangu sababu huu wimbo mama yangu bado anauimba.

Rafiki yangu FLORA
Yeye aliniambia alivyomaliza Mitihani alichelewa kurudi nyumbani kwa miezi kadhaa, sasa kuna siku akaumwa akalazwa mama yake alivyoenda hospital akamkuta Flora yupo na boyfriend wake ila huyo bf akawapisha waongee.

Mama yake akamuuliza 'huyo kijana ni nani' Flora akamjibu ni rafiki yake.
Mama yake akamwambia bills ni kiasi gani ili alipie! Flora akamwambia 'rafiki yangu ameshalipia' mama yake akaguna.

Sasa Flora alivyorudi kwao, mama yake akaanza kuimba nyimbo kila mara 'Yule rafiki yako yuko wapi akuoe kuliko kushinda ndani kila siku' Flora akaishia tu kucheka.

Rafiki yangu REBECCA
Yeye alikuwa anabanwa sana, ni wale watoto geti kali. Alivyomaliza chuo kuna siku akamuomba mama yake ruhusa ya kwenda kumsalimia rafiki yake. Mama yake hakumuuliza maswali mengi kama alivyokua anafanya hapo awali.

Jioni mapema Rebecca aliporudi mama yake akamwambia 'Mbona umerudi mapema' akamjibu nilienda kumuona tu mara moja. Mama yake akamwambia 'Ebu tembeatembea wachumba wakuone sio kujifungia tu ndani'

Ila ameniambia huo wimbo mama yake aliuacha baada ya yeye kupata kazi.

Rafiki yangu ASHA
Huyu ndiye amenichekesha sana, anasema tulivyomaliza chuo baba yake akawa anamwambia 'fanya uolewe sitaki kukuona nyumbani kwangu'

Kuna siku akaenda kazini kwa baba yake akamkuta yupo na wanaume wengine akawasalimia.
Kijana mmoja akamwambia mzee wake kwamba hakujua kama ana binti mkubwa vile! Mzee wake akajibu 'Huyu ni binti yangu kamaliza chuo mwaka huu na bado hajaolewa' wote wakaishia kucheka.

Haikupita miezi mingi baba yake akamletea mchumba, ubani ukachomwa sasa hivi yupo kwenye ndoa.

Nilichokiona wazazi wengi ambao hawajajipata kazi wanayotupa watoto wa kike ni kuolewa tena kama mtoto hajapata kazi ya kufanya.

Ila ukiwa na kazi nzuri unapata pesa, hii risala ya kuolewa hawatoi hata ukifikisha miaka 40.

Sasa sijui wa kulaumiwa ni CCM, wazazi wetu au sisi watoto.
KAMA SIO BIKRA HANA HADHI YA KUOLEWA
 
Heshima ya mwanamke ni kuolewa bila kujali una ajira rasmi au la!
Mzazi kushauri uolewe ni kutaka kukuheshimisha.
Ukiendelea kucheka na vijana nao wataendelea kucheka na wewe badae utalia wao wanacheka.
 
Wazazi wanataka uolewe kwasababu mbili. Kwanza, wanataka uolewe kwasababu wanataka maokoto na wewe umeshakuwa mkubwa hivyo basi upate mwenzako wa kusaidiana kuwalea na kuwanyanyua wadogo zako hiyo wanameweka ni lazima vichwani mwao.

Pili wazazi wanayajua maisha. Maisha kuyajua ni lazima ufike miaka kuanzia 40 kwenda juu. Hapo ni umri ambao hata wale wasio serious na Maisha wataanza kuwa serious bila kutaka. Ingawa wapo ambao wanaanza kuwa serious mapema sana ila ile inakuwa sio imara kama hii ya umri wa kuanzia miaka 40+.

Wazazi wengi kwa miaka yetu hii wameshavuka umri huo na wapo huko 60+. Hivyo basi, wewe kama binti wanakutazama namna unatumia uzuri wako kushangaa shangaa mjini ukipiga picha za kupost Instagram badala ya kuutumia uzuri wako kukamata bwege fulani na kumpa hamasa ya kujenga maisha bora na wewe na kujiwekea future ya kueleweka nae pamoja yaani mume.

Wengi mnatumia wakati huu kupuyanga halafu umri wa miaka 30 ukifika mnaanza kusumbuana na wanandoa mkitaka wenzenu walioanza kuyajenga maisha kitambo wawapishe ninyi muingie. Haya ndio madhira wazazi wako wanataka kukuepusha nayo.

Kimsingi wazazi wako wanataka kukufundisha kuishi kimkakati na sio kama mwanaharakati wa haki za wanawake. Wanajua utakwenda kwama wapi, ndio maana hata feminists mwenye kelele tele akifika tu kuanzia miaka 45 huwa ukweli unamzidi nguvu anaacha kubwatuka kama jibwa la kizungu.

Anyways, naomba tu nikuelekeze kuwa uwe mpole , wasikilize wazazi wako wanachokutaka ufanye wanajua unakwenda kukosea wapi, wasikilize wana hoja ya msingi sana. Kaza fuvu utakuja kuelewa kwa matendo ule msemo wa asiyesikia la mkuu huvunjika guu na mdharau mwimba mguu huota tende.
 
Hapana sio kweli kitu kipya ni kipya tu, na mtumba ni mtumba umalaya ni wakurithi
Jidanganye,umalaya ni chaguo.
Oa bikira halafu nje akutane na mishindo ya masela,hadi kwa mparange anatoa.
Ukikua utaelewa.Umalaya hauna ubikra umalaya ni chaguzi.
Wapo wameolewa wakiwa sio bikra ila wametulia katika ndoa zao,wapo wameolewa mabikra na wanagawa mpaka nyaaa huko nje.
Kua kwanza ndio utaelewa
 
Back
Top Bottom