Wazazi na walezi, Kosa gani mtoto wako amewahi kufanya ila ukashindwa kumuadhibu sababu na wewe ulilifanya ukiwa mtoto?

Wazazi na walezi, Kosa gani mtoto wako amewahi kufanya ila ukashindwa kumuadhibu sababu na wewe ulilifanya ukiwa mtoto?

Teslarati

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2019
Posts
2,621
Reaction score
10,466
Habarini wana jamvi,

Nmesukumwa kuleta hii mada sababu nimekumbuka kitu nikaishia kucheka tu. Mwaka jana mtoto wangu wa pili alipelekwa kuandikishwa shule na mzazi mwenzangu lakini jioni nikakuta timbwili sababu dogo alikua kapoteza begi lote la madaftari.

Mama ake alikua anakaribia kumuadhibu ila nlipofika nikamwambia aniachie hio kesi nimuadhibu mimi. Ilikua saa 12 hivi jioni nikatoka na dogo nikaenda kumnunulia begi jipya na madaftari ila nikampa warning kali sana hadi leo ni mtunzaji mzuri sana wa vitu vyake hasa vya shuleni.

Ila sababu kubwa ni kwamba mimi mwenyewe siku ya kwanza napelekwa shule miaka hio nliibiwa mfuko wote wa madaftari, na kwenye madarasa ya mbeleni niliibiwaga viatu na begi sabab nlikua nmevua nimeweka pembeni tunacheza mpira, game likanoga kuja kumaliza mchezo nilishaibiwa kila kitu nikarudi nyumbani peku af bila madaftari. Yaan nlipofikiria hilo nikakosa kabisa confidence ya kumuadhibu dogo.

Ww mzazi au mlezi ulishaona mwanao kafanya kosa gani ila ukakosa hata confidence ya kumuadhibu sababu na wewe yalishakutokea.

NOTE: Ni makosa madogomadogo tu ili tuburudishane, makosa makubwa lazima mtoto aadhibiwe hata kama mzazi nilifanya sababu nishajua madhara yake.
 
Kalinilamba makofi ya uso nikiwa nimelala, nikikaangalia kana mwaka mmoja, nikasema hata ingekuwa ni mimi kipindi hicho nataka kumwamsha mtu afu siwezi kuongea I'll do the same. Nikaamka tukaanza kucheza wote.
 
Kupiga wenzake, mimi nilikua ngumi jiwe, kesi kama zote
Kupiga wenzake ataacha hukohuko. Mie nakumbuka nilikua mbabe sana akaja dogo mpya wakaniweka nae zile za kuweka mchanga viganjani then mkivipiga wote ngumi zinaanza. Aisee nilidundwa balaa na yule dogo hadi sikwenda shule kesho yake kisa aibu. Ila tukaja kuwa marafiki sana baadae.
 
Mi mtoto ukifanya kosa lolote unapigwa haijalishi ninewahi lifanya au la
 
Kupiga wenzake, mimi nilikua ngumi jiwe, kesi kama zote
Umenikumbusha enzi hizo niko Mkoa wa kanda maalum shuleni nikitokea mikoa ya Pwani, nilikuwa napiga ngumi kwa mbwembwe za sarakasi zote na kushinda, shida kuu kwa Watu wa kabila lile hata ukimpiga akatokwa na damu au hata akazimia ila kesho mkikutana naye tu mnaanza upya hadi siku utayokubali wewe kushindwa.

Niliona najijengea maadui wengi tu na visa visivyoisha hadi niliamua kuwa mpole mwenyewe ndipo nilipopumzika kupigana.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Mwezi uliopita nileletewa kesi kijana wangu wa Form 2 kakutwa bweni la wanawake mida ya prep.

Nilikwenda shule nikayasuluhisha kwa kuridhia dogo apewe adhabu ya kufyeka shamba la shule lakini ndani ya nafsi yangu wala sikuchukulia ni kosa kubwa.

Nilipokuwa kidato cha nne kuelekea mitihani ya taifa wakati wenzetu wanajisomea mimi na mshkaji wangu tulishapanga miadi na wenza wetu.

Walitupa mabaibui yao tukayavaa ili tuingie kama wasichana na kwenda katika fungate mabwenini kwa mademu.

Bahati mbaya kulikuwa na vitoto vya pre form one, vilipotuona vikapiga kelele. Matron akaja na kutukuta na mabaibui yetu bila mitandio.

Kuliitishwa assembly ya dharula muda huo huo mimi na mwenzangu tukasimamishwa mbele ya shule tukiwa na mabaibui yetu. Na yule matron alivyokuwa mkuda akasema tufunge na mitandio kabisa.

Kilichotuokoa kutokufukuzwa shule ilikuwa tunajimudu kichwani ila tulikula mboko karibia kutoka kwa kila mwalimu.

Tukio la kijana wangu nilichukulia kama maji hufuata mkondo tu. Japo nilijifanya kumkanya na kuzuga kuchukia lakini ndani ya nafsi yangu nilikuwa nacheka tu.
 
Kijana wangu kusababisha mimba kwa, mabinti wawili katika umri ule ule ambao mimi baba yake niliharibu.

Japo kupitia uharibifu huo hahaha alipatikana yeye, ambae najivunia sana sasa.
 
Mwaka jana dogo alipata kesi ya mapenzi shule alikamatwa kapakata mtoto wa kike na kumla mate, kufika shule walimu wakakomaa nirudi na mwanangu siku 21,nikapiga hesabu nikaona ngoja nijitoe ufahamu kidogo.Nilichapa fimbo na ushauri kibao mpaka walimu wakaingilia kati na kufuta adhabu hivyo akabaki shule ila sasa nilipomwona binti mwenyewe aliyepakatwa nikaona hata ingekuwa mimi enzi za barehe ningemla tu.
 
dogo ni legend, kazi na dawa.
 
Kijana wangu kusababisha mimba kwa, mabinti wawili katika umri ule ule ambao mimi baba yake niliharibu.

Japo kupitia uharibifu huo hahaha alipatikana yeye, ambae najivunia sana sasa.
bao lako kabisa hilo, mtoto wa nyoka ni nyoka
 
Mwezi uliopita nileletewa kesi kijana wangu wa Form 2 kakutwa bweni la wanawake mida ya prep.

Nilikwenda shule nikayasuluhisha kwa kuridhia dogo apewe adhabu ya kufyeka shamba la shule lakini ndani ya nafsi yangu wala sikuchukulia ni kosa kubwa.

Nilipokuwa kidato cha nne kuelekea mitihani ya taifa wakati wenzetu wanajisomea mimi na mshkaji wangu tulishapanga miadi na wenza wetu.

Walitupa mabaibui yao tukayavaa ili tuingie kama wasichana na kwenda katika fungate mabwenini kwa mademu.

Bahati mbaya kulikuwa na vitoto vya pre form one, vilipotuona vikapiga kelele. Matron akaja na kutukuta na mabaibui yetu bila mitandio.

Kuliitishwa assembly ya dharula muda huo huo mimi na mwenzangu tukasimamishwa mbele ya shule tukiwa na mabaibui yetu. Na yule matron alivyokuwa mkuda akasema tufunge na mitandio kabisa.

Kilichotuokoa kutokufukuzwa shule ilikuwa tunajimudu kichwani ila tulikula mboko karibia kutoka kwa kila mwalimu.

Tukio la kijana wangu nilichukulia kama maji hufuata mkondo tu. Japo nilijifanya kumkanya na kuzuga kuchukia lakini ndani ya nafsi yangu nilikuwa nacheka tu.
Hahahaaaa hatari sana. Mbususu haijawahi kumuacha mtu salama
 
Back
Top Bottom