Wazazi wa Azory Gwanda watuma barua kwa Rais Samia Suluhu Hassani

Wazazi wa Azory Gwanda watuma barua kwa Rais Samia Suluhu Hassani

Kutoweka kwa huyu mwandishi kunatatanisha kwani hata haijulikani alikuwa akiandika au akitafuta taarifa juu ya kitu gani ambacho kingeweza kuwa ndiyo sababu ya kutoweka kwake.

Hivi huko Mwananchi nao hawajui alikuwa akishughulika na habari gani?

Je kwenye magazeti ni habari zipi alizokuwa anaziandika, ili tujaribu kuunganisha doti?.

Hii ni tofauti kabisa na kutoweka kwa Ben Saanane, ambaye habarizilizosababisha apotee zinajulikana wazi.

Mkuu ina maana hujui alienda Kibiti kupeleleza lile saga la wakati ule wa kibiti?
 
Akihojiwa na chombo cha habari,mke wa Azory kinachomuumiza ni swali analoulizwa na mwanaye kuhusu baba yake alipo maana alimwambia baba atarudi.Kumbuka huyu mtoto alikuwa tumboni wakati baba yake akichukuliwa na magaidi.
Ni maumivu zaidi.
 
Wazazi wengine nao ni hovyo kabisa sasa hawa walikuwa wapi siku zote toka mwanao atoweke utafikiri huyo mtoto walimchuma mtini.

Wale wa Beny Saanane ndio kabisa hata habari hawana utafikiri walimtoa kafara mwanao. Hizo ndizo "Legacy" za huyu dikteta Magufuli, rais wa hovyo kuwahi kuonekana katika nchi hii.
Mkuu wangeanzia wapi?
 
04 June 2021



Baada ya kauli za kupingana kati ya ile ya waziri Prof. Palamagamba Kabudi wa serikali ya Tanzania alipohojiwa na BBC Swahili na ya msemaji wa Mkuu serikali ya Tanzania Dr. Hassan Abbas kuhusu kutoweka kwa mwandishi wa habari Azory Gwanda hapo mwezi November 2017.

Msemaji wa serikali Dr. Hassan Abbas alisema serikali iliyokuwa chini ya hayati rais John Pombe Joseph Magufuli inafanya jitihada zote kujua kuhusu kutoweka kwa mwandishi Azory Gwanda.

Wazazi wa Azory Gwanda wameomba msaada wa serikali ya Mh. Samia Suluhu Hassan rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iendelee kufuatilia kujua taarifa kamili juu ya suala la kupotea mwandishi huyo wa Mwananchi Media Corporation ili ieleweke kilichompata mwandishi huyo ili wazazi na familia ya Azory Gwanda wafahamu yaliyomkuta kama bado yupo hai au amefariki .

Chanzo: CHADEMA MEDIA TV
Aibu. Barua wameandikiwa na CHADEMA imesomwa hazarani na mtu wa CHADEMA, mbele ya kikao cha Kigalia wa CHADEMA. Aibu kwa ndugu yenu, msikubali kutumiwa. Azory Gwanda aliajiriwa na magazeti ya Kenya kama mtaalamu wa breaking news kila wakiuliwa polisi na makada wa CCM na magaidi Kilwa Lindi, lakini CHADEMA na CUF na TLS hawaguswi. Mnyika akasema Bungeni "CCM ni kosa lao kwa vile hawataki kuleta tume huru, wamejitakia" (a real smart fellow, Bunge lililofuata akaona kuna kiza mbele hakugombea). Leo familia inalaumu Serkali badala ya kuishukuru kuwafukuza magaidi? Ndugu yenu hatujui yuko wapi, waulizeni Waajiri wake walifaidika sana na breaking news zake. Walau basi waombeni wawasomeshe watoto wake na kuwalisha wazazi wake. Aibu.
 
Back
Top Bottom