Wazazi mnashirikiana na shule kuwatesa watoto

Umeandika point kubwa sana mkuu inafikia hatua mpaka jumapili watoto wanatakiwa waende shule nadhani hii ni kuwafaidisha walimu zaidi na pesa za mikakati na mitihani isiyo na faida .
Kitu cha ajabu serikali kila ikitoa maelezo hayafuatwi ,yan nchi hii hakuna utaratibu maalum unao ongoza shule wengine wanatoka saa 8:30 mchana ,wengine saa 9:30 mchana ,wengine saa 11 jion wengine likizo wanafunga wengine hawafungi mikoa mingine ijumaa masomo mwisho saa 6 mchana wengine saa 11 jion yani kila mtu anajiamlia anavyo taka.

Ukiuliza unaambiwa utaratibu wa mkoa sijui wilaya mara shule ndiyo imeamua yani fujo tupu. Elimu bongo sarakasi tupu.
 
Mbona sisi enzi zetu tulisoma shule nasomo yanaanza saa moja na nusu hadi saa nane kamili shule za serikali na binafsi utaratibu ulikuwa huo. Masomo ya ziada ya kulipia ilikuwa hiari ya mzazi.
Nakumbuka nikienda mikoani nilikuwa nawaona wanasoma hadi saa sita halafu wanaenda nyumbani halafu saa nane wanarudi shule hadi saa kumi.
 
Watoto wa siku hizi wanasoma kitu gani cha ajabu?
Hadi weekend unakutana nao saa 11 wanaenda shule.

Hasa hizi shule za serikali, Ni kama kuna mradi wa kukusanya pesa za wanafunzi kupitia masomo ya ziada
 
Sasa sikuhizi watoto kwanza wanabakizwa shule hadi muda wa likizo hadi mzazi unajiuliza kulikoni hii elimu ya miaka hii
 
Hao watoto wana wazazi, wazazi wameamu kufanya hivyo kwa watoto wao, hakuna shule inaweza amua kama mzazi hajaridhia.

Niliamua kuwa nawapeleka watoto shule asubuhi na kuwarudisha nyumbani, na hakuna ratiba ya ziada kwao.
Wazazi wengine hawajui kama wana mamlaka ya kuamua watoto waspend muda gani shule.
Kwa mfano; Shule ikiwaita wakaambiwa watoto lazima waje boarding kisa mitihani ya grade 4, wanalalamikia pembeni tu. Kukataa wanashindwa, so wanaishia kuburuzwa.
 
Mkishangaa ya Tanganyika basi hamjayaona ya Zanzibar, huko Wanafunzi wa secondary tuition wanaenda usiku yaani kuanzia saa 1 mpaka saa 4.
Shule wanaenda asubuhi ya saa ngapi na wanaotoka saa ngapi?
Please share hayo maarifa!
 
Umeandika point kubwa sana mkuu inafikia hatua mpaka jumapili watoto wanatakiwa waende shule nadhani hii ni kuwafaidisha walimu zaidi na pesa za mikakati na mitihani isiyo na faida .
Kuna shule anasoma mtoto wa jirani wanaenda had j2, afu ni private.
Najisemeaga Pesa zinatolewa ilo watoto wateseke, lol [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Naunga mkono hoja....

Unakuta katoto kadogo kamebeba begi kubwa mno limejaa madaftari na vitabu mpaka anatembea huku kainama....na ndio kwanza yupo darasa la 4 tu.

Hii sio sawa.
 
 
Yaani mimi my young anasoma grade 4 anaenda anaamka saa 11 anareport shulw saa 12 kamili anaanza na remedial then masomk saa 1 mpaka saa 10 then anaanza remedial tena saa 10-2 usiku...saa mbili ndio naumona home tena..sometimes hatuonani ata siku mbili hivi nakuta tuu kaniachia ujumbe au kanipigia sim dada uko wapi?Dad alienda shule kuweka complains akaambiwa either avumilie au amuhamishe shulw
 
Msisahau kuwaandalia mazingira ya kazi watoto wenu wanaosoma hizo shule wakimaliza.

Sifa zisishie tu kupoteza pesa bure kwa kujibana na kujitesa katika hizo shule.

Nawakumbusha elimu ya hapa nchini haitofautiani kati ya shule za pesa na zisizo za pesa kazi inabaki kwako kunyoa au kusuka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…